RIWAYA JELA YA KICHAWI SEHEM YA KUMI NA TATU FANYA USIUKOSE HUU UHONDO

RIWAYA JELA YA KICHAWI
MTUNZI GADI MLWILO
SEHEM YA KUMI NA TATU

ILIPOISHIA.......

Siku zote tulizo ishi mle ndani
nilikuwa nikimridhisha Ramadhani
ikafika kipindi nikaanza na mimi
kunogewa na ile michezo. Siku tatu
zilipopita tulipelekwa sehemu na
kukabidhiwa nguvu za kichawi na
kuchemshwa
kwenye vyungu siku nzima “sasa
mmekuwa watu wakubwa sana na
mnaweza
kuondoka na kuishi maisha myatakayo”
tulikabidhiwa watu wakutusindikiza
mbaka kijijini kwetu.

Watu walifurahi sana kutuona
tumerudi salama na tulikuwa na nguvu
zingine ambazo kwa pale kijijini
hakuepo mtu hata mmoja alifikia nguvu
tulizopewa kule chini ya baharini.

Tulifikisha salaam zote tulizoagizwa na
kuingia ndani kupumzika wale watu
waliokuwa wametusindikiza waliondoka
na kurudi nchini kwao Kenya.
Wakati wa usiku tukiwa ndani
tumetulia na mke wangu Janeth ambaye
ni mama kijacho mlango uligongwa aliingia mwanamke mmoja kutuletea chakula, wakati tunakula tuliendelea kufulahia maisha “darling mi sitaki kuishi humu ndani” Janeth aliongea kwa kudeka “sasa tutaishi wapi mamaangu?” “mimi nataka twende Dar Es salaam tukatafute nyumba tuilete huku kwa uwezo tulionao” “waaaau wazo zuri sana mke wangu, kesho alfajiri itabidi twende tukatafute na jioni turudi nayo”
tulifurahi sana na kufurahia penzi letu.

Asubuhi alfajiri tuliaga tunaenda
Dar es salaam kutafuta nyumba,
wazee wakawa wanashangaa “vipi
mnahama?” lilikuwa ni swali la mzee
Kibito “hapana tutarudi usiku” walitamani kutuzuia lakini kwa uwezo tulionao hawakuweza kuzuia safari yetu, tulianza safari na moja kwa moja tulielekea Dar es salaam Masaki.

Tulipofika tulizunguka huku na
huko tuka ziona nyumba kama mbili
ambazo ni nzuri na zilikuwa na ulinzi
mdogo katika ngu zetu “sasa mke wangu nyumba ile nimeipenda lakini itabidi tuichukue kwa staili ya kuteketeza kwa moto” “sawa mimi nakusikiliza wewe tu” tulikaa katika sehemu ya kivuli na kusubili ifike mida ya saa 10 kazi ianze “unajua tuna kazi nzito sana
kwahiyo tugawane majukumu wewe
inabidi ulete mvua kali na radi na
nitakachofanya mimi nitailipua nyumba
kwa moto kisha tutabeba nyumba na
kuwachia kivuli cha nyumba” “sawa”
tukawa tumekubaliana hivyo.

Geti la ile nyumba lilifunguliwa,
kuna gari aina ya Benzi rangi
nyeupe lilitoka mbele alikaa mwanamke
na watoto wawili walikuwa wamekaa
kwa nyuma. Walielekea barabara ya kwenda upanga, tuliruka hewani bila kuonekana na mke wangu akaanza kazi ya kukusanya maji ya bahari na kuruhusu mvua kubwa ianze kunyesha.

Jiji la Dar es salaam mvua kubwa
ilinyesha ikiambatana na radi kwa
takribani saa moja upepo ulivuma kuna
nguzo ilikuwa karibu na ile nyuma
nikaisukuma na kuiangusha ili
kuwafanya watu wasifikirie vibaya.

Nilianza kuivuta ile nyumba
nikafanikiwa kuingoa giza lilikuwa
limetanda watu walijifungia ndani
ikabidi niwashe moto lile eneo na
kuondoka na ile nyumba.

Tulifanikiwa kufika kigoma katika
kijiji chetu na kutafuta sehemu
na kuisimika ile nyumba, watu
walikuwa kichanjani wakian daa
chakula cha usiku lakini baada ya kusikia kishindo walikuja mbio nakushangaa jumba tulilokuja nalo.
Wengi walitupongeza sana na
kuomba tuwafundishe njia tuliyo itumia
tuliwafundisha kiroho safi na wengi
walielekea maeneo ya karibu na kuleta
nyumba zilizo vutia.

Ilifika kipindi niliheshimika sana
pale kijijini na baadhi ya watu
waliniogopa, nilijikuta nimekua mchawi
mkubwa sana nchini na maarufu
kutokana na vikao mbalimabali nilivyo
kuwa naalikwa nchi mbalimbali.
Katika safari za vikao vyote nilizidi
kukutana na Ramadhani Abdul
Ramadhani ambaye nilikuwa nalala
naye na kuendelea kufanya naye
mapenzi kinyume na maumbile Ramadhani alikuwa ananipenda sana na kunifanya nianze kufanya nianze kuwatongoza wanaume na kuwaonga pesa ili niwafanyie michezo
michafu na kwa kuwa mke wangu
alikuwa anakaribia kujifungu basi
nilizunguka sehemu nyingi na kuishi maisha ya kishetani sana.

Nilipokuwa kigoma nasubiri siku za
kujifungua mke wangu nililetewa
taarifa kuwa Ramadhani Abdul
Ramadhani amefariki Dunia kwa ugojwa
hatari wa UKIMWI katika hospitali ya Kenyata Busiku wa kuamkia hiyo siku.

Hakuna maoni