RIWAYA: JELA YA KICHAWI
MTUNZI: GADI MLWILO
gamidizzle@gmail.com
insta @gamideetz
Majira ya saa saba mchana tulikua kama
kumi na mbili tukifanya kazi
ngumu bila kupumzika, afande mwita alikua
ametulia pembeni akituamlisha
mara kwa mara kufanya kazi bila huruma na kwa
maneno machafu.
“Mzee Ally waletee maji hawa” ilikua sauti
ya afande Mwita
akimwamura mzee mmoja ambaye kwa pale
gerezani tulipenda kumwita babu Ally
kutokana na umri wake. Mzee Ally alielekea
yalipokua mapipa ya maji ili
kuchota maji aweze kutugawia kama alivyo
agizwa.
Upepo mkali ulivuma kutoka kule alikokuwa
mzee Ally wote tukalala
chini “mamaaa mamaaa….” Ilikua nisauti ya babu
Ally akilia huku akielea
juju, gafra giza zito lilitanda angani ngurumo za
radi zilisikika woga
ulinishika nikajikunyata mithiri ya nyoka
anayetaka kuruka.
Baada ya muda mfupi hali ilianza kurejea
tena lakini babu Ally
hakuonekana tena, tulirudishwa katika chumba
chetu tukiwa tumechanganyikiwa
sana. Nilikua nina kama siku nne toka kipindi
nimefika pale gerezani lakini
nilikua sielewi lile gereza lilikua la kipekee sana
milango haifungwi
lakini haikuwezekana kutoka njee.
“hivi inakuaje hii?” nilimtupia swali jaamaa
aliyefahamika kwa jina
la David “bwana mdogo sisi ni mateka wa
wachawi na inavyosemakanika watu
wanao tufahamu wanaamini tumekufa”
tumekufaa!!!!!!!” nilimdakia kwa
mshangao bwana David “ndio na tulishazikwa
kwa kabisa kwani wewe imekuaje
mbaka ukafika hapa?”.
“kumbukumbu zangu nilikua nikiamishwa
gereza la Ukonga Dar es salaam
kwenda gereza la kigoma kwa treni, wakati tukiwa
safarini tukianza kuingia
Kigoma mvua ilianza kunyesha upepo mkari
ulivuma radi zilipiga mfurulizo
treni lilianza kuyumba na kwa bahati mbaya Treni
(gari moshi) likaanguka na
hapo sikuelewa kitu chochote mbaka nikajikuta
humu ndani” nilikua
nikimwaadisia David huku nikitetemeka “basi ile
ajari ilikua ni tiketi yako
ya kuja huku kutumikishwa kazi” davidi alikuwa
akinieleza kwa hisia, “sasa
wewe umejua vipi haya?” “kunaaskari alitwambia
yote yanayoendelea gerezani
na alipogundulika walimla nyama”.
Mwili ulianza kufa ganzi nikajikuta
nimeanguka chini baada ya
kuishiwa nguvu mwilini. Baada ya muda kadhaa
fahamu zilianza kunirudia
nikawa katika msongo wa mawazo hasa
nikimkumbuka mamaangu kipenzi na
mchumbaangu aliye uwawa kikatili na kesi
nikapewa mimi “ baraha gain hili
tena?” nilijisemea mwenyewe akilini.
Zilisikika nyayo za watu wakitembea kuja
kwetu “huyu kijana kuna
muda alianguka na kupoteza fahamu” alikua ni
afande mwita akimwonyesha mtu
mmoja aliyeogopwa sana pale gerezani huku
ameninyoshea kidole “beba peleka
CHIKATE” aliamurisha yule afande wakaja jamaa
wanne walio jazia mithili ya
John Sina na kunipeba juju juju nililia kama mtoto
wakati wao wakicheka kwa
furaha sana.
Tulifika sehemu na wale jamaa wakawa
wameniweka chini nakuanza
kufukuzana wakigombaniana kitu ambacho
sikukijua, niliona ndio sehemu yangu
ya kujaribu bahati yangu niliinuka nakuanza
kukimbia, nilikimbia umbari
mrefu bila kutokezea barabarani wala katika
makazi ya watu.
Kwa mbali niliuona kama moshi ukifuka kwa
juu ikabidi nielekee kule
labda nigeweza kusaidiwa, niliona nyumba nzuri
zikiwa bondeni ila sikuona
mutu yeyote “ha-ha-ha-ha-ha-haa” walikuwa
wale jamaa waliokuwa wamenibeba
wakicheka nilitamani ardhi inimeze nisionekane
machoni kwao.
Walinikamata na kunifunga katika miti
iliyopangwa kama kichanja na
safari ya kule kule bondeni nilikokuwa nataka
kwenda ndiko tulikoelekea,
“anaweza akatumika kesho eh?” “mmmh sidhani
maana bado wapo kama saba hivi”
“natamani sana hata angetumika leo huyu”
sikuzielewa stori zao ila zilizidi
kunitisha na kunichanganya akili yangu.
“mamaaaaaaaaaah” nililia nilipoona kichwa
cha mtu kimeshikwa na mtoto
akichezea kwa mbele ngozi ya binadaamu ilikuwa
imeaanikwa, wale jamaa
wakawa wanacheka sana “aaaaaaaaah” nililia
tena baada ya kubamizwa chini
kama mzigo wa kuni mbaka vumbi likatoka.
“CHIKATEEEE” mmoja wa wale jamaa
aliongea hilo neno kwa sauti ya juu,
baada ya muda mfupi watu waliwasili na
kunizunguka “ha-ha-ha-ha-ha-ha”
kilikua ni kicheko cha mama mmoja wa makamo
akinisogelea wakati nimelala
pale chini “kijana unaitwa nani? Na ni mwenyeji
wa wapi?” alinitupia swali
yule mama “naitwa Joseph Mponzi wa Iringa
Ndolezi” “mponzi…!!!!!!!”
aliitikia kwa mshangao kama alinijua vile
“Ndolezi, Mponzi!!!” alijisemesha
huku akishika kichwa “vipi unamfahamu? Mzee
mmoja alimtupia swali lakini
akakana kwa kutikisa kichwa “mpelekeni kwa
wenzake”.
Alisogea binti mmoja akiwa ameziba sehemu
zake za siri tu huku kifua
chake kikiwa wazi alikua anaumbo zuri
hatasikumwelewa kwanini aliyachagua
maisha yale hali alikuwa mzuri kiasi kile hata
angeamuwa kugombea miss
Dunia yawezekana angeweza kushinda, yule binti
alikuwa na bilauli mkononi
na mkia kama wa ngombe, aliuchovya ule mkia
na kunipiga nao usono kisha
wale jamaa wakanibeba na kunipeleka waliko
agizwa.
“Joseph!!!!!!” “babu Ally!!!!” nilishangaa sana
kumkuta babau Ally
katika kile kibanda cha miti kilichokuwa wazi na
upande mwingine ulizibwa
kwa maboksi, Babu Ally alinikumbatia kwa nguvu.
“vipi kijana?” “mzee nashindwa kuelewa
kwanini wanatufanyia hivi
hawa watu na umefika vipi huku babu?” “mjukuu
wangu kama nilivyo chukuliwa
vile pale shambani” tuliongea mambo mengi sana
na babu Ally nikawa nalia tu
“kijana vumilia, kulia haina maana yeyote ile sisi
ni vitoweo tu kwa hawa
mbwa…..” “no Kimoti usiseme ivyo jambo la
msingi nikuangalia tunajinasua
vipi mikoni mwa hawa watu” yalikua ni
mabishano ya Kimoti na Chazi ambao
walikua ni wafungwa nilio wakuta mle ndani na
nilipokua kule gerezani
nilisikia stori zao kama nao walikuwa pale na
walichukuliwa katika
mazingira tatanishi.
Niliwaza mambo mengi sana, usingizi
ukanipitia nikaja kushitushwa na
kelele za watu nnje “vipi tena??” niliuliza wenyeji
wangu “shiiiiiiiiiii
ndo mida yao ya kula hii subiri uone maajabu”
Kimoti alinijibu nikawa
nasubiri nione nini kitafanyika.
Watu walikusanyika pale nnje ya kile kibanda
watoto, vijana, watu wa
makamo na wazee mkononi wakiwa na sahani.
Ililetwa miili ya wanawake wawili
na kulazwa chini ikiwa uchi wa mnyama
“Bony…..” “naaam” “Sonyo…” “naaam”
“haraka fanyeni ibada watu waweze kula
tumechelewa leo” alikuwa ni mama
mmoja akiamrisha ibaada ifanyike.
Walitokea njemba wawili waliojazia wakiwa
nao kama walivyo zaliwa na
chupa mikononi. Walitoa vitu katika zile chupa na
kupaka katika nyeti zao
na kupaka katika sehemu za siri za ile miili ya
wale wanawake, sikuamini
tendo linalotaka kufanyika wakati ule, yani hata
mshipa waaibu hawakua nao
wale jamaa wakaanza kufanya mapenzi na zile
maiti “mamaaaa hivi hawa jamaa
wakoje?” “subiri kijana bado utaona makubwa
zaidi” babu Ally alinijibu kwa
sauti ya upole.
Tukiwa bado tunashangaa nnje mlango wa
kile kibanda ulifunguliwa ,
aliingia Yule kisura aliye nipiga na mkia siku ya
kwanza nafika pale
“Joseph njoo” nikaanza kutetemeka akanisogelea
na kunishika bega nilijikuta
nipo juu ya mbwa akikimbia porini kwa woga
nikawa nimemkumbatia nisianguke.
“ashilaaaaashi” Yule mrembo aliongea kitu
nisicho kijua Yule mbwa
akasimama tukashuka “tukae pale” alionyesha
kwa kidole, tukaketi kwenye
gogo “naomba usiniogope” nikatikisa kichwa huku
hofo ikinitawala “nimesikia
wewe ni mtu wa Mafinga” aliniuliza swali “ndio”
mimi naitwa Janeth ni mtoto
wa pekee katika familia yetu naaaaa ni mzaliwa
wa Iringa Ndolezi”
nilishituka kusikia vile “na wakati nikiwa mdogo
wazazi wangu walifukuzwa
pale kijijini wakidhaniwa ni wachawi” nilikumbuka
kitu kilichotokea miaka
ya nyuma pale kijijini “inamaana wewe ni mtoto
wa Kinyunyu?” “ndio”.
Nilikumbuka nilipokuwa mdogo nilikuwa na
rafiki aliitwa Janeth, Janeth
alisimama na kunikumbatia “Jose wewe ni rafiki
yangu wa utotoni na siku
zote nilikuwa nakufikiria sana” aliongea Janeth
kwa sauti ya chini huku
machozi ya kimtoka “usijari naomba usilie”
nilimbembeleza Janeth akiwa bado
amenikumbatia mwili wangu ulianza kusisimka
kwa joto nililo lipata kutoka
kwa Janeth na hasa maziwa yake yalivyo kua
yamesimama yakinichomachoma
kifuani kwangu.
Janeth alikuwa ni mrembo wa Dunia pasipo
kujijuwa, umbo lake jinsi
lilivyo umbika utazani kajitengeneza mwenyewe
Janeth alikuwa ni mzuri kiasi
kwamba ukisema umwelezee sifa zake utakesha
kwa kusimulia bila kummaliza.
“Janeth” “abee” aliitika kwa sati ya chini
“baba mbona sijamwona yuko
wapi?” “mama alimtoa kafara ili yeye amiliki
himaya ya kichawi pale
kijijini” alinijibu kwa huzuni zaidi “inamaana yule
ndio mamaako mzazi?”
“ndio na ninamchukia sana mama kwa kumuua
baba” “Janeth nahitaji msaada
wako na sikia sisi ni wakufa tu katika kijijini
chenu?” “usijari mimi
ntakusaidia na nimefurahi sana kukuona na
ningependa siku moja tuishi
pamoja, naaaah muda umeenda tutaongea kesho
twende tuondoke” nilitaka
nisirudi tena kule kijijini lakini Janeth alinishika
bega nikajikuta nipo
ndani ya kibanda.
Wakati Janeth anatoka mlangoni kulikua na
mbwa mweusi amekaa “mama!!!”
Janeth aliita kwa mshangao, yule mbwa
akabadilika na kuwa mtu niliogopa
kumwona yule mama “umetoka wapi?” “ndani”
Janeth alimjibu mamaake huku
akiondoka “wewe kuja hapa” yule mama aliniita
akininyoshea kidole mimi
nilimsogelea huku mwili ukitetemeka “mimi
unanikumbuka?” aliniuliza swali
nikakataa kwa kutikisa kichwa “aah haa safi
umekua kijana mzuri sana na
endapo utafwata masharti yangu basi huto kufa”
aliongea maneno yasio
eleweka na kuondoka mle ndani.
Nnje watu walikuwa wachache ilinibidi nianze
kuwaeleza yalio tokea
huko niliko kuwa na Janeth “dah afadhari
mwenzetu hutokufa” kimoti aliongea
maneno ya huruma sana “usiseme hivyo kimoti
jambo la msingi tuangalie
tutajitoa vipi humu kibandani mbona bado tupo
pamoja?” “ni kweli” Chazi
alinisapoti kwa niliyoyaongea naye.
Ilikua asubuhi tulishitushwa na kelele za
watoto nilipoangalia nje
nilistuka sana kuona watoto wakikimbia angani
huku wakigombania kichwa cha
binadamu, kwa mshangao niliwatazama
wenzangu nikagundua kimoti alikuwa
akilia uso wake ulilowa machozi “Kimoti vumilia
brother, amini yatakwisha”
“hapana mdogo wangu sifikirii kifo changu ila
naikumbuka familia yangu
istoshe mke wangu nilimwacha na ujauzito
sielewi wapo vipi na wanaishi
vipi….??” Kimoti aliongea kwa uchungu sana
mbaka alinitoa machozi “jamani
kila mmoja anamakubwa yake hapa sasa sidhani
kama kulia kutasaidia jambo la
msingi tuangalie tutajiokoa vipi” aliongea babu
Ally kwa ujasili wa
kulazimisha kama hakuwa na hofu moyoni
mwake.
Walikuja jamaa wanne kutuchukua
nakutupeleka kufanya kazi za kukanda
udongo mfinyanzi wa kutengenezea vyungu,
wakati tukikanyaga kanyaga ule
udongo kuna mabinti walikuwa wanaleta maji
ilikufsnikisha zoezi la ukandaji
udongo, katika wale mabinti kuna dada mmoja
alikuwa akiniangalia sana
nikahisi labda ananifananisha, tulifanya kazi kwa
muda mrefu sana tukawa
tumechoka, walileta chakula cha ajabu utafikiri
nguruwe ndio anakula lakini
kutokana na njaa ilitubidi kula hivyo hivyo.
Tulipomaliza kula tukarudishwa
katika kibanda chetu.
Jioni ilikuwa imewasili kama kawaida yao
walifika katika kichanja
chao kwaajili ya kafara waliimba nyimbo za
ajabuajabu siku hiyo huku
wakicheza na kugongana makalio “ngeeeeee
ngeeeee” ilisikika sauti kama ya
kengele watu wote wakakaa kimya “kuna mmoja
amesaliti, na kanuni zetu zipo
wazi kwa watu waaina hii” aliongea mama
Janeth kwa sauti ya juu “afande
Peter!!!!!!!” wote tulishituka kumwona afande Peter
ameletwa mzega mzega
“oooooooooh” kele za shangwe ziliibuka upya.
Walimlaza kichanjani afande Peter na kazi ya
kumtengeneza ikaanza
“jamani sasa…” wakati nikiongea nilikatizwa na
mrembo Janeth, aliingia
ndani na kunikabidhi kitu kama tunda lakini
sikujua ni tunda gani “kula
Jose” nikabaki nimeduwa tu nilipomtazama babu
Ally alitikisa kichwa ishara
kukubaliana na nilichoagizwa nikala, sijui ni seme
ni tunda? Maana lilikuwa
tamu sana. Janeth alinishika bega nikajikuta
nikipaa kuelekea angani.
“usiogope wewe ni mtoto wa kiume” “mtoto
wakiume ndo haogopi kufa?”
“hapana siwezi kukuacha ufe Kapolisi wangu”
alinitania kwa kuniita jina la
utotoni Kapolisi basi tulicheka sana tukawa
tunaelea juu juu huku
tukikumbushana mambo mengi ya utotoni yalivyo
kuwa.
Kila nilipo mtizama Janeth alivyo umbika
mwili wangu ulikuwa
ukisisimka basi na vile alivyokuwa akinishika
shika basi nikasahau shida
zangu na kama nipo juu angani. Michezo ilizidi
ikatupelekea mbaka kufanya
mapenzi kule angani.
Kwajinsi alivyokuwa Janeth nilimpa mambo
makubwa na zaidi
nilimpagawisha nilipomnyonya sehemu x zake
hapo ndipo Janeth
alipochanganyikiwa kabisa. Alinishukuru sana
kwa mambo niliyo mpa zaidi
akawa anasisitiza nije kumwoa siku moja ili awe
mke wangu, wakati kwa
upande wangu nilimwomba anisaidie kunitoa
katika kile kifungo cha kichawi,
tulipo maliza tukarudi tena chini akiniacha
kibandani.
Nnje bado kulikuwa kuna watu wakati mwili
wangu ulikuwa umechoka sana
kutokana na mechi iliyofanyika kule angani,
nilitamani nipate maji ya kuoga
lakini hakuwezekana “eh hee vipi huko utokako?”
lilikuwa ni swali la babau
Ally “kwema ila nasikitika nimefanya mapenzi na
huyu mwanamke” “eheeeeee”
wote walishituka “ndio lakini halikuwa kusudio
langu” “mmmh” aliguna kwanza
babu Ally “mjukuu wangu pole sana yawezekana
nyota yako ni nzuri kwao kwani
mara nyingi mchawi akifanya mapenzi na
binadamu wa kawida yeye kwa upande
wake huongeza nguvu” “njoo we kijana” alikuwa
ni mama Janeth akiniita
nilisimama kwa woga.
Mam Janeth alininyooshea mkono nikajikuta
nipo kitandani kwake
“usiniogope kijana, na kama nilivyokwambia
ukifwata masharti yangu utaishi
maisha marefu” alizungumza huku akivua nguo
zake nilianza kutetemeka na
nikikumbuka maneno ya babu Ally ya kunyonywa
nguvu basi nikaamini
inawezekana na labda ndio lengo lao.
Mama Janeth alikuja kitandani na kuanza
kunishika shika “kwanini
unanifanyia hivyo lakini?” nilimtupia swali lakini
hakunijibu akaendelea
kulamba lamba mwili wangu “basi naomba
uniache kwa leo tufanye
sikunyingine” “hapana kijana muda ndo huu nipe
japo kidogo” “sijisikii
vizuri” nilijitetea kwani nilikuwa nimechoshwa
sana na mechi ya mwanae ila
alizidi kunipapasa mwili wangu, alipofika sehemu
nyeti alianza kunyonya kwa
ustadi wa hali ya juu nikajikuta nikitoa miguno ya
maraha “lakini
utaniachia?” “endapo utafwata maagizo yangu”
Maneno yale yalinifanya nipate moyo
wakumwonyesha uwezo wangu nikidhani
nitapona, nilianza kuuchezea mwili wake na
baadaye kwa kumdatisha kabisa
niliamua kuzama chuvini ambako kulimfanya atoe
milio kwasauti kubwa usiku
ule. Nilipoona ameiva na yupo tayari kwa kuliwa
taratibu nikaanza kumpa
myoto na kwa kuwa nilitoka kwenye mechi na
mwanae basi haikuwa raisi mimi
kufika mlimani wakati yeye alienda karibu mara
mbili na mara ya tatu ndipo
tukaenda wote tukuwa tumechoka sana
tukajitupa kitandani.
“nashukuru sana kijana kwa penzi lako tamu”
sikujibu kitu nikawa nawaza
vipi akijuwa na mwanae nimetembea nae
“nitafanya kila liwezekanalo uje
tuishai humu ndani ili nikufaidi zaidi” nilishituka
“kwani siulisema
utaniacha huru?” “yaah endapo utaamua kuwa na
mimi. Naona muda umeenda hebu
nikurudishe sasa” sikumjibu chochote nikajikuta
nipo kibandani.
Niliwakuta Chazi, Kimoti na babu Ally wakiwa
wamelala, kichwani mawazo
mengi yalinitawala nikajikuta nalia mwenyewe “eh
mwenyezi Mungu nimekukosea
nini mimi?” nilijiuliza maswali bila majibu sauti ya
kilio changu ikasikika
kwa wenzangu mle kibandani “vipi tena?” “kuna
nini Joseph?” maswali
mfurulizo nilitupiwa “kwani imekuaje?” “mama
Janeth naye amenitaka
kimapenzi sijui wananitaka nini hawa watu”
“kwani umefanya nae?” “ndio”
“aaaaah kwanini umefanya hivyo na hilo ndilo
linalokuliza?” hapana Kimoti
hupaswi kumlaumu tambua wachawi wana mbinu
nyingi sana” babu Ally
alionyesha kujuwa mambo mengi sana.
Niliwasimulia yote yaliyo tokea ndani kwa
mama Janeth, usingizi mzito
ulinichuku kwa uchovu nilio kuwa nao mbaka
asubuhi tulipoamswa kufanya kazi
za kukanda udongo.
Hakuwa kama siku zote tulifanya kazi kwa
muda mfupi tukarudishwa
kibandani, tukiwa tunatafakari jinsi ya kujinasua
kabla hatuja uwawa
alikuja bibi kizee mmoja na wanaume wa shoka
wane “nahitaji maini ya Yule
kijana” aliongea Yule bibi akimwonyesha kidole
Chazi, wale jamaa wakambeba
Chazi mbaka kwenye kile kichanja “mayooooo”
ilikua nisauti ya kiume ikilia
kutazama nnje niliona jamaa mmoja aliye kuwa
amembeba Chazi akigalagala
chini huku akivuja damu, Chazi aliruka na
kumkita jamaa mwingine shingoni
kwa bisu kubwa alilo lichomoa katika kile
kichanja.
Wakati anamfwata mtu wa tatu Yule bibi
alimnyoeshea mkono Chazi
akatupwa ukutani Yule bibi akainua mkono Chazi
alienda hewani na kubaki
akining’inia hewani huku akitukana matusi mazito
kwa wale wachawi.
Watu walikuwa wamewasili eneo la tukio na
kuwazunguka walejamaa
waliokuwa wamelala chini “ndugu zetu hatupo
nao tena jamani” aliongea
kijana mmoja aliyekua na mikogo mingi sana,
kilisikika kilio cha mtu mmoja
aliye lia kwa uchungu na kwa sauti ya juu “ni
nani kafanya unyama huu?”
aliuliza Yule mama aliyekuwa akilia “Yule pale”
jamaa mmoja alionyesha kwa
kidole huku watu wakiwa na majonzi sana “wewe
thamani ya kizazi chako chote
ipo mikononi mwangu” watu walikuja na
kumshika na kumwondoa eneo lile.
“tumepoteza vijana wa kazi ila sidhani kama
kimeharibika kitu na hawa
ndio milo yetu ya leo na keshoo” aliongea mama
Janeth kwaujasili lakini
jambo lililo nishangaza nilipoona watu
wanashangilia “inamaana wanawala
wenzao?” nilimtupia swali babu Ally na Kimoti
“hawa watu hawana ndugu jambo
la msingi tumwombee ndugu yetu asiliwe” mzee
Ally aliongea maneno ya busara.
Nnje yaliendelea mambo yao ya kuandaa mili
ya wenzao huku wakiimba
nyimbo za ajabu na kucheza. Mida ilikuwa
imeenda sana tukawa tuna mwangalia
Chazi gizani akining’inia hewani na watu waliketi
katika makundi huku
wakila nyama za ndugu zao mwili wangu ulikuwa
ukitetemeka sana.
Usiku wa siku hiyo hatukuweza kutoka
pamoja na jitihada za kuharibu
mlango ikabidi tujipange upya. Asubuhi ya siku
hiyo ilikucha tofauti sana
nnje kulikuwa na wazee wamekaa angani
mikononi wana glasi nyekundu wakinywa
na kucheka sana bila hofu na woga wowote kule
angani.
Ulizuka ubishani mara mvua kubwa
ilinyesha ngurumo za radi
zilisikika, lakini jambo la kushangaza wao
hawakuloa wakati kwetu mvua
iliingia ndani baada ya dakika chache giza zito
lilitanda lakini bado pale
walipokaa wale wazee kulikuwa na mwanga
“puuuuuuuuh” kilisikika kishindo
ambacho kilifwatiwa na vicheko. Hali ya kawaida
ililejea tuliona pale chini
amelala mzee mmoja walitelemka wale wengine
na kuendelea kutambiana
“nilikuambia huni wezi wewe” “bado sikubali
ngoja ntakuonyesha tu mi ni
nani”.
Siku hii ilikuwa ni siku mbaya sana kwetu
maana baada ya wale wazee
kumaliza mambo yao waliitisha watu katika
sehemu ya kafala “jamani huyu
kijana kwa aliyo yafanya sidhani kama anastahili
kuishi katika hii dunia”
bibi aliyekuwa amekuja kumchukua Chazi
aliongea huku akimwonyeshea kidole
Chazi pale alipo ning’inizwa toka jana yake “na
leo nitahitaji watoto
watuandalie huyu mtu kwa kumpiga mawe mbaka
jioni muda wa kafala
utakapofika” maneno yale yaliwafurahisha sana
watoto.
Baada ya kauli ya bibi wa kichawi kumalizika
watoto walitawanyika na
kukusanya mawe na kuanza kazi ya kumrushia
mawe Chazi, tulishuhudia Chazi
akivuja damu na kupasuka pasuka roho yangu
ilium sana. Wakati tukiendelea
kushuhudia lile tukio aliingia dada mmoja na
bakuli kubwa mkononi “kaka
samahani ninahitaji kuongea na wewe” aliongea
yale maneno huku akinisogelea.
Nilijikuta natetemeka “ naitwa Joani na
naomba usiniogope Jose”
aliongea na kujitambulisha jina huku
akinishikashika sikuelewa amelijuaje
jina langu “wee-wee-wee-wee pumbavu mkubwa”
alikuwa ni mama Janeth
aliyeongea kwa sauti ya ukali, aliwaita watu wake
“beba huyu” mama Janeth
aliwaamuru wale jamaa wamkamate Yule dada
“Joseph I love u so much”
aliongea Joani kwa sauti ya chini iliyo sikika.
Sikuweza kujibu lolote alipokuwa anatoka
mlangoni aligeuka na
kunambia tena “Jose I love u” kwasauti ya
uchungu, mama Janeth alizidi kuwa
mbogo walimpeleka Joani kwenye kile kichanja
chao cha kafara, lamgambo
lilipigwa watu wakajaa “huyu mtu asiyekuwa na
haya ameamua kutusaliti, na
adhabu yetu msaliti ni kifo na nyama yake ni
halali yetu” watu
walishangilia “na inakuaje Yule kibaka aliye niuli
mme wangu?” lilikuwa ni
swali la mama mmoja aliye onyesha kupinga na
kuonyesha hasira sana juu ya
Chazi aliyekuwa hoi hajitambui baada ya kupigwa
mawe kwa muda mrefu
“usijali binti, Yule kijana anatakiwa afe taratibu
na leo ni huyu msaliti.
Watu walipiga mayowe wakifurahia hasa
wanawake sauti zao ndizo
zilikuwa juu niliumia sana kuona Joani anauwawa
kwasababu yangu niliamini
Janeth ndio msaada wa mwisho “Janeth Janeth
Janeth” nilijikuta nikimwita
Janeth Kimoti na babu Ally wakawa
wananiangalia.
Haikuchukuwa muda Janeth aliingia “Janeth
please msaidie Joani kwani
hana kosa lolote alileta chakula humo” Janeth
alibeba bakuli hakujibu
lolote nakwenda mbaka pale kichanja “jamani
Joani hana makosa mimi
nilimtuma apelike chakula sidhani kama anahitaji
kuuwawa bila kuchunguzwa”
Janeth aliongea kwa kujiamini na watu
wakamsapoti lakini mamaake
hakuopendezewa na kile kitendo.
“jamani kutokana na pingamizi hili sioni
sababu ya kumuwa huyu binti
bila uchunguzi” watu hawakueleweka
walishangilia tena yale maneno
“kwasababu wapo wanao afiki na wasio afiki basi
tupige kura jamani”
“ndiiooooo” wote walijibu kwa pamoja. Baada ya
muda mfupi “na matokeo yetu
ni kama ifwatavyo wanaokubaliana na swala la
kuuwawa kwa Joani ni 437”
mtangazaji matokea akakaa kimya kidogo
ambapo mapigo ya moyo wangu yalizidi
kwenda mbio “na wanapinga hiliswala ni 439”
ziliibuka shangwe nyingi kutoka
kwa wanaume “kwa maana hiyo Joani
anafanyiwa uchunguzi na ratiba ya leo
itaendelea pale pale” wote walipiga mayowe.
Siku ilizidi kuharibika zaidi tulipoona Chazi
anabebwa na kuwekwa
kichanjani Janeth aliingia kibandani kwa kasi
“sasa olewako nije nijue ni
kweli kinachosemwa, nitakunywa thamani ya uhai
wako” kabla sijamjibu
aliondoka kwa hasira nilizidi kuchanganyikiwa
“hivi itakuaje siku wakijuana
na mama yake kuwa nimesha wachanganya”
nilijiuliza bila kupata majibu.
Nnje giza lilikuwa limetanda watu walikuwa
wametawanyika katika makundi
makundi wakila nyama ya ndugu yetu chazi
“jamani leo lazima tuondoke”
aliongea kimoti na kuelekea mlangoni “hee kumbe
mlango upo wazi tuondoke”
tuliinuka haraka na kuelekea mlangoni na
kufanikiwa kutoka njee.
Tuliwafungulia na wengine walio kuwa karibu
yetu na kuingia porini,
tulitembea umbali mrefu sana bila kutokezea
barabarani tulifika sehemu
ikabidi tupumzike ili kukicha safari iendelee,
usingizi ulitupitia wote
tukalala.
Wakati nimelala nilianza kuota jitu kubwa
linanikimbiza huku mkononi
limeshika panga linavuja damu utafikiri limetoka
kuuwa nilikimbia sana
nikajikwaa na kuanguka wakati linataka kuni
choma nikastuka nakuoa nipo
pekeangu huku nina hema sana “wameniacha”
nilijiongelesha pekeangu,
nikasikia kama mtu anakuja nyuma yangu nilipo
geuka nilimwona Joani
“Joani!!!!!!” niliita kwa mshangao, “unatafuta nini
huku? Na wenzangu wapo
wapi?”.
Nilimtupia maswali mfurulizo “Jose mmefanya
makosa makubwa sana kaa
mkijua hamuwezi kurudi tena duniani” maneno ya
Joani yalinichanganya
“duniani??????” “ndio, watu wengi wanaamini
kuwa nyie mlishakufa” “sasa
Joani wenzangu wapo wapi na kwanini nipo
hapa?” “wenzako wamekamatwa na
wapo katika mateso makari sana wewe
nimekuiba hivyo unatafutwa sana”
nilichanganyikiwa kusikia vile na kuona
yawezekana Joani anaweza
kunisaidia, nililia sana huku nikimwomba msaada
Joani.
Joani alinifwata na kunikumbatia “usilie
Joseph mimi nipotayari kufa
kwaajili yako nitajitahidi kukusaidia” maneno yale
yalinifariji sana na
kunifanya nimkumbatia Joani kwa nguvu
tukaanguka chini tukiwa tumeshikana
Joani alinipa midomo yake nami bila hiyana
nilifanya vile anavyotaka,
shetani la mahaba likanipanda nikajikuta
nimezama kwenye mapenzi mazito na
mrembo Joani takribani masaa manne.
Baada ya kumaliza michezo michafu
tukajitupa chini usingizi ukatubeba
wakati tumelala nilijikuta nikiamrishwa na afande
Mwita kuchimba shimo huku
amenisimamia, wakati naendelea aliibuka nyoka
mkubwa sana kutoka kwenye
lile shimo na kummeza afande Mwita kisha
kunigeukia mimi lile joka
lilijivuta na kutaka kunimeza nikashituka
“mamaaaaa” nilijikuta nipo
katikati ya watu wa mama Janeth, wakaanza
kucheka sana “ha-ha-ha-ha”.
Nilitazama huku na kule sikumwona tena
Joani, niliamini kuwa Joani
amenisaliti ameamua kuniuza. Wale jamaa
walinipiga sana na kunibeba mbaka
kijijini kwao ambako nilipigwa kipigo cha mbwa
mwizi kama waswahili
wasemavyo “aahaaaa” vilisikika vilio vya
wanawake wawili wakilia baada ya
kupigwa na gogo lililo vunjikia kichwani kwangu.
Vilio vile vilifanya
niachwe kupigwa na kuwafwata waliolia “nyie
mnamfahamu sana huyu mbwa?”
jamaa mmoja aliongea kwa ukali.
Maumivu makari yalinishika nikawa
sijitambui nilibebwa na kwenda
kufungwa walipofungwa wenzangu nikiwa
sijitambui. Usiku wa manane fahau
zilianza kurejea nikawa na hisi maumivu
nilipoangalia pembeni niliwaona
babu Ally, Kimoti na wale jamaa wanne
tuliotoroka nao wakiwa wamechakazwa
wote tulikuwa kimya.
Niliumia sana kila nikimfikiria mamaangu
nyumbani kwani maisha yao
walinitegemea sana mimi tangu baba alipofariki,
nilimkumbuka dadaangu na
kipenzi wangu Suzi tuliyekuwa tumepanga
mambo mengi sana na ni muda mrefu
ulipita nikawa natamani kuwaona.
Asubuhi ilifika tukiwa katika kamba za
nguvu huku tumening’inizwa
kama nyama buchani “hatuna budi kumwomba
Mungu atuepushe katika mateso haya
maana bora kufa tu” aliongea babu Ally kwa
shida lakini hakujibiwa lolote.
Kwambali alikuja jamaa mmoja alionekana
anahasira sana ambaye
alifika moja kwa moja kwangu na kuanza
kunichapa bila kujali nililia lakini
sauti na machozi havikutoka kutokana nililia sana
na kitendo hicho
kilimwongeza hasira Yule jamaa na kuzidi
kunipiga huku yeye mwenyewe akilia.
Watu walifika eneo la tukio na mama Janeth
akaamuru aniache lakini
haukuelewa na kuendelea kunichapa. Ilibidi jamaa
wamkamate “mniache, na
sema mniacha jamani huyu sio wakunifanyia hivi
mimi” “kwani kakufanya
nini?” “huyu sio wakutembea na mke wangu
Janeth ona amesha haribu ndoa
yangu” watu walishituka na kumwangalia Janeth
jamaa aliongea kwa uchungu
huku akilia “na kibaya zaidi wameshapeana
mimba” “eeeh!!!!!!” mama Janeth
alijibu kwa sauti ya mshangao “ndio” “we kijana
umejipalia makaa ya moto
huwezi kunifanyia hivi nikakuacha” aliongea kwa
hasira mama Janeth nikahisi
kiama changu ndio kilikuwa kimefika.
Nilimwona Janeth kwa mbali akilia “hivi
unawezaje kula kuku na
mamaake? Wewe kikaragosi wakunichanganya
mimi na mwanangu?” nilishituka
alivyo ropoka vile na watu wote walishituka,
mama Janeth aliongea kwa
uchungu sana “lazima ufe mshenzi mkubwa….”
alininyoshea mkono nikajikuta
nimejibamiza ukutani wazee wakaingilia kati
“jamani hili jambo inabidi
tukae tulijadili kwa pamoja sawa” “ngraaaaaa”
waliitikia wote. Basi
tukabebwa na kwenda kufungwa kibandani nikiwa
hoi.
Tukiwa mle ndani ya kibanda nilishangaa
kumwona Joani ameingia
akilia “pole sana Jose nilishindwa kukimbia na
wewe walinishinda nguvu”
Joani aliniomba msamaa huku akinifuta futa
damu alinibeba akawa anatoka
namimi nnje “wanatorokaaaaa” tukawa angani
sielewi tunaenda wapi wakati
nyuma yetu kulikuwa na kundi la watu
wakitukimbiza mwanga mkubwa ulitumlika
lakini Joani aliukwepa.
Hata hatukifika mbali tukawa tumezungukwa
wakaturudisha kijijini
nikaenda kuwekwa kibandani huku mwili wangu
ulikuwa katika maumivu makari
nnje ilikuwa inasikika sauti ya kilio kutoka kwa
Joani alilia kwa sauti
kubwa huku akiniita nilitamani sana niwe
nnauwezo nikamsaidie lakini sikuwa
na uwezo huo.
Nilishuhudia kuona mtu niliye mwaamini
akiuwawa kinyama mbele yangu
niliumia sana kwani Joani alikufa kwaajili yangu
watu waligawana nyama yake
na kunywa damu yake, tendo lile lilifanyika kwa
unyama wa hali ya juu “na
olewake Yule atakaye jaribu tena kitendo kama
alicho kifanya Joani”
aliongea mama Janeth kwa mkwara wa nguvu.
Nilipoteza matumaini ya kuishi, niliiwazia
sana familia yangu nyumbani
nnje kulikuwa na giza nene nilijaribu kumwita
Janeth kama nilivyo funzwa
lakini alichukuwa muda sana kufika “Janeth
najua nimekukosea sana lakini…”
“lakini nini mbwa mkubwa wewe” aliongea kwa
suti ya ukali na kuondoka
“Janeth Janeth” hakujari nakuondoka “kijana
jaribu kumwomba msamaha
atakuelewa tu hizi ni hasira” “unafikiri nifanye vipi
babu Ally unavyo
mwona hivi?” “jambo la msingi ni kumwandikia
meseji” niliona wazo zuri
kutoka kwa mmoja wa wale tuliotoroka nao.
Ulichukuliwa mkaa ukachongwa kama penseli
likachanwa boksi ukutani
nikawa nataja maneno yule jamaa akawa
ananiandikia. Meseji ilipokuwa tayari
nilianza kumwita Janeth bila kuchoka, Janeth
aliingia ndani kama upepo
“wewe ntakunyonga sasahivi” nilimrukia na
kumshika mguu “sawa Janeth mimi
nmekukosea nakuomba ukasome ujumbe wangu”
alipokea nakuondoka huku akilia.
Haikuchukuwa muda Janeth alirudi
“nisamehe mimi Joseph wangu,
nilikuwa gizani na bado ninakupenda na nitajaribu
kukusaidia kwa hali na
mali maana walipanga baada ya siku nne uwawe
kwa adhabu kari kuanzia jana
hivyo zimebaki siku tatu tu” nilichanganyikiwa
kusikia vile “sifikirii kufa
ila naomba ukawape taarifa nyumbani” “no Baby
usiseme hivyo niachie mimi”
akasimama na kuondoka.
Nilifarijika kiasi kwa wazo lile la ile meseji
iliyo andikwa
Janeth najua nimekukosea sana lakini nakiri
makosa yangu na nnahitaji
msamaa wako. Janeth katika mapenzi yetu
hukuwahi kunambia umeolewa mbaka
leo hii naingia katika mateso haya makari ila
nisamehe kwa hilo na kwa
upande mama yako yeye ndiye alinilazimisha
kufanya naye mapenzi huku
akinitishia kuniuwa endapo nikikataa naomba
unisamehe sana kwasababu
sikuweza kukueleza ukweli nilihofia maisha
yangu. Jambo la msingi naomba
ukawaeleze ndugu zangu kwamba sipo tena
duniani ila nawapenda sana na
msalimie sana mamaangu. Naomba msaada
wako na msamaha wako pia.
Ahsante Janeth na
maisha mema.
Mawazo yalinitawala kichwani hasa
nikiwakumbuka ndugu zangu nyumbani
sikufikiria kufa wala kuogopa ila niliwaza
kuuwawa kinyama na kuliwa nyama
na wale watu “kijana huna budi kumwomba
Mungu na sio kukaa na mawazo kiasi
hicho” “sawa babu” nilijibu ila sikuyatilia maanani
maneno yake.
Zilibaki siku mbili ili niuwawe na hii siku
ilikuwa mbali sana kwa
upande wetu, aliingia mzee mmoja na vijana
watatu mle kibandani “nina mtaka
yule” alimnyoshea mkono kimoti, basi walimbeba
kimoti mbaka kichanjani,
Kimoti alilia sana lakini hawakujali kabisa
walianza kukata viungo vyake
akiwa mzima mzima na kugawana, walifanya
ukatili wa hali ya juu sana
walianza kumng’oa miguu wakafwata mikono,
nilishindwa kuendelea kuangalia
nikabaki nalia pembeni kama mtoto mdogo.
Waligawana viungo vya mwili wa Kimoti na
damu iliyo tiririka kwenye
ndoo walizotegeshea chini. Sikuweza kulala ile
siku nikawa najutia biashara
haramu nilizokuwa nazifanya mbaka zikanipeleka
Gerezani.
*************
Katika utafutaji wa maisha nilikutana na
kijana aitwaye Fadhili ambaye
alikuwa akifanya biashara za madawa ya kulevya,
alianza kunishawishi
taratibu kwa kunipa pesa nyingi kwa kazi ndogo
jambo lililonipelekea kuanza
biashara ya madawa ya kulevya na baadaye
kuanza kusafiri kwenda nchi za
nnje kufwata mizigo na kuingiza nchini ili niweze
kusaidia familia yanagu
kwani maisha ya wazazi wangu yalikuwa mabaya
sana na ndiomaana
nilishawishika kwa haraka zaidi.
Nilipata dili ya kupeleka mzigo China,
mipango yote ikawa sawa usiku
nilipelekwa kwa daktari aliye nifanyia operation
na kuniweka madawa
tumboni. Safari ya kwenda china ilianza na katika
viwanja vingi vya ndege
nilipita safi lakini nilipofika China watu ambao
ilibidi waje kunichukuwa
walikuwa hawaja fika mwili ulikuwa umeanza
kupoteza nguvu na baadaye
nilianguka chini na kupoteza fahamu.
Fahamu zililejea nikiwa kitandani na mkononi
nilikuwa nina pingu
“ooooh nimekwisha” nilijiongelesha huku nikijaribu
kujifungua asikari akaja
na kunionya. Hali ilizidi kuwa mbaya ikabidi
wapige simu ubalozi wa
Tanzania ikabidi kufanyiwa utaratibu wa
kurudishwa nchini chini ya ulinzi
mkali, nilifikishwa hospitali ya muhimbili na
kupewa matibabu nilipo pona
nika somewa mashitaka na kupelekwa katika
gereza la ukonga jijini Dar es
salaamu.
Basai safari ya maisha ya gerezani ndipo
ilipoanza na kunifanye
nikutane na maswahiba ya ajabu yaliyo badilisha
kila kitu katika mfumo
maisha yangu.
***************
Ilikuwa imebaki siku moja ili kufanikisha
adhima yao ya kunitoa
kafara pale kijijini. Siku ambayo nilitawaliwa na
mawazo mengi kichwani
nililia bila kupumzika hata machozi hayakunitoaka
tena.
Usiku uliingia tukawa tunasubiri kukuche ile
siku iliyopangwa
niondolewe dudiani, nikiwa katika mawazo mazito
mlango ulifunguliwa
aliingia Janeth “ Joseph njoo” nikasimama na
kumfwata, tulienda porini
umbari mrefu sana “lala hapo subiri baba eh”
alinisubirisha akawa
anazunguka huku anazunguza maneno kwa lugha
nisiyo ijua.
Alimaliza kazi yake nakunisogelea “Jose
unahitajika kuwa na moyo wa
kiume kwa kazi inayokwenda kufanyika sawa?”
niliitikia kwa kutikisa kichwa
ingawa sikujuwa ni kazi gani “na unachotakiwa
nikukubaliana na kila kitu
kitakachotokea mbele yako, umenielewa?” “ndio”
“na huu ndio utakuwa msaada
wangu wa wewe kutokuuwawa” nilikubaliana na
kila kitu ingawa sikujuwa
Janeth anania gani na mimi “simama”
nikasimama na kusubiri kama alivyo
niambia.
Janeth aligeuka nyuma na kuanza kuongea
tena maneno ambayo sikuweza
kuelewa hata neno moja, aliponigeukia alikuwa ni
mtu aliye badilika sana
mbaka nikataka kukimbia lakini kwasababu
alinambia niwe na moyo wa kiume
ilibidi nijikaze, alinisogelea “panua mdo”
aliniamuru basi nami nikafanya
alinishika mashavuni na kutoa moshi mweusi
mdomoni mwake na kuuingiza
midomoni kwangu kwa muda wa dakika moja.
Alipo maliza liletendo mwili uliishiwa nguvu
basi nikaanguka chini
kwa mbali nilimsikia akinambia “naomba
usiniangushe Jose wangu utaniuwa
endapo hutofanya watakayokuagiza” nilijikuta
nimetokezea pangoni ambako
nilipokelewa na mtoto mdogo mwenye umri kama
wamiaka sita hivi “nifwate”
yule mtoto alinambia kwa kujiamini ikabidi
nimfwate.
Katika lile pango kulikuwa na mambo ya
ajabu sana niliona mafuvu ya
watu kulikuwa na panya wakubwa wakitembea
tembea na milio ya ajabu lakini
nikawa najikaza namfwata yule mtoto huku
nikiogopa sana tulifika sehemu
kulikuwa na giza nene sana, yule mtoto alikuwa
hana hofu hatakidogo alifika
sehemu akainama na kuinuka “shika hii”
alinikabidhi gogo na kuliwasha moto
ilikuupata mwanga.
Tulitembea kwa muda wa dakika kama kumi
katika lile giza, mbele
niliona kama ulikuwa mwisho hivi “mlango
funguka ni mimi Kashebo na mgeni
wangu” lango likafunguka nikaona madhari nzuuri
inayovutia ilionekana kama
waliishi watu mabilionea sana.
Tuliingia katika jengo lililojengwa kwa
dhahabu tupu kulikuwa na
mtu ameketi kwekiti kilichokuwa na namna ya
pekee na sijawahi kukiona
katika maisha yangu yote niliyozunguka katika
nchi mbalimbali duniani
“fanya nifanyavyo” mtoto Kashebo kama
alivyojitambulisha mlangoni alinimbia
kwa sauti ya utulivu, akapiga magoti nami pia
nikafanya vile atakavyo kisha
akaanza kusujudu nilifwata kila alichokifanya
bwana mdogo Kashebo huku
nikitetemeka.
Tulipo maliza tukainuka nilishangaa
kumwona yule jamaa pale kwenye
kiti amegeuka mzee na ameota pembe mbili
alisimama akicheka kwa kujidai
“karibu sana katika falme za dunia kijana na leo
nitakupa uwezo wa kinga
yako ya mwili kama nilivyoombwa na endapo
utakubaliana na sisi utaifaidi
sana dunia” alipomaliza kuongea kunamaneno
alinambia niyafwate vile anavyo
ongea maneno ambayo sikuyatambua mbaka na
maliza.
Nilifanya kila watakalo huku nikiyakumbuka
yote aliyo nambia Janeth
endapo nikishindwa basi atauwawa, yule mzee
alinikabidhi bilauli lilokuwa
na kimiminika chekundu kama damu “kunywa
yote” nikawa naogopa kupokea
“naomba usiniangushe Joseph utaniuwa endapo
hutofanya wachokuagiza” maneno
ya Janeth yalijirudia kichwani mwangu na
nilipokumbuka kuwa nimebakiza
masaa machache kuuwawa nililipokea lile bakuli
na kugugumia haraka
niligundua nimenyweshwa damu tena damu ya
binadamu, vicheko vilifwata
vikionyesha kufurahia lile tendo nilolifanya.
Sikujuwa kama ndio niliingizwa katika
uchawi “safi sana kijana sasa
nipe mkono wako wa kushoto” nikampa
nikijisemea liwalo na liwe, niliona
dada mmoja akija na sinia ambalo lilikuwa na
visu viwembe na vyuma vyuma
yule mzee alichukuwa kiwembe na kunichana
mkononi, nilisikia maumivu makari
nikawa na vuta mkono bila mafanikio alichukuwa
kitu kama sindano na
kuniweka pale nilipopasuliwa na kupafunika na
kiganja chake alinena kwa
lugha nisiyo ijua alipotoa nilishangaa kuona
pamejifunga na kama
hapakupasuliwa.
Nilianza kupewa darasa jinsi ya kutaka jambo
litendeke na likafanyika
kwa kuongea pale katika ile sindano mkononi
niliruka hewani nakufundishwa
mambo makubwa kupitia ile sindano mkonini
mwangu, “unaweza kwenda kijana na
unapo hitaji msaada usisite kutuita”.
Yule mzee alinishika paji la uso, “nenda
kijana” niilijikuta na
inuka pale chini nilipokuwa nimeanguka wakati
nipo Janeth, nilimwona Janeth
amepiga magoti huku amefumba macho utafikiri
alikuwa akisali, nilimshitua
katiak maombi yake kwa kujikoholesha “khooooo
khoooooo” aliinua kichwa na
kunitazama huku akitabasamu “ahsante kwa
kutoniangusha, sasa utakuwa kijana
shujaa na hakuna atakaye kuuwa tena” “kweli
Janeth?” “ndio” “jambo la
msingi fwata masharti tu na usimwambie siri hii
mtu mwingine” tukaanza
kucheza angani lakini nilihisi kama ndoto tu
“sasa inabidi tuondoke muda
umekwenda sana” “sawa” “sio sawa jibu
ngraaaaaaaaaaa” ikabidi nijibu
“ngraaaaaaaaaa” tukaondoka mbio mbaka kijijini
yeye alienda ndani na mimi
nikaenda kibandani.
Sikutaka kuwambia wenzangu yaliotokea
kwakuwa niliambiwa ni siri,
mawazo yalinichukuwa nikawa nawaza endapo
nimedanganywa alafu nikafa
“potelea pote” nilijisemea lakini sauti ikanitoka
wenzangu wakanisikia
“vipi mjukuu wangu” “hapana babu Ally
kuchanganyikiwa tu” “usijari kijana
sisi sote ni wakufa hakuna atakaye pona
naitamani sana nafasi yako ili
nijikomboe katika hiki kifungo” aliongea kwa
busara sana jamaa mmoja alieye
kuwa mle ndani “siogopi kufa hofu yangu ni
mamaangu na dadaangu kule
nyumbani maana niliwacha na hali mbaya sana,
hata sielewi wanaishi vipi?”
“mwachie Mungu hujui anamakusudi gani na
familia yako”.
Tuliongea mambo mengi sana mbaka
kunakucha hata hatukulala kabisa
usiku ule lakini ilipo fika mida kama ya saa nne
asubuhi usingizi mzito
ulinipitia kwasababu sikulala kabisa usiku
wakuamkia siku hiyo nikawa
nimelala sijielewi kabisa.
“heeeeeeeeeee” nilishitushwa na kelele
zilizokuwa zinapigwa nnje
na watu walikuwa wamejaa pale kichanjani
wakiwa wameshika sahani na kikombe
mikononi, watu walioandaliwa kwa kufanya
unyama ile siku walikuwa wamejazia
na walikuwa wanafuraha sana.
Nyimbo nyingi ziliimbwa za ajabu ajabu kila
mmoja alionyesha
ushirikiano wa hali ya juu. “kamleteni huyo
ngedele” mama Janeth aliongea
na watu wakashangilia sana utafikiri walikuwa
hawanipendi hata chembe.
Nilibebwa mzega mzega mbaka katika kile
kichanja watu waliruka ruka
wakipiga kelele, mwili ulinitetemeka nikawa
nimesahau yote nilifundishwa
nikawa nalia tu “huwezi kunichanganya mimi na
binti yangu, unaanza wewe na
hivi viumbe vya tumboni vita fwaata” aliongea
mama Janeth kwa hasira,
nilimwona Janeth kwa mbali akilia bila kusema
kitu chochote.
Jamaa mmoja alinishika mkono ili waanze
kunicharanga taratibu
mwingine aliinua panga juu nilimwangalia Janeth
nikaona ameshika chuma huku
ameinua juu nilitamani iwe ni ndoto ili nishituke
usingizini, wakati panga
linashuka nikaropoka “chu-u-ma” lile panga lilipo
goti katika mkono wangu
lilivunjika katikati yule jamaa aliyetaka kunikata
akaanza kulia “naumia
naumia ahaaaa” nilishangaa kuona ameshika
mkono akilia na sijaumia na panga
limekatika, watu walibaki wakinishangaa.
Ilibidi aitwe jamaa mwingine wenyenguvu ili
ajaribu kuniuwa,
alikuja jamaa miraba minne na shoka mkononi
watu wote walikaa kimya
wakisubiri kuna nini kitatokea, nilimtazama Janeti
nikaona akimwaga maji
chini basi shoka lilipokuwa likitu usoni kwangu
nililia “maji…” watu wote
waliokuwa karibu waliloa maji na yale yaliyo ruka
juu yalipo tua chini
hayakuonekana palikuwa ni pakavu kabisa watu
walishangaa nikicheka kwa
sauti na kwa kujiamini nilifurahi kuona vile
ingawa kuna wakati nilihisi ni
ndoto.
Baada ya kuona vile alikuja mzee mmoja
pale kichanjani “wewe ni
nani?” nilimtazama Janeth nikaona kaweka kidole
mdomoni ishaara nikae
kimya, aliniuliza maswali lakini sikumjibu hata
moja. Minong’ono ya watu
ilisikika ikistaajabu maajabu niliyoyafanya.
Yule mzee ilimbidi kuhutubia, “sasa jamani
kama mlivyoshuhudia hivi
ngoja tukafanye kikao mara moja kisha mtajua
nini kifanyike” basi watu
walitawanyika na kukaa katika makundi makundi
na kila kundi likiongea lao
“sasa kijana vikao vyetu havifanyiki
ardhini”waliruka na kuketi angani,
nami nikaongea na mkono wangu nikaruka mbaka
walipo kaa.
Wote walikaa kimya utafikiri walijiuliza nani
aanze kuniuliza, mzee
mmoja alianza kwa kukohoa “khoooo, mama Jane
kuna kitu nahisi kinaendelea
juu yenu nini ukweli wake?” “nikweli huyu kijana
nina mfahau vizuri na
kijiji nilichofukuzwa ndiko alikotoka isitoshe
babaake mzazi alikuwa ni
mwanachama mwenzetu ila tulimuwa kutokana
na kukaidi agizo la kumtoa kafara
huyu kijana” nilishituka kusikia vile “kumbe wewe
ndiye uliye muuwa
babaangu?” nilipaniki kusikia vile nikaanguka
chini “ha-ha-ha-ha-haa”
walianza kucheka.
Niliinuka baada ya kumwona Janeth
amesimama dirishani na kuruka
tena mbaka pale walipo kaa, nkakaa kwa
ukakamavu “kijana unaonekana
unanguvu ndogo lakini kwanini upo imara hivyo?”
“mzee mwenyewe sielewi haya
mambo yakoje, hata mimi najishanaa”
“mmmmh!!!!, kumbe eh?, yawezekana
mizimu yetu imekupenda kwasabau nguvu ulizo
nazo zinatoka katika dini yetu”
sikujibu chochote ila niliona wote wakiitikia kwa
kitikisa vichwa “laiti
wangejua ni mwanao Janeth ndio amefanya hivi
sijui inge kuaje?” nilijisemea
mwenyewe kimoyomoyo.
Nguvu zilianza kuniisha nilikuwa
nimechoka kukaa kulea angani
basi nikawa nina kaza ilifika kipindi nikaanguka
tena lakini kabla sijafika
chini niligandishwa tena kisha wale wazee nao
wakashuka mbaka chini “simama
kijana” aliniamuru mzee mmoja nikasimama
“tufwate” nikawafwata tukaingia
ndani ya jengo ambalo lilikuwa kama ukumbi
ndani kulikuwa na mafuvu ya watu
ngozi za wanyama pori “keti hapo” nilikaa huku
nikitetemeka “kijana hupaswi
kuogopa wewe ni mwanafamilia mwenzetu sasa”
kuna mzee alinitia moyo.
“kwakuwa umeonyesha kuwa wewe ni
mwana chama wetu itabidi upate
nyumba ile pale karibu na mzee Maganga”
“nashukuru sana mzee” wakati huo
mama Janeth alikuwa amenuna anataka
kupasuka “jamani sasa vipi mgogoro wa
huyu kijana na Mlopelo mme wa Janeth” “ah
haaaaa swala jema sana mzee
Kibito, ni vyema tumwite Mlopelo na Janeth ili
tulimalize hapa hapa” wote
waka kubaliana hivyo.
Haikuchukuwa dakika Janeth aliingia na mme
wake Mlopelo “kaeni hapo”
walionyeshwa wakae kati kati utafikiri walikuwa
ni wambea wanataka
kuwasutwa “jamani jambo tulilowaitiena hapa ni
kuhusu mapenzi yenu yalio
leta doa kubwa kati ya Mlopelo na mkeo Janeth
pamoja na huyu kijana”
Mlopelo na Janeth waliinamisha vichwa chini
wakisikiliza walichoitiwa
katika kikao.
Mzee Kibito alisimama nakuzungumza ili
kuondoa tofauti zetu mimi na
Mlopelo “kwa hiyo ndio hivyo kijana jambo la
msingi ujue huyu kijana ni
mwana chama mwenzetu na nilichowaitia hapa ni
kuwaunganisheni ili kuondoa
tofauti zenu” mzee Kibito aliendelea “hivi
Janeth…” “abeeeee….” Janeth
aliitika kwa sauti ya chini “nani unampenda kati
ya huyu kijana Joseph na
mmeo Mlopelo?” mzee Kibito aliketi na Janeth
akapiga magoti kabla hajaanza
kuongea na kusujudu mara nne.
Wakati amepiga magoti alianza kuongea
“samahani sana wazee wagu”
Janeth alivuta pumzi kidigo na wote tulimsikiliza
kwa makini “Joseph ni
kijana niliyeanza naye urafiki tokea utotoni,
tumecheza wote na kukua
pamoja mbaka imefika siku sisi tunafukuzwa
katika kile kijiji. Katika
maisha yangu nilikuwa nnamfikiria sana Joseph
na-a-a-aa nilipenda sana
siku moja kuja kuishi nae kama baba wa watoto
wangu hivyo siku ile ya
kwanza wamemleta hapa kijijini na yeye
alivyojitambulisha anaitwa Joseph
Mponzi ni mkazi wa Iringa Ndolezi basi niliamini
mizimu imesikia kilio
changu”.
Janeth alivuta tena pumzi na kuendelea
kuongea “kwa kweli nnampenda
sana Joseph na kuhusu Mlopelo mimi
nililazimishwa tu kuolewa nae ila sina
mapenzi na Mlopelo hata kidogo” alipomaliza
alisujudu tena mara nne na
kuketi, nilimtazama mama Janeth nakuona
akitikisa kichwa ishara ya
kutoamini binti yake anachokisema. Alisimam
Mlopelo na kuinama ishara ya
kutoa heshima yake huku machozi yakimtoka
“sinabudi kukubaliana na Jane
akisemacho”
Niliona Mlopelo akilia huruma ikaniingia
nilitamani niwaunganishe na
mpenzi wake Janeth nikawa najutia uamuzi nilio
uchukuwa wa kutembea na
Janeth hali ilio pelekea kumuumiza mwanaume
mwenzangu, mlopelo aliendelea
kuongea “Joseph kwa moyo mmoja nakuachia
Jane, naomba umlinde umjali na
kumthamini kama yeye anavyokupenda, na jambo
la mwisho karibu sana katika
familia yetu” Mlopelo alimaliza huku usoni ameloa
machozi, hata alipomaliza
kuongea aliondoka na kuelekea nnje.
Muda ulikuwa umeenda sana “jamani
ilimradi Mlopelo kakubaliana na
hilo basi, sijui Joseph una jambo la kusema”
ilibidi nisimame nitoe heshima
kama alivyofanya Mlopelo nakuongea
“samahanini sana wazee wangu, binafsi
nilikuwa sijui kama Janeth ameolewa na
nimwanamke ambaye ninampenda sana”
“na vipi kuhusu mama Janeth” lilikuwa ni swali la
mzee Maganga “jamani mama
Janeth ni mamaangu na itabaki kuwa hivyo”
Tuliongea mambo mengi sana mbaka
mipango ya ndoa ikapangwa baina
yangu na Janeth. Mzee Maganga alihairisha
kikao na kuelekea kulala. Usiku
ule nilikuwa siamini yaliyotokea nilihisi ni ndoto
na itafika muda
ntashituka katika ndoto nilizokuwa naota na
kumbe ndio nilikuwa naingizwa
katika mambo ya kichawi na yasiyo mpendeza
Mungu.
Asubuhi kulikucha la mgambo likalia wote
tukakusanyika katika eneo
lile wanalofanyia unyama kila siku na mzee Kibito
alianza kwa kusalimia na
wote wakaitikia kisha akanza kunitambulisha kwa
kuniweka katikati ya
halaiki ya watu “nijambo la heri sana tulilo
waitieni leo kwani huyu kijana
tumegundua ni mwanachama wetu ambaye
amechaguliwa na mizimu yetu hatayeye
pasipo kujua, hivyo basi anahitaji sana
ushirikiano wenu katika utendaji
kazi ili kuijenga kazi yetu na dini yetu sawa?”
“ngraaaaaaaaaaaaaa” wote
walijibu kisha akaendelea “na ninapenda
kuchukua nafasi hii kwaajili ya
kutangaza ndoa baina yake na binti yetu kipenzi
Janeth kama mzimu ilivyo
amua” watu walionyesha kuguna lakini
hawakuwa na sauti, walipo amrishwa
kukaa kimya wote walifanya, kikao cha dharula
kilipangwa na nikakabidhiwa
vijana ambao watanifundisha kazi pale kijijini.
Katika maisha yangu nilimchukia sana
mchawi mawazo mengi yalikuwa
yananipelekea kumchukua babu Ally kutoroka nae.
“Jose inabidi twende
gerezani kule tukakutembeze na kuchukuwa watu
wengine” jamaa mmoja niliye
kabidhiwa kwaajili ya kazi aliyefahamika kwa jina
la Solo aliniambia,
ikabidi nikubalianeane nae “ngraaaaaaaaa”
tuliruka hewani mbaka gerezani.
Nilitembezwa gereza lote huku nikielezwa
unyama wanaowafanyia
binadamu na kuonekana wamekufa katika macho
ya kawaida, tulienda nnje
nikawa naelekezwa jinsi ya kutengeneza upepo na
radi kama walivyo fanya
siku waliyo mchukua babu Ally tukiwa shambani
“sasa wewe utamchukuwa yule
na mimi nitamchukuwa yule “1…. 2…. 3”
alipomaliza kuhesabu tulitoka spidi
na kuwanyakuwa wale watu mbaka kijijini,
ambako nilishangiliwa sana.
Nilionyeshwa mazingira yote ya kile kijiji
huku nikiisubiri siku
yangu ya ndoa iliyopangwa ifungishwe na mtu
aliyefahamika kwa jina la
Ramadhani Abdul Ramadhani mtu
aliyesemekanika ni mkuu wawa chawi Afrika
Mashariki.
Baada ya miangaiko ya hapa na pale jioni
ilipoingia watu wote
walikuwa wameelekea kichanjani ila mimi nikawa
nimelala katika ile nyumba
niliyo kabidhiwa na mzee Kibito, alitumwa Solo
aje anifwaate ikabidi nitoke
mbaka pale kichanjani, nilielekea upande wa
wanaume nikasimama huku naogopa
lakini upande wapili waliko simama akina mama
nilimwona Janeth akinipungia
mkono nikatabasamu.
Aliletwa jamaa mmoja niliyekuja nae mimi
kutoka kule gerezani na
kulazwa katika kichanja, niliumia sana lakini kila
nikimtazama Janeth
alinionyesha ishara zilizo nipa ujasili na
kuendelea kuangalia unyama
unaotendeka ambao sikuzote nilikuwa nauona
ndani ya kibanda nilichokuwa na
ishi tokea nimefika katika kile kijiji.
Ilikuwa ni siku ambayo sitoisahau katika
maisha yangu kwani ni siku
ambayo nilianza kufundishwa kula nyama za
watu na kunywa damu za watu kwa
kulazimishwa na wazee wa kile kijiji “endapo
utashindwa basi wewe ndiye
utakuwa chakula chetu cha kesho”, maneno yale
yalifanya niogope na nijikute
najaribu kula kipande kimoja cha stake kavu ya
kuchomwa “kwa-kwa-kwa-kwa”
yalisikika makofi yaliyo ambatanishwa na
shangwe nyingi kutoka watu
nikagundua kumbe watu wengi walikuwa
wakisubiri nilifanye lile tendo.
Katika maisha yangu ilikuwa ni siku ya
kwanza kula nyama ya binaadamu
na niligundua kwanini wale watu walipenda sana
kula nyama za watu yaani kwa
kweli nyama za binadamu ni nyama ambazo
naweza kusema ni nyama tamu kuliko
nyama ya mnyama yeyote yule katika dunia.
Nilijikuta nikila na kunywa damu
katika kundi lile la wazee, mambo mengi
yalifanyika bado nikawa napewa
elimu na kila ninae kaa naye.
Vijana wengi pale kijijini walionyesha
kunichukia kwasababu
nilipendwa sana na wazee ambao nao waliamini
mimi nimechaguliwa na mizimu
yao na kunijari hata baadhi ya kazi ngumu mimi
sikuzifanya.
Maisha mapya katika dini ya kichawi
yaliendelea nilijikuta kuanza
kuyazoea yale maisha na kufanya mambo
makubwa zaidi yaliyo wavutia wengi
katika kile kijiji, sikumkumbuka tena babu Ally
wala ndugu zangu zaidi
niliisubiri siku ya ndoa yangu na Janeth
aliyekuwa anafungiwa ndani kama
mwali.
Nyakati za usiku nimejilaza naitafakari
asubuhi ambayo ndio siku
iliyosubiliwa kwa hamu na watu ili kushuhudia
ndoa itayo fungishwa na mkuu
wawachawi Afrika Mashariki ambaye alikuwa
ameingia usiku ule na watu
wengine walio msindikiza.
Asubuhi ilifika tulielekea sehemu ya mizimu
ambako tuliamliwa kuvua
nguo zote na kubaki watupu kama tulivyo zaliwa
bwana Ramadhani Abdul
Ramadhani aliomba mizimu ikubali ndoa yetu ili
tuwe mwili mmoja,
alipomaliza tulishauliwa kufanya tendo la ndoa
mbele ya halaiki ya watu
kama kutuunganisha, niliona aibu lakini nikajivua
ufahamu na kumshika
Janeth ambaye nilimlaza juu ya kaburi la mzimu
mkuu wa kijiji lililokupo
eneo lile na kuanza kuufanya ufusika mbele za
watu.
Ilichukua muda kama wa dakika 25 kumaliza
lile tendo ambapo
tulipomaliza watu walishangilia na kuimba
nyimbo nyingi sana kwa furaha.
“kijana unaonekana una nguvu sana safi sana
nimevutiwa na wewe, jambo la
msingi naomba ANIMUNI yenu niwapeleke
sehumu nzuri ambapo hamkuwahi kufika
wala kupahisi katika maisha yenu na huko
huenda watu wakubwa tu hivyo
mtakwenda kujifunza mambo mbali mbali” sikuwa
na jinsi ilinibidi
kukubaliana nae tena kwafuraha sana.
Sikuhiyo hiyo baada ya kusherekea kwa
kula kunywa na kucheza mimi
mke wangu Janeth na Ramadhani Abdul
Ramadhani pamoja na timu yake tulianza
safari usiku ule mbaka ufukwe wa bahari ulioko
nchini Kenya “Ramadhani
Abdul Ramadhani” alijitambulisha niliona njia
yakuingia majini “nifwateni”
wote tukamfwaata.
Tuliende mbaka chini ya bahari ambako
nilishangaa kuona majengo ya
kifahari yaliyo jengwa kwa madini tofauti tofauti
na maadhari zilizo vutia,
ukijani uliokuwepo eneo lile utafili ulikuwa wa
kuchora vumbi la dhahabu
ndilo lililo tawala ardhini.
Tulingia katika jengo kubwa sana liliokuwa
na vitu vya thamani
sana bwana Ramadhani Abdul Ramadhani
alituonyesha chumba kilicho andaliwa
kwaajili yetu, chumba kilikuwa ni kizuri sana
ukutani kulikuwa na picha za
viumbe vya ajabu, picha zenyewe zilikuwa ni
picha za mapenzi kutoka kwa
wale viumbe tukawa tumepumzika tukipiga stori
na my lovely Janeth.
Alikuja kijana mmoja chumbani kwetu na
kuniita “unaitwa na mkuu”
nilisimama na kumfwata Janeth nikamwacha
amelala nilimkuta Ramadhani
ameketi kitandani akiwa kifua wazi “karibu
kijana” “ahsante” “karibu ukae”
kulikuwa hakuna kiti zaidi ya kile kitanda basi
nikakaa.
Wakati tunapiga stori nilikuwa simwelewi
vizuri bwana Ramadhani
alikuwa ananishikashika mara ajilaze mapajani
kwangu baadaye alipoona
sielewi chochote ilibidi aongee tu “kijana wakati
ukifanya lile tendo la
ndoa na mkeo pale kaburini ulitokea kunivutia
sana sasa namimi ninataka
unifanyie vile” nilishituka kusikia vile nikawa na
hisi yawezekana
Ramadhani alikuwa ni shoga “hapana
haiwezekani” niligoma kufanya vile.
Nilishangaa kuona Ramadhani akivua
suruali na kunisogelea “endapo
hutokubaliana na hili nitakufanya kitu kibaya sasa
hivi” aliongea huku
akinivua nguo nilibaki natetemeka akautoa uume
wangu na kuuweka mdomoni
mwake na kuanza kuunyonya nikawa kama
sijielewi baadaye akachukua mafuta na
kunipaka sehemu zangu za siri na kujipaka
makalio yake na kuniamlisha
nifanye atakavyo ilibidi nifanye vile ili nimuwahi
mke wangu Janeth, lakini
nilipomaliza bado Ramadhani alining’ang’ania
nilale nae ndani kwake.
Usiku ule hatukulala tulikesha na Ramadhani
nikimfuraisha nafsi yake
mbaka kuna kucha asubuhi ilipofika nilirudi
chumbani kwangu nikamkuta
Janeth ameketi kitandani akilia “Janeth kuna nini
tena” hakunijibu ila
aliendelea kulia, ikabidi nimdanganye
“nimeambiwa tukiwa katika nyumba hii
takatifu hatupaswi kufanya tendo la ndoa mbaka
siku zote tatu zitakapo
kwisha ndipo tutaruhusiwa” kidogo Janeth
akanielewa.
Siku zote tulizo ishi mle ndani nilikuwa
nikimridhisha Ramadhani
ikafika kipindi nikaanza na mimi kunogewa na ile
michezo. Siku tatu
zilipopita tulipelekwa sehemu na kukabidhiwa
nguvu za kichawi na kuchemshwa
kwenye vyungu siku nzima “sasa mmekuwa watu
wakubwa sana na mnaweza
kuondoka na kuishi maisha myatakayo”
tulikabidhiwa watu wakutusindikiza
mbaka kijijini kwetu.
Watu walifurahi sana kutuona tumerudi
salama na tulikuwa na nguvu
zingine ambazo kwa pale kijijini hakuepo mtu
hata mmoja alifikia nguvu
tulizopewa kule chini ya baharini. Tulifikisha
salaam zote tulizoagizwa na
kuingia ndani kupumzika wale watu waliokuwa
wametusindikiza waliondoka na
kurudi nchini kwao Kenya.
Wakati wa usiku tukiwa ndani tumetulia na
mke wangu Janeth ambaye ni
mama kijacho mlango uligongwa aliingia
mwanamke mmoja kutuletea chakula,
wakati tunakula tuliendelea kufulahia maisha
“darling mi sitaki kuishi humu
ndani” Janeth aliongea kwa kudeka “sasa tutaishi
wapi mamaangu?” “mimi
nataka twende Dar Es salaam tukatafute nyumba
tuilete huku kwa uwezo
tulionao” “waaaau wazo zuri sana mke wangu,
kesho alfajiri itabidi twende
tukatafute na jioni turudi nayo” tulifurahi sana na
kufurahia penzi letu.
Asubuhi alfajiri tuliaga tunaenda Dar es
salaam kutafuta nyumba,
wazee wakawa wanashangaa “vipi mnahama?”
lilikuwa ni swali la mzee Kibito
“hapana tutarudi usiku” walitamani kutuzuia
lakini kwa uwezo tulionao
hawakuweza kuzuia safari yetu, tulianza safari na
moja kwa moja tulielekea
Dar es salaam Masaki.
Tulipofika tulizunguka huku na huko tuka
ziona nyumba kama mbili
ambazo ni nzuri na zilikuwa na ulinzi mdogo
katika ngu zetu “sasa mke wangu
nyumba ile nimeipenda lakini itabidi tuichukue
kwa staili ya kuteketeza kwa
moto” “sawa mimi nakusikiliza wewe tu” tulikaa
katika sehemu ya kivuli na
kusubili ifike mida ya saa 10 kazi ianze “unajua
tuna kazi nzito sana
kwahiyo tugawane majukumu wewe inabidi ulete
mvua kali na radi na
nitakachofanya mimi nitailipua nyumba kwa moto
kisha tutabeba nyumba na
kuwachia kivuli cha nyumba” “sawa” tukawa
tumekubaliana hivyo.
Geti la ile nyumba lilifunguliwa, kuna gari
aina ya Benzi rangi
nyeupe lilitoka mbele alikaa mwanamke na
watoto wawili walikuwa wamekaa kwa
nyuma. Walielekea barabara ya kwenda upanga,
tuliruka hewani bila kuonekana
na mke wangu akaanza kazi ya kukusanya maji
ya bahari na kuruhusu mvua
kubwa ianze kunyesha.
Jiji la Dar es salaam mvua kubwa ilinyesha
ikiambatana na radi kwa
takribani saa moja upepo ulivuma kuna nguzo
ilikuwa karibu na ile nyuma
nikaisukuma na kuiangusha ili kuwafanya watu
wasifikirie vibaya.
Nilianza kuivuta ile nyumba nikafanikiwa
kuingoa giza lilikuwa
limetanda watu walijifungia ndani ikabidi niwashe
moto lile eneo na
kuondoka na ile nyumba.
Tulifanikiwa kufika kigoma katika kijiji chetu
na kutafuta sehemu
na kuisimika ile nyumba, watu walikuwa
kichanjani wakian daa chakula cha
usiku lakini baada ya kusikia kishindo walikuja
mbio nakushangaa jumba
tulilokuja nalo.
Wengi walitupongeza sana na kuomba
tuwafundishe njia tuliyo itumia
tuliwafundisha kiroho safi na wengi walielekea
maeneo ya karibu na kuleta
nyumba zilizo vutia.
Ilifika kipindi niliheshimika sana pale kijijini
na baadhi ya watu
waliniogopa, nilijikuta nimekua mchawi mkubwa
sana nchini na maarufu
kutokana na vikao mbalimabali nilivyo kuwa
naalikwa nchi mbalimbali.
Katika safari za vikao vyote nilizidi kukutana
na Ramadhani Abdul
Ramadhani ambaye nilikuwa nalala naye na
kuendelea kufanya naye mapenzi
kinyume na maumbile Ramadhani alikuwa
ananipenda sana na kunifanya nianze
kufanya nianze kuwatongoza wanaume na
kuwaonga pesa ili niwafanyie michezo
michafu na kwa kuwa mke wangu alikuwa
anakaribia kujifungu basi nilizunguka
sehemu nyingi na kuishi maisha ya kishetani
sana.
Nilipokuwa kigoma nasubiri siku za
kujifungua mke wangu nililetewa
taarifa kuwa Ramadhani Abdul Ramadhani
amefariki Dunia kwa ugojwa hatari wa
UKIMWI katika hospitali ya Kenyata usiku wa
kuamkia hiyo siku.
Nilichanganyikiwa sana kusikia Ramadhani
amefariki kwa ugonjwa
hatari wa UKIMWI “mme wangu umepatwa na
nini? Mbona hivyo?” “aaaah
nimepokea taarifa Ramadhani Abdul amefariki
Dunia” “eeeeeeh” “ndio hivyo
inabidi niende huko” “sasa utaondoka vipi na
mimi karibu najifungua” “no
inabidi niende tu” basi maneno yale hakuyapenda
Janeth.
Wakati nipo ndani nikiwa katika mawazo
mazito huku nikijiandaa kwa
safari ingawa plani zangu ilikuwa ni kwenda
kupima afya yangu na sio kwenda
msibani nilisikia sauti ya Janeth akilia, ilibidi
nitoke haraka nikamkuta
amelala chini akilia huku analalamika ilibi niite
wakunga wa jadi wakambeba
na kuingia na chumbani wakati huo nilikuwa na
subiri sebleni.
Katika maisha niliwachukia sana watoto
wakike hivyo sikupenda
kupata mtoto wa kike nikawa naomba apatikane
mtoto wa kiuume, haikuchukua
muda alitoka mama mmoja aliyefahamika kwajina
la mama Kidawa “hongera sana
mkeo amejifungua salama ametuleta kabinti na
mmefanana nako sana”
nilijichekesha kinafiki lakini sikupenda mtoto wa
kike hata kidogo.
Walipomaliza nilienda kumwona mke wangu
na mwanangu “oooooooh
ahsante sana mke wangu kwa kunizalia mtoto
mzuri” nilimbusu katika paji la
uso na kuaga naenda Kenya kuonekana tu alafu
nitarudi lakini wazee
walinizuia sikuweza kuondoka kichwani niliwaza
sana kama nitakua nime
athirika au lah.
Wakati nipo katika msongo wa mawazo
sebleni kwangu nikiwa na wageni
wengi waliokuwa wamekuja kumwona mke wangu
waliona nipo tofauti na kila
waliponiuliza nilijitetea msiba wa bwana
Ramadhani kumbe haikuwa hivyo
“samahani baba tunaomba utupe jina la mtoto”
“aaaah mpeni hatajina la
mizimu yetu” niliongea kwa kuropoka lakini
nilishangaa kuna nashangiliwa na
kupewa sifa kemu kemu kwa kuijali mizimu yetu
ndipo bibi mmoja akashauri
mtoto aitwe Kabula.
Muda ulikuwa umeenda walibaki watu
wachache sana kwaajili ya
kumuhudumia mke wangu na mimi mwenyewe,
usiku wa manane kuna mtu alitumwa
aniite niende nyumbani kwa mama Janeth
ambako nilifika nikakuta wazee
wamekaa na kina mama.
Nilipokelewa kwa furaha na hongera nikawa
najua hongera zile zilikuwa
za mke wangu mama Kabula baada ya
kujifungua, nilisikia sauti ya kichanga
ikilia “kijana pita tu ndani ukamwone mwanao”
nilielekea chumbani kwa mama
Janeth nilikuta mama Janeth amelala na mtoto
pembeni nikajua tayari
kimelipuka “umefwata nini wewe hebu toka ndani
kwangu sitaki hata kukuona
toka haraka…” mama Janeth aliponiona
alinifukuza kama mbwa alionekana
alikuwa amenichukia sana katika maisha yake
“kijana nenda kapumzike ni
hasira tu ila umeletewa mtoto wa kiume”
nilifurahi sana kusikia vile
nikajua nimepata mrithi wangu nilienda nyumbani
kwangu lakini sikuweza
kumwambia kitu chochote mke wangu mama
Kabula.
Asubuhi kulipokucha nilipokea hongera
nyingi kutoka sehemu
mbalimbali duniani nilifarijika sana lakini bado
nilishindwa kuwa na amani
kwasababu ya taarifa za kifo cha Ramadhani
niliamini fika Ramadhani atakuwa
ameniambukiza virusi vya UKIMWI “potelea pote”
nilijisemea mwenyewe lakini
sauti ilitoka “nini tena mme wangu?” “aaah basi
tu mke wangu, unajua
Ramadhani aliniahidi mambo mengi sana lakini
ndio basi tena” nilijitetea na
mke wangu akanielewa.
Siku ziliende huku taarifa za mwanangu
upande wa mama Janeth
nilizisikia kwa watu lakini siku hii ilikuwa ya
pekee sana na niliipenda
sana kwasababu wazee walitumia busara zao
kwa kutupatanisha na mama Janeth
na hapo niliweza kumwona mwanangu ambaye
nilifanana nae sana, walipo maliza
kutupatanisha nilirudi nyumbani kwangu
nilimkuta mke wangu amenuna usoni
amelowa machozi.
Ilibidi nianze kumwelewesha yaliyotokea huko
nyumbani kwa mama yake
“namchukia sana mama…… simpendi” “hutakiwi
kufanya hivyo mama Kabula yule
ni mamaako” nilijitahidi sana kumbembeleza mke
wangu lakini alishindwa
kunielewa kabisa.
Katika maisha yangu sijawahi kufikiria kuwa
mchawi lakini
nilijikuta nimekuwa mchawi mkubwa sana na
maarufu sehemu mbalimbali za
Afrika. Mke wangu alianza kunishauri kumtoa
kafara mamaake mzazi ili kutoa
sadaka kwa myungu kwa sehemu tuliyofikia.
Niliamini labda anaumia mimi kuzaa na
mamaake lakini niliona
amekazana sana “sasa kama wewe hutofanya
basi nitafanya menyewe”
alipomaliza kuongea aliondoka kwa hasira na
kuelekea ndani, ilinibidi
nimfwate nikamkuta analia “mama Kabula
nimekuelewa mke wangu tutafanya
hivyo” ilibidi nimuunge mkono nikaona amefurahi
sana.
Tulipanga njama na njia ya kutumia
kumwondoa mamaake Janeth usiku ule
ule. Basi tulituma ugojwa na kumkata sauti
mbaka kufikia siku ya pili
mchana ndipo tulipoanza kazi ya kuichukua
pumzi yake, haikuwa kazi nyepesi
kama tulivyo fikiria mwanzo ilibidi nimwache mke
wangu akipambana mimi
nikaenda kujiongeza nguvu niliporudi nilikuta mke
wangu ameanza kulegea
aliponiona alianguka chini nikajua labda
ameuwawa nilienda kumwangalia
nikagundua ni mzima hapo ndipo niliporejea kwa
mama Janeth kwa hasira zote
na kufanikisha kitoa roho yake ambayo niliondoka
nayo mbaka ndani kwetu
nikawa naiandaa tayari kwa kuliwa.
Nilimsikia mke wangu akikohoa, ilinibidi
nimfwate “vipi mmengu”
aliongea kwa shida “usijali nimefanikiwa”
nikainuka na kwenda kuuleta ule
moyo wa mamaake na kugawana kisha tukaula
kwa pamoja na baada ya kumaliza
tulisikia kelele za watu nnje tukajua tayari.
Ilibidi tutoke nnje na kukuta watu
wamekusanyika kwa mama Janeth na
kwasababu nilikuwa ninakubalika sana wengi
walisuburi tamko langu ni nini,
nilisimama kiuume nakuongea “poleni sana ndugu
zangu kama mlivyoona na
wengine mlivyo sikia kuwa tumepoteza kiongozi
wetu wa muda mrefu sana
lakini kawaida yetu mtu akifariki inafahamika
hivyo waandaaji fanyeni kazi”
kabla sijamaliza watu walishangilia sana na
kuelekea kichanjani na watu
wengi walionyesha kuto kuupenda uongozi wawa
mama Janeth.
Watu walipomaliza kula nyama ya mwili wa
mama Janeth ilibidi wazee
wapeendekeze kiongozi mwingine alisimama
mzee wa kwanza na kupendekeza jina
langu nilona wengi wanashangilia kusikia jina
langu alisimama mzee kibito
nae “jamani kama mnavyomjua kijana wetu jinsi
anavyo tuwakilisha vizuri
Afrika” “nje ya hivyo huyu ndiye aliyefanya tuishi
kwenye nyumba nzuri hivi
uongo?” “kweeeeeeeliii” wote waliitikia kwa
kushangilia.
Nilifarijika sana kuona watu wananikubali
nilimtazama mke wangu
niliona machozi ya furahaa yakimtoka mzee
Maganga alisimama na kuzungumza
“Kijana uwanja ni wako na wote wanakuachia
mpira wewe, unalolote la kusema
kabla hatuja tawanyika?” “nashukuru sana kwa
nafasi mliyo nipa na jambo la
msingi naomeni ushirikino na pale nitakapokuwa
nakwenda tofauti tusisite
kuambizana” nilivuta pumzi kidogo “na kuhusu
mipaka yote iliyokuwa imewekwa
kwaajili ya kutotoka nnje ya mkoa huu naivunja
na kuanzia sasa wote
tutakuwa ni sawa” watu walishangilia sana na
hawakutegemea kupewa uhuru.
Ilibidi nimchukue mwanangu ambaye nilizaa
na mama Janeth na kuishi
nae nyumbani kwangu, watoto wangu Kabula na
mdogoake Dickison aliyepewa
jina la babu yake walipendana sana na waliishi
kwa kushirikiana vizuri
mbaka nilipenda ila taizo moja alilokuwa nalo
mwanangu Kabula alikuwa
akiumwa umwa mara kwa mara na tiba za asili
zilishindwa kijua ugonjwa wake
hata siku moja.
Maisha yangu yalibadilika sana nilizidi
kupewa nafasi za juu hadi
ilinilazim kuhama pale kijijini na kwenda kuishi
jijini Daer es salaam
ambako nilipewa nyumba maeneo ya Mbezi bichi
na raisi wa nchi ambaye mambo
mengi ya ulinzi na mipango mibaya juu yake
nilikuwa nikiifunga.
Maisha yangu ya uchawi yalibadilika
nilianza kuishi kama shetani
kwani kazi yangu kubwa ilikuwa kuzindika nchi
na viongozi mbali mbali wa
nchi na wa dini na nchi za karibu zilinialika katika
mambo mengi ya kitaifa.
Watanzania wengi walinipenda sana
kutokana na misaada niliyokuwa
naitoa kwao kupitia nyanja mbali mbali nilifungua
vituo vya watoto yatima
na wazee wasio jiweza na kuwapa chakula kumbe
nilikuwa nikijitengenezea
jina nchini.
Siku moja nikiwa natoka Ikulu iliopo Posta
jijini Dar es salaam
nilikuwa nimechoka sana wakati nimeingia ndani
sikuona mtu yeyote lakini
katika kuangaza huku na huko nilisikia sauti za
miguno ya kimahaba kutokea
jikoni nilienda kwa kunyata kutazama ni nani
anayefanya ushenzi nyumbani
kwangu kwa wakati ule.
Sikuamini macho yangu kwa nilichokiona
kwani walikuwa ni wanangu wa
kuwazaa Kabula na mdogo wake Dickison mapigo
ya moyo yalinienda mbio mwili
uliishiwa nguvu na katika maisha niliyo walea
sikuwahi kuwachapa hata siku
moja ilinibidi niwashitue na kuwaita sebuleni ila
kilichonishangaza hata
hawakuogopa.
“kwanini mnafanya hivi na nyie ni ndugu et?”
“baba mimi sioni tatizo
kwani sisi…..” ilibidi nidakie maana Kabula
aliongea upuuzi “pumbavu mkubwa
wewe kelele, mama Kabula unamsikia mwanao
huyu” “lakini baba huwezi kuzuia
hili kwani sisi tumependana na hatujaanza leo”
niliishiwa ma neno nikabaki
nikiwatazama tu “baba tusamehe sana kama
tumekukera ila sisi tunataka
tuowane na tuishi pamoja” sikuamini kama
mwanangu Dickison anaweza kufanya
ushenzi na dadaake.
Sikuwa na mawazo mngine zaidi ya kwenda
hospitali na kupima ingawa
binafsi niliamini fika mimi ni mwathirika “sasa
kesho itabidi ni mlete
daktari wangu ili atupimea afya nyumba nzima
sawa?” nikaondoka na kuelekea
chumbani wao nikawacha wanaongea na mama
yao kila nikifikiria kupima
namkumbuka bwana Ramadhan Abdul ambaye
aliniingiza katika tabia ya kufanya
mapenzi na wanaume tena mapenzi yasiyo
salama.
Asubuhi na mapema nilimwita daktari wangu
moja kwa moja alipofika
akatutoa damu na kuifanyia uchunguzi.
Ilichukuwa kama nusu saa daktari
alikuja na majibu yetu pale sebuleni kichwani
nilisha yajua majibu lakini
nilisubiri uthibitisho wa daktari.
Daktari alianza kuongea nasaha zake na
kutupa moyo wa uvumilivu
katika utoaji wa majibu yetu “majibu siyo mabaya
sana na siyo mazuri Kabula
unaonekana unaujauzito wa miezi miwili”
tulishituka kusikia hivyo ingawa
yeye na mwenze walifurahi sana “jambo la msingi
uanze kwenda clinic
ilikumwepusha aliye tumboni asiathilike” “dokta
ina maana nimeathilika?”
daktari ilibidi atumiea utaalamu wake kumpooza
Kabula atulie “na vipi
kuhusu mimi?” “Dickisoni mshukuru Mungu wewe
ni mzima” wote hatukuamini
maneno yale mbaka Kabula alihisi ni mipango
yetu kuharibu mapenzi yao.
Ilichukua muda mrefu sana kuutuliza ule
mzozo wa majibu ya Dickison
na Kabula lakini baadaye walitulia ndipo majibu
ya mwisho yalikuwa ya mimi
na mke wangu ambao matoko yetu yalikuwa
kama nilivyo fikiria kabla ya
kupima, daktari alitupa ushauri na kutuahidi kuwa
pamoja nasi kama
ilivyokuwa mwanzo na kutushauri ni vyema tunze
dozi mapma.
Kilanikifikiria kuwa mimi ndiye chanzo cha
ugonjwa ule katika
familia yangu nilikuwa naumia sana kwani nilijua
fika hakuna ujanja juu ya
ugojwa hatari wa UKIMWI ambao hata sisi
pamoja na utaalam wote wa kichawi
hatukuweza kupata dawa yake hivyo nilikuwa
sina amani kabisa moyoni mwangu.
Wakati nimelala ndani na mke wangu
ambaye alinitupia lawama zote
mimi kwamba mimi ndiye niliye uleta ugonjwa
ndani, nilitumia kila namna ya
kumshawishi ili aniamini na kwakuwa mke wangu
mama Kabula aliniamini sana
alikubali ingawa nilijua hakukubali toka moyoni.
“unawaza nini mm wangu?” “aaah sielewi
nini nifanye juu ya Kabula
na mimba ya kakayake, wananichanganya sana
hawa watoto akili yangu” “mme
wangu siku zote maji hufwata mkondo”
“unamaana gain?” “umesahau kuwa wewe
ulizaa na mama na mtoto?” maneno yale yalinipa
hasira kiasi kwamba
niliinuka na kumpiga kibao mke wangu ambaye
alianguka chini na kujigonga
kwenye pembe ya kitanda kisogoni hali ambayo
ilimfanya azimie pale pale.
“mke wangu, mke wangu…..” niliita pasipo
majibu ndipo nilipoamua
kumwita askari tukambeba mke wangu na bila
kuchelewa nilimkimbiza katika
hospili ya Lugalo iliopo karibu na nilipokuwa
naishi Mbezi bichi.
Tulifika hospitali na moja kwa moja
tulipokelewa vizuri kutokana na
jina nililokuwa nalo nchini ilibidi apewe chumba
cha pekeake na kuanza
kupewa huduma.
Nikiwa nimketi kwenye kiti nasubiria majibu
ya Daktari nilishangaa kuwaona
wanangu Kabula na Dicksoni wakitoka ndani kwa
Daktari huku Kabula akilia
niliinuka haraka na kuwafwata “Dickison kuna nini
mwangu??” niliuliza kwa
mshangao “tulikuja kuhakikisha majibu” “eeeh
he….!!!! Imekuaje?” “nikama
yale ya Dokta Mbuta” “aah poleni sana wanangu”
niliongea kwa masikitiko
kwasababu nilijua kabisa mimi ndio chanzo cha
mambo yote.
“mbona na wewe upo hapa?” Dickison
alinitupia swali baada ya dadaake
kunyamaza kulia “mama yenu anaumwa,
amepoteza fahamu…” wakati naongea
nilimwona Dakitari akitoka katika kil chumba
alipokuwa mke wangu ilibidi
nimwite “Dokta dokta” alisimama nikamfwaata
haraka na wanangu walifwata
nyuma yangu.
“Dokta vipi?” “oooooh mr Gami, pole sana
ila bado tupo tuna
mshughulikia mkeo na muda mfupi itabidi
tumwamishe na tumpeleke Muhimbili
tatizo linaonekana ni kubwa kidogo ila atapona
tu” nguvu ziliniishia
kusikia vile nilijikuta nashindwa kuongea lolote na
Daktari akotoweka
“kwani baba imekuaje” Kabula aliniuliza swali “ni
bahati mbaya aliteleza na
kudondoka akajigonga kichwani” niliwaongopea
wanangu na sikutaka wajue
ukweli kabisa.
Madaktari walimaliza huduma ya kwanza
na kumpakia mke wangu katika
gari la kubebea wagonjwa safari ya kwenda
hospitali ya muhimbili ikaanza,
mimi na wanangu tulipanda gari letu na Dickisoni
ndiye aliliendesha gari
letu kutokana na mimi na Kabula kuwa
tumechanganyikiwa na
kilichonichanganya zaidi nipale nilipochukuwa
uamzi wa kumpiga mke wangu
isitoshe mimi ndiye niliye peleka ugonjwa hatari
katika famlilia.
Tulichukua muda mrefu barabarani
kutokana na foleni nilitamani
kushuka na kutemba kwa mguu lakini ilihitaji
uvumilivu. Tulifika katika
hospitali ya Muhimbili na kukuta tayari mke
wangu ameanza kupata huduma
moja kwa moja niliingia kwa Dackitari mkuu na
kuongea nae lakini alinisii
nisubili bado walikuwa wanamfanyia uchunguzi,
ilinibidi kutoka na kwenda
kuketi kwenye benji nikisubiri ripoti kutoka kwa
Daktari.
Muda ulikuwa umeenda sana mbuu
walikuwa wakining’ata sana ikabidi
niwaruhusu Kabula na mdogo wake waende
nyumbani wakapumzike mimi nibaki
pale nasubiri majibu kutoka kwa Daktari.
Nyakati za usiku wa manane ilibidi niende
bafuni ambako
nilijibadilisha katika hali ya ubinadamu na kuingia
katika hali ya
kishetani niliita mizimu imsaidie mke wangu
apone, lakini kufanya vile
kulifanya tarifa za kuumwa kwa mke wangu
ziwafikie watu wengi wanao tumia
nguvu za giza, usiku ule ule nilianza kupokea
wageni kutoka sehemu mbali
mbali na walikuja wakawa wanajaribu kusaidia
kumponya mama Kabula bila
mafanikio yoyote yale.
Alfajiri ilifika watu wakatawanyika na kurudi
makwao nililejea katika
benji la kusubilia wagonjwa na haikuchukuwa
muda mrefu niliona daktari
akitoka katika chumba alichokuwa amelazwa mke
wangu “samahani Dokta”
nilimwita daktari “aaaah bila samahani
mheshimiwa” nilimsogelea huku
nikitetemeka “usijari mheshimiwa, punguza
presha mkeo atapona bado
tunajitahiti kuokoa maisha yake tulichogundua
fuvu lake lilipata ufa lakini
imekuwa bahati damu haikuvujia katika ubongo
na madaktari wanajitahidi
kuokoa maisha yake”.
Ilikuwa ni kipindi kigumu sana kwangu
pale kila nilipoyafikilia
matatizo yanayo nikabiri lakini sikukata tamaa na
niliendelea kumwangaikia
mke wangu kwa hali na mali ilimradi apone,
nilipokea pole nyingi kutoka kwa
viongozi mbali mbali wa siasa na wa dini ambao
walitoa michango mingi sana
iliyokuwa inanifariji.
Siku karibu ya tatu nipo hospitali sijarudi
nyumbani kwangu
ninamwangalia tu mke wangu ilifika kipindi
tulianza kufanya vikao vyetu
pale pale hospitali na baadhi ya madaktari
walikuwa wapo katika chama chetu
hivyo haikuwa shida sana.
Kilichoanza kufanyika katika ile hospitali ya
Muhimbili tulianza
kula nyama za wagonjwa na hasa hasa
tulipendelea kula nyama za watoto
waliokuwa wanazaliwa na wakati mwingine
kuharibu mimba na kuzifanya vitoweo.
Hivyo hivyo pia mke wangu nilimlisha nyama
kwa njia za kichawi huku
tukisubiri myezi mitatu niliyo ahidiwa na
madaktari kuwa atazinduka katika
usingizi mzito aliokuwa nao.
Idadi ya vifo iliongezeka katika hospitali ya
Muhimbili hasa hasa kwa
kina mama na watoto wachanga ambao nyama
zao zilikuwa ni nzuri sana na ni
tamu sana.
Bado afya ya mke wangu haikuweza
kuonyesha matumaini lakini
kilichowashangaza watu wengi ni pale walipoona
mtu anaumwa lakini anazidi
kunenepa na kupendeza hali yupo tu kitandani
amelala hajielewi na hakuwahi
kupewa chakula hata siku moja.
Baadhi ya watu ambao walikuwa ni wana
chama wa dini ya kishetani
walianza kunishauri nimtoe tu kafara mke wangu
kwani alikuwa ananipotezea
muda “no haiwezekani, mke wangu nimetoka nae
mbali sana na amenisaidia
mambo mengi sana siwezi kufanya hivyo”
“mheshimiwa angalia taifa limeanza
kuyumba na wewe ndiye unayetegemewa jaribu
kutuelewa” aliongea waziri wa
mambo ya ndani huku akinishawishi mipango yao
“siwezi na kama mmechoka
kunisaidia semeni bila huyu mimi siwezi chochote
nusu ya nguvu zangu zipo
kwake”
Kusikia vile walikubaliana na mimi na kuahidi
kuwa bega kwa began a
mimi wakanishauri kumwamisha hospitali na
kumpleka India ili kupata
matibabu zaidi.
Siku moja wakati naamka asubuhi ili niwahi
haospitali kwa mke wangu
nilihisi kuumwa maana karibu mwili mzima
ulikuwa ukiuma nilienda chooni
mara kwa mara na nilikuwa nikindesha sana kifua
kiliniuma nikawa nakohoa
kwa tabu sana nilijaribu kumeza madawa yangu
ya asili lakini haya
kunisaidia chochote kile ilibidi niwatume wanangu
wakamwangali mama yao
hospitali anaendeleaje na wamwite daktari wangu
aje nyumbani kunicheki nini
tatizo.
Niliketi sebuleni nikiwa nimevaa taulo ili
nisipate shida wakati
wa kwenda uwani kujisaidia, ilichukua muda wa
dakika 20 hivi daktari kufika
pale nyumbani “aaaah karibu daktari”
“nimeshakaribia, pole sana mheshimiwa”
“najisikia vibaya sana” “nini tatizo?” “kifua
kinaniuma sana na ninaharisha
sana yani nateseka kweli yani” “vipi dozi
unatumia?” “sijatumia tokea mke
wangu aanze kuumwa” “umefanya uzembe sana
mheshimiwa” dokta alikuwa kama
anataka kunilaum lakini baadaye alinihudumia na
kunianzishia dozi mpya,
alinipa dawa za kifua na kukatisha kuharisha.
Watoto nao walirudi kutoka hospitali
wakanikuta nimelala chini
katika mkeka “unaendeleaje dady” “naendelea
vizuri mama, vipi mama yenu
anaendeleaje?” “bado hali yake ipo vile vile ila
mgongoni ameota vidonda
sana” “niliviona na madaktari walinambia ni
kwasababu amelala sana ila
baadaye tutaenda wote kumwona”.
Nilijikuta machozi yananitoka kila nikifikiria
matatizo yanayo
ikabili familia yangu na yote niliyasababisha mimi
mwenyewe “dady vipi?
Mbona unalia?” “aaah nachanganyikiwa kwa
kweli” “baba vumilia na unatakiwa
kuzoea na kuridhika kwa hali tulizo nazo mama
atapona tu” Dickisoni
alijaribu kunifariji huku akinifuta machozi,
nilijisikia aibu kuona watoto
wamechukulia kawaida ingawa hawakujua vizuri
kinachoniliza.
Nilitumia dozi kwa kuzingatia ipasavyo
hali yangu ilianza
kwenda sawa nikaendelea kufanya kazi zangu za
nchi na nikaona ni vyema
kutoa sadaka kwa mizimu ambampo nilianza
kupanga njama za kuchafua barabara
kuu ya morogoro road maneo ya mlandizi.
Ilikuwa mida ya asubuhi nilipanga vikosi
vyangu kwaajili
yakuchukuwa roho na damu za binadamu, Gari
moja la abilia aina ya Basi
lililosomeka ubavuni kwa jina la Hood lilikuwa
likitokea Dar es salaam
kwenda Songea likiwa katika mwendo mkali
nilimtumia giza nene dereva ambaye
alihama njia na kuingia katika makazi ya watu
pale pale bila kuchelewesha
tulichukuwa roho za watu wote bila kujali wale
waliokuwa karibu na eneo
lile hatukuacha hata tone la damu na moja kwa
moja nilipeleka kuzimu kama
sadaka lakini jambo la kushangaza nikaambiwa
damu haitoshi na ni kwa muda
mrefu sana walisubiri sadaka yangu na ndipo
walipoamua kutaka kumchukuwa
mke wangu.
“haaaa ina maana nyie ndie mmemfanyia
hivi mke wangu?”
“tumekuvumilia kwa muda mrefu sana bila kupata
sadaka yako kijana
hahahahahaha” walicheka kwa kebei “jamaani
naombeni msimuwe mke wangu na
kama ni damu nakwenda kuileta yakutosha”
“fanya hivyo maana siku iliyobaki
ni moja tu” kusikia vile sikutaka tena kuendelea
kuwasikiliza nikaondoka
haraka na kurudi duniani.
Ilikuwa ni usiku mnene wenye mambo
makubwa moja kwa moja
nilielekea hospitali ya Muhimbili kumwangalia
mke wangu, nilifika bado
amelala hajitambui roho iliniuma sana “usijali
mke wangu kesho fahamu
zitarejea na utakuwa mzima” nilimwambia mke
wangu huku nikimwonea huruma na
kwenda uwanja wa taifa wa mpira wa miguu
ambako kulikuwa na elimu juu ya
mambo ya shetani ikiendelea.
Wengi walishangaa kuona nimefika katika
eneo lile kwasababu haikuwa
desturi yangu kwenda mahali pale, basi nikawaita
na kuwakusanya sehemu moja
“jamani ninafurahi sana kuwaona mnaendelea
vizuri, ila nataka tubadilishe
zoezi kwani ninahitaji damu nyingi sana ambayo
nafikiria sehem kubwa ya
kuipata ni kwenye treni au meli zile kubwa” wote
walikuwa wakinisikiliza
kwa umakini ndipo nilipo panga vikosi vya
kuchafua reli itokayo Dar kwenda
Kigoma na wengi kupendekeza tutumie reli hiyo
kwasababu ilikuwa inatumika
asubuhi kwa kusafirisha abilia.
Wengine niliwapa kazi ya kuhakikisha treni
halifiki kigoma na
kulisababishia ajali, “kazi yangu itakuwa moja tu
kubeba roho zao na damu
zao” wote waliitikia na mara moja walitawanyika
na kuanza kuichafua reli
iendayo kigoma, kila mmoja alionyesha mbwebwe
zake na kufurahia kitengo
alichopewa.
Baada ya kuona kazi ikiendelea nilirudi
nyumbani ili nikawafahamishe
wanangu kazi itakayo tendeka asubuhi kukicha
“ni mizimu inayo msumbua mama
yenu lakini kesho mambo yote yatakwisha
wanangu” “basi baba tutakuwa wote
katika kuyapigania maisha ya mama” nilifurahi
sana kuona watoto nao
wameamua kusaidiana na mimi.
Asubuhi ilifika nikawa ninasubili muda ufike
lakini nikaona ni vyema
nikamchukue kabisa mke wangu arudi nyumbani
kwasababu niliamini ndio siku
yake ya uponyaji.
Nilienda hospitali nikamfwata daktari na
kuongea nae lakini
hakunielewa ilibidi nmfwate Daktari mkuu wa
hospitali ya Muhimbili ambaye
naye alikuwa ni mwanachama wa chama chetu
cha Kishetani lakini alinigomea
ikabidi niondoke na kurudi nyumbani kujipanga
kwa kazi.
Nikiwa chumbani kwangu naangalia TV
yangu asilia niliona treni likiwa
katika mwendo mkali sana angani kulikuwa na
mitego mingi sana ikabidi
nianze kufyatua mtego mmoja mmoja.
Mtego wa mwisho kuufyatua na uliokuwa
na matunda mema wakati treni
inaingia katika mkoa wa Tabora niliyumbisha reli
basi kichwa cha Treni
kilianza kuanguka na mabehewa mengine
yalifwaata huku treni likibilingika
kuona vile nilifurahi na moja kwa moja niliondoka
na wanangu hadi sehem ya
tukio.
Ilichukua sekunde 60 kufika sehemu ya
tukio ambapo tulifika watu
wapo hoi ndipo nilipoanza kazi ya kukusanya
damu na roho zao na wanangu
niliwapa kazi hya kuwamalizia wale waliokuwa
bado hawajakata roho vizuri.
Haikuwa kazi nyepesi sana kwasababu
ilichukuwa muda mrefu kupitia
kila behewa wakati polisi wakikaribia kufika ndio
tulikuwa tukimalizia kazi
yetu na moja kwa moja tulielekea kuzimu na
kuwa kabidhi damu nyingine.
“Nimekamilisha kazi yenu wakuu, naombeni
uhai wa mke wangu” “nenda
ukampulizie pumzi mdomoni kwa mwake”
niliondoka haraka nikikimbizana na
wanangu hadi nyumbani ambako nilikwenda
kubadilisha nguo na kuelekea kwenye
gari letu “Dickison utadrive (utaendesha) gari”
“sawa” tuliingia kwenye
gari na safari ikaanza kuelekea Muhimbili.
Tulifika hospitali na moja kwa moja
tulielekea katika chumba
alichokuwa amelazwa mke wangu mama Kabula
tulikuta madaktari wakiendelea
kutoahuduma “jamani mbona hivyo subilini nnje
basi mara moja” nesi moja
aliongea kwa utaratibu lakini hatukujari na
kueleka kitandani ambako
madaktari walinizuia “mheshimiwa tuache tufanye
kazi yetu” “no naombeni
mniache” nilijitetea lakini wakanishika na
kunirudisha nnje na kufunga
mlango kwa ndani.
Nilibaki nimechanganyikiwa sielewi ni fanye
nini, akali ilinijia
nimpigie simu Daktari mkuu ambaye naye alikuwa
hapatikani hewani.
Nikiwa katika mawazo niliona mlango
ukifunguliwa ndipo nilipoingia
kwa mara nyingine kwa kulazimisha “hivi
mheshimiwa kwanini usituache
tufanye kazi yetu?” “niachani nimwone mke
wangu ni mzima” niliongea kwa
ukari madaktari wakasimama pembeni wakijua
nimechanganyikiwa.
Nilifika pale kitandani nikaanza kuongea
maneno yaajabu kama
nikisali, niliinama na kumwekea midomo yangu
mdomoni mwake na kumpuluzia
pumzi yangu nilipomaliza nikamsii “amka mke
wangu” niliona mke wangu
akiamka utafikiri alikuwa katika usingizi mzito
sana, mimi na wanangu
tulimkumbataia kwa furaha madaktari
hawakuamini macho yao.
“mbona nipo hapa?” lilikuwa ni swali la
kwanza kabisa kutoka kwa mke
wangu “usijali mama Kabula tukifika nyumbani
utayajua yote” niliwaomba
daktari atuchunguze afya zetu kwa pamoja na
kwasababu tulikuwa tunazijua
afya zetu haikutupa shida majibu yalipokuja kuwa
sisi tumeathilika.
Daktari baada ya kuona vile alitushauri
tuanze kutumia dozi na
kumsihi mwanangu Kabula kuwa makini sana
kwa sababu mimba yake ilikuwa
kubwa sana na alikuwa akikaribia kujifungua
“binti unatakiwa wewe na
mwenzio kuhudhulia sana Clinic kwani unasiku
chache zilizobaki”.
Kwakweli kila nikifikili juu ya ujauzito wa
mwanangu
nilichanganyikiwa sana na sikupenda hata kidogo,
daktari alipoona amemaliza
alituruhusu kwenda nyumbani, tulielekea kwenye
gari ambapo Dickison
alitufungulia milango mimi na yeye tulikaa mbele
na Kabula na mamaake
walikaa nyuma na safari ya kurudi nyumbani
ilianza.
Tuliwahi kufika nyumbani kwasababu
hakukuwa na foleni sana
barabarani, ilikuwa ni siku ya furaha sana katika
maisha yetu kuona familia
inarejea nyumbani ila tatizo kubwa lililokuwa ni
ugonjwa hatari wa UKIMWI.
Tuliingia ndani nakundelea kusimliana jinsi
ilivyokuwa na kwa muda
gani ameteseka akiwa kitandani bila kujitambua
alisikitika sana kusikia
vile mke wangu lakini akakubaliana na hali halisi
nikamsihi afanye mpango
wa sadaka.
Vyombo vingi vya habari vilionyesha ajari
kubwa ya treni
iliyotokea mkoni Tabora watu wengi
walikusanyika wakisaidiana na polisi
kiitambua miili ya marehem “yote haya ilikuwa ni
kuokoa misha yako mke
wangu”, “nashukuru sana mme wangu” “itabidi
tutume salam za lambi lambi”
“ni kweli” tulishaulina hivyo na tukafanya hivyo
ilimradi kujitengenezea
jina kwa wananchi.
Maisha yaliendelea huku tukizingatia sana
kutumia dawa na ushauri
wa daktari na kulitumikia upya taifa letu na
kuhakikisha kila palipokuwa
pameyumba palianza kukaa sehemu yake kama
ilivyokuwa awali.
Afya zetu zilirudi mahali pake nilianza tena
michezo michafu ya
kuwarubuni wanaume kwa kuwapa pesa na
kuwaingilia kimwili ili na mimi
kuueneza uonjwa tena kwa kasi ya ajabu.
Siku moja nikiwa hotelini na njemba moja
miraba minne nikiwa
nafanyanalo mapenzi haramu simu yangu iliita
alikuwa ni mama Kabula lakini
sikujali nikaikata kabisa mlio nikaendelea kupewa
penzi chafu na la yule
jamaa, baadaye nilipo maliza tulienda kuoga
wakati tukiwa bafuni tulianza
tena kupeana raha na yule shoga mle bafuni
baadaye nilimpa pesa na kuondoka
kuelekea nyumbani.
Nikiwa kwenye gari nilikumbuka mke wangu
alikuwa akinipigia simu
kuangalia nilikuta missed call za mke wangu 17
na meseji 12 kuwa mtoto
ameshikwa na uchungu hivyo amepelekwa
hospitali ya Muhimbili ilibidi
nigeuze gari na kuelekea hospitali kama nilivyo
pewa taarifa.
Moja kwa moja nilielekea chumba maalum
walicho nielekeza lakini
sikuruhusiwa kingie nilimkuta mke wangu amelia
amechoka “ulikuwa wapi muda
wote?” “nilikuwa na kikao, vipi anaendeleaje?”
“sielewi chochote muda wote
wameniweka tu hapa” mlango ulifunguliwa alitoka
daktari “aaaah Mheshimiwa”
“ndio dokta, vipi hali ya mwanangu” dakrtari
alisita kujibu haraka kama
kulikuwa na kitu “tweni ofisini mheshimiwa”
tukamfwata nakuelekea ofisini
kwake.
Dokta alionyesha kama kunajambo hivi
lakini akawa anafikilia aanze
vipi kuongea “docta vipi kunatatizo?” ilibidi
nimchokoze “aaaah yap lakini
unahitaji kuwa na moyo mkubwa mkuu” niliona
kama ananichanganyia habari
“kwani kuna nini? Hata usijari dokta ongea”
“sawa, aaaah binti amejifungua
salama ametuletea mtoto wa kiume” tulifurahi
sana kusikia vile hasa
mwanangu Dickisoni aliyekuwa amesimama
nyuma ya kiti nilichokuwa nime kaa.
“kwahiyo vipi kuhusu hali yake?” niliona
dokta ameinamisha kichwa
chini na kuvuta pumzi nilihisi kuna jambo “dokta
vipi?” “taarifa mbaya ni
kwamba wakati binti akijifungua amepoteza damu
nyingi sana hivyo yeye
amefariki dunia” taarifa ile ilitushitua sana hali
iliyo mfanya mke wangu
Janeth kuanguka na kupoteza fahamu pale pale.
Tulimbeba mke wangu na kumlaza kitandani
na daktari aliendelea
kumhudumia mimi na mwanangu Dickison
tukaenda kuangalia mwili wa marehemu
ambao tayari ulikuwa umepelekwa Mochwari
Dickison alionekana
kuchanganyikiwa sana wakati mimi nilianza
kufikiria mke wangu asija lala
tena ule usingizi mzito aliokuwa ameupata
nilipokuwa nimempiga kibao
akaanguka.
Tulirejea katika sehemu alikokuwa
amelazwa mke wangu ambako
tulimkuta akiwa amerejewa na fahamu ila alikuwa
akilia na manesi
wakimbembeleza “mke wangu, nipigo kubwa sana
kuondokewa na kipenzi chetu
Kabula lakini naomba ujikaze ilitaratibu zingine
ziendelee” pamoja na
maneno yale mke wangu ndio alizidi kulia zaidi.
Tulisambaza taarifa sehemu mbali mbali
maandalizi ya msiba
yalifanyika na siku ya pili yake ndipo mwili kivuli
wa mtoto wangu kabula
ulizikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam ambapo watu
wengi walihudhulia msiba wa mwanangu.
Usiku ule ule wa msiba, watu walikuwa
wamelala tuliubeba mwili
halali wa mwanangu na kwenda kula nyama yake
katika maeneo ya bichi iliopo
maeneo ya mbezi.
Msiba uliisha lakini mke wangu alikuwa
katika majonzi na ilichukua
muda mrefu sana kuzoea, siku zilienda huku
tukiendelea kumlea mtoto wa
marehem mwanangu Kabula ambaye naye
alionekana alikuwa amezaliwa na
maambukizi ya virusi vya UKIMWI hivyo alikuwa
akisumbua kwa kuugua ugua
kila mara.
Bila kujali Edina alikuwa ni mjukuu wangu
lakini sikuwahi kumpenda
hata siku moja kwani wanangu walinitia aibu
sana kila nikitafakari kitendo
walichofanya watoto wa baba mmoja.
***********************
Nilizidi kujiimarisha na kusimama zaidi
katika idara ya uchawi na
ushetani na kulitangaza jina langu nchini kama
mfanya biashara mkubwa sana
duniani na kufungua vyombo vyangu vya habari
zilivyo kuwa vikihubiri injiri
nilifungua Redio, Magazeti mawili na TV moja.
Kazi nzito nilipewa kuzimu ni kuwateka watu
wasimwamini Mungu na
kuamini kuwa mkuu wa dunia ni Lusifa (Shetani)
na anauwezo mkubwa kitu
kilichowafanya wafanyabiashara wengi kuingia
katika dini yetu na moja kwa
moja nikawa msajili mkuu wa dini yetu
iliyotambulika kwa jina la Freemason.
Mkutano mkubwa wa Injiri nchini Tanzania
ulikuwa ukiandaliwa na
makanisa mbalimbali hivyo viongozi mbali mbali
wadini kutoka nchi za jirani
walialikwa hivyo hivyo pia na sisi kwa upande
wetu tulikuwa tukijipanga
kwaajili ya kuaribu mkutano usifanyike.
Vyombo vingi vya habari nchini Tanzania
vilitangaza mkutano ule
utakao fanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja
jijini Dar es Salaam na
waimbaji mbalimbali watakao tumbwiza siku hiyo
na baadhi ya waimbaji
maarufu walikuwa wapo katika chama chetu na
baadhi ya wachungaji
walioalikwa nao walikuwa ni wana chama wetu.
Kwakuwa nilikuwa nina vyombo vya habari
na nilikuwa nikitoa
misaada mingi nchini basi nilialikwa kama mgeni
rasmi na mfunguzi wa
mkutano ule.
Ilibaki siku moja ili kufanyika kwa
mkutano ule tuliweka kikao
na kupanga jinsi gani tuta haribu mkutano na
kuteka watu ili waingie katika
dini yetu ya Freemason, tulipanga mambo mengi
sana na kupanga jinsi
watumishi wa mungu ambao wapo katika chama
chetu watakavyo tufanikishia
zoezi letu.
Siku ilikuwa imewadia nikawa naelekea
mkutanoni kama mgeni rasmi
nikiwa na mke wangu kipenzi Janeth tulikuwa na
gari letu jipya ambalo
tulipewa zawadi Nigeria lakini gari lile halikuwa
gari alikuwa ni mnyama
pori ambaye ni Tembo aliyekuwa amenenepa
sana.
Watu wengi walilishangaa gari langu kwani
wao walitumia magari ya
kawaida na katika maisha ya kawaida watu
wengi huona ni magari lakini si
magari asilimia kubwa ya magari barabarani ni
wanyama pori na wasio na
macho ya kawaida ni vigumu kutambuwa kitu
kama hicho.
Tukiwa maeneo ya Kalume mkoa wa Ilala
nikitokea barabara itokayo
Buguruni kwenda Posta kupitia Karia Koo
nilimwona mwanangu Dickison akiwa
juu ya Kifaru aliyeonekana ni gari katika macho
ya kawaida.
Yule kifaru alikuwa katika mwendo kasi
akija katika gari letu
akitokea barabara itokayo Temeke kwenda
Kinondoni nilijaribu kumkwepa
lakini haikuwezekana na moja kwa moja Yule
kifaru aliligonga gari letu pale
pale nilipoteza fahamu na sikujua tena
kinachoendelea.
Fahamu zilianza kunirejea baada ya kusikia
mwili ukiwaka moto na
maumivu makari sana niliyokuwa nayapata,
“ahaaaaaaaaaaa” nililia kwa sauti
na nilipofumbua macho niligundua nilikuwa
hospitali ya Muhimbili na
wachungaji wengi walikuwa wamenizunguka pale
kitandani huku wakiniombea
“tokeeni…..” niliongea kwa ukari lakini waliendelea
kusali.
Mwili ulianza kutetemeka kila nikisikia jina
la Yesu nilizidi
kuungua ghafla nikasikia sauti ya juu
“haleluyaaaaa” ilikuwa ni sauti ya
Dickisoni wote waligeuka na kumtazama
“ameeeni” baadhi yao walijibu “nina
shukuru sana kwa maombi yenu, mwenyezi
mungu kuna kitu ameniambia
nizungumze na babaangu naombeni mnipishe
dakika moja” wale wachungaji wa
chama chetu walimsapoti na wengine walipinga
lakini kwasababu wa chama cha
Lusifa walikuwa wengi basi walipitisha mswaada
na kutoka njee.
“Dickison mwanangu kwanini unataka
kuniuwa?” “hahahaha baba
nahitaji kurithi kiti chako kama mlivyo mfanyia
mamaangu na hapa nimekuja
kuitoa roho yako tu”. “mamaaaaaaaa” nilipiga
kelele mlango ukafunguliwa
wachungaji wakaingia ndani Dickison akaanza
kushindana nao akisaidiana na
wale wachungaji wengine waliokuwa katika
chama chetu.
Sikuamini kuona nimesalitiwa na mwanangu
wa kumzaa mwenyewe tena
niliye mpenda sana na kupa uwezo alikuwa nao,
kwa kuwa sikuwa na nguvu za
kunyenyuka pale kitandani nilibaki nikishangaa tu
huku nikilia mwenyewe.
Niliona Dickisoni akiishiwa nguvu na
kudondoka chini baadaye wale
wachungaji feki walifwaatia ndipo nilipoamua
kujibadilisha na kuwa nyoka
ili nipambane mwenyewe, kitendo kile kiliwafanya
wachungaji walee wa ukweli
kuongeza kasi ya kuomba na kukemea kwa
nguvu zote.
Ilichukuwa muda mrefu sana nikiwasumbua
kwa kujibadilisha mara kwa
mara kwa kujifanya mnyama pori lakini baadaye
nilipigwa na mwanga mkubwa
usoni kwangu ulionifanya nianguke chini na
kupoteza fahamu.
Fahamu zilianza kunirejea nilijikuta nipo
chini na nimezungukwa
na wachungaji pembeni nilimwona mwanangu
Dickison ameshikana mikono na
mwanae Edina huku wakilia, nilijiona nimekuwa
mwepesi sana.
“haleluyaaaaa jina la bwana lihimidiwe”
mchungaji moja aliongea
ghafla nnje mvua ilianza kunyesha ngurumo za
radi zilisikika upepo mkali
ulivuma kitu ambacho kilikuwa kigeni machoni
mwa watu nilisimama kwa
wasiwasi na kwenda kumkumbatia mchungaji
aliyekuwa karibu yangu “wanakuja
kunichuwa, wanakuja kunichuwa” niliongea huku
nikiogopa.
Wachungaji waliongeza kasi ya kuomba
“jamani kunanguvu ya ajabu
mahali hapa kazaneni kuomba”, watu waliomba
sana na baadaye mvua ilitulia
hali ikawa sawa nilimwona mke wangu Janeth
akiingia ndani na wachungaji
wengine, niliinuka na kumkimbilia mke wangu na
kumkumbatia wakafwatia
Dickisoni na mwanae tukawa tunalia tu.
“hamnabudi kumshukuru Mungu kwa
uponyaji jambo la msingi ni
kumpokea yeye na kukiri kuwa ni bwana na
mwokozi wenu ilimsitafutwe tena na
Shetani” mchungaji mmoja alishauri huku
akitungalia usoni “je mpo tayari?
Na kama mpo tayari pigeni magoti chini ili
niwzez kuwaongoza saara ya toba”
mke wangu alikuwa wa kwanza kupiga magoti
akafwatiwa na Edina, Dickison
naye alipiga magoti ndipo na mimi nilipopiga
magoti na zoezi la kuongozwa
sala likaanza.
Baada ya kumaliza sala ya toba ikabidi
tuhamie nyumbani kwani
usiku ulikuwa umeingi na watu wengi walijaa
eneo lile la hospitali
wakishuhudia maajabu yaani hospitali ya
Muhimbili siku hiyo iligeuka kuwa
ndio sehemu ya mkutano.
Safari ya kwenda nyumbani ilianza tukiwa
tumepanda gari la Mchungaji
David wakati gari nyingine zilitufwaata nyuma
yetu ambapo moja kwa moja
tulifika nyumbani ambako maombi yalianzia pale
getini.
Milio mingi ilisikika ikitokea ndani na
baadaye kutulia, tuliingia
ndani na timu nzima ya maombi huku watu
wakisali na baadaye walianza kuomba
tena kwa nguvu na kwa kukemea kwa jina la
Yesu hivyo hivyo na mimi na
familia yangu tuliendelea kuomba kwa kumkataa
Shetani.
Nyumba ilianza kutetemeka utafikiri
kulikuwa na tetemeko la ardhi
likipita “puuuuuuuh” nyoka mkubwa aina ya chatu
alianguka kutoka dalini na
kuangukia meza ilikuwa katikati na kuivunja, vioo
vya meza ile vikauka na
kutawanyika.
Yule Chatu alikuwa ni mkali lakini Mchungaji
David na wenzake
hawakuonyesha woga wowote na kushukuru
“ahsante Yesu” huku wakikemea vikari
yule nyoka alianza kubadilika na kuwa Chui mara
Paka baadaye yule nyoka
alitoa mlio mkubwa na kuyeyuka kuwa moshi
mweusi na kupotea kabisa eneo
lile.
Maombi yaliendelea hali ikawa imetulia baada
ya muda na wachungaji
walimaliza kusali “bwana Yesu asifiweee” Mch.
David aliongea kwa furaha na
wote tuliitikia “nijambo la neema sana ndugu
zangu Mungu aliye hai siku
zote hashindwi kitu ameeni?” “ameeeni”
nilimtazama mke wangu alikuwa akilia
na kuonyesha kuguswa zaidi na maneno ya
Mch.David ambaye aliongea vitu
vingi sana na vya msingi ambavyo vingetusaidia
katika maisha yetu mapya ya
wokovu.
Kila kitu kilipokuwa kimekaa sawa
wachungaji waliondoka na
kutuacha pale nyumbani tukiwa watu wapya
kabisa, hatukuogopa kitu kabisa
kwani Mchungaji David alitushauli mambo mngi
na kutuachia Biblia kila mmoja
wetu.
Asubuhi kulikucha na tuliamka tukiwa
salama kabisa Mchungaji David
na wnzake walikuja kututembelea na kutualika
kufanya rasmi uzinduzi wa
mkutano wa Injiri ulio kuwa umepangwa
kufanyika katika viwanja vya Mnazi
mmoja na mimi ndio nilipewa dhamana na Lusifa
kuuaribu mkutano ule lakini
matokeo yake nikajikuta nikiokoka mimi na
familia yangu.
Tuliongea mambo mengi na tukapata
kifunguwa kinywa kwa pamoja na
kuendelea kufanya maombi pale nyumbani, nje ya
geti la nyumba yangu
kulikuwa na waandishi wa habari pamoja na watu
wengi wakisumbua na kutaka
kuniona lakini wakaambiwa wafike katika
mkutano utakao fanyika katika
viwanja vya Mnazi mmoja kuanzia saa 9 alasili
hadi saa 12 jioni ndio tamati
yake.
Muda ulipokuwa unakaribia tulielekea katika
mkutano wa Injili
ambapo tulikuta watu wengi wamefurika katika
viwanja vile walipoona tu
magari yanaingia watu walipiga kelele
nakushangilia, waandishi wa habari
walikuwa bize kupiga picha bila kupumzika.
Katika mkutano ule mimi na familia yangu
tulikuwa kama vivutio
vikubwa sana kwa watu maana jinsi walivyokuwa
wakiangaika kunitazama
niliamini kabisa Mungu alikuwa na makusudi
yake.
Tulieleka jukwaani na kuketi baadaye mc
alitangaza na kuniomba
niufungu mkutano ule, nilisimama na kulekea
mbele ya jukwaa nikasalimia
“bwana Yesu asifiweeee” uwanja mzima uliitikia
“tufunike macho tuombe”
nilifungua mkutano kwa saala na kuwaachia
waongozaji waendele.
Watu walikuwa bado wakisumbua wakitaka
kujua historia ya maisha
yangu ndipo nilipo pewa nafasi ya kuushuhudia
umati maajabu ya Mungu katika
maisha yangu, nilianza kuwaeleza tangu nauza
madawa ya kulevya
nilipokamatwa na kufungwa jinsi nilivyo pata ajari
iliyo nipeleka katika
JELA YA KICHAWI na mateso tuliyo yapata jinsi
nilivyompata mke wangu Janeth
na kuzaa naye pamoja na mamaake mzazi.
Niliwaeleza watu jinsi nilivyo jiingiza
kwenye tabia za Ushoga za
kuwageuza wanaume wenzangu ni wake zangu,
nilijiona mkosaji sana
nilimfwaata mke wangu na kupiga magoti
nikimwomba msamaa kwani mimi ndiye
niliye uingiza ugonjwa hatari wa UKIMWI katika
familia.
Mke wangu alilia sana na kusimama
akaondoka wachungaji walimfwata na
kumbembeleza wakati huo mimi nililala chini
nikilia baadaye niliokotwa na
kusitisha mkutano mbaka siku inayofwaata
ambayo nitasimama na mke wangu
pamoja na familia yangu ili kuwaeleza mambo
mengine.
Nilirudishwa nyumbani juu ya ulinzi mkali
nilimkuta mke wangu na
wachungaji nilishangaa kuona mk wangu
amenipoka vizuri tofauti hata vile
nilivyo kuwa nafikiria “nisamehe sana mke wangu
natambua nimewakosea sana
lakini nahitaji msamaa wenu” “usijari mme wangu
yamekwisha na kesho
tutakuwa wote katika mkutano, nilifarijika sana
kusikia vile na kuwashukuru
sana wachungaji ambao nao walinambia
“usitushukuru sisi ila mshukuru
mwenyezi Mungu kwa kukukomboa” Mch. David
aliwakilisha.
Usiku tulilala tukiutafakari ukuu wa Mungu
na jinsi alivyo tuokoa
katika kifungo cha giza “mke wangu juma tatu
itabidi twende Iringa
nikamsalimie mamaangu nimemkumbuka sana”
“sawa haina shida, sijui
atajisikiaje kukuona” “hata sielewi wapo hai au
laa, maana ni muda mrefu
sana umepita, isitoshe vyombo vyote vya habari
nchini vinaelezea maisha
yetu inamaana hatuoni?” “siunajua kule ni kijijini
mme wangu, tumwombe
Mungu tu” tuliongea mengi usingizi ukatupitia.
Juma pili ilifika muda ulikuwa tayari moja
kwa moja tulielekea
mkutanoni na kuona watu wamejaa mara nne
tofauti na walivyokuwa jana yake.
Mchungaji David alikhubili na baadaye kutupa
muda wa kuendela kutoa shuhuda
na sikuu hii tuliongea wote huku tukipokezana
pamoja na mwangu Dickison na
mjukuu wetu Edina ambaye alizaliwa na mtu na
dadaake.
Wengi walikuwa wanaguswa sana na stori na
baadaye tuliuliza wangapi
wapo tayari kuokoka baada ya stori kuisha
niliona karibu watu wote
wamenyoosha mikono ndipo nilipo mwachia Mch.
David aendelee na zoezi la
kuongoza saala ya toba kwa walionyoosha
mikono.
Nilimshukuru sana Mungu kwa kunifanya
niwe mtumishi wake ndipo
nilipo amua kutoa vyombo vyangu vya habari
katika makanisa ya kikristo na
baadhi ya miradi yangu pia.
Mkutano ulimalizika, tulipiga picha na watu kasha
nililejea nyumbani
kujipanga na safari ya kuelekea Iringa asubuhi
kukicha mapema.
Asubuhi na mapema tulielekea stendi kuu
ya mabasi yaendayo mkoani
Ubungo ambako nilimkuta Mch. David na timu
yake walijitolea kunisindikiza,
nilifarijika sana na walikuwa wamekwisha kukata
tiketi moja kwa moja
tuliingia kwenye gari na kuketi na safari ikaanza.
Nikiwa kwenye gari niliona kama sifiki kwani
nilimmisi sana mamaangu
na dadaangu ambao niliwaacha katika mazingira
magumu sana “unawaza nini
baba?” “aaaah namfikiria mamaangu na
dadaangu ntafurahi sana nikiwaona
maana ni muda mrefu umepita”.
Saa tisa na dakika arobaini na tatu ndio
tulikuwa tunashuka kwenye
basi aina ya NEW FORCE stendi ya Mafinga mjini
ambako niliona kama
kumebadilika sana.
Moja kwa moja tulikodisha Taksi tatu na
safari ya kwenda kijijini
kwetu Ndolezi ilianza,tulitembea mwendo wa saa
moja kwa mbali niliona
kijiji “tuna karibia kufika, nyumbani ni pale mbele”
nilimwonyesha dereva
Taksi.
Wakati tunakaribia niliona watu wamejaa
nnje ya nyumba yetu “kuna
nini mbona watu wamejaa vile?” “inaonyesha
labda kuna msiba” dereva
alinijibu huku akipaki gari niliona makaburi manne
mbele ya nyumba yetu
wakati mimi naondoka niliacha kaburi moja la
marehem babaangu, nilianza
kuchanganyikiwa.
Niliruka kwenye gari na kukimbilia kwenye
yale makaburi ambapo
niliona kaburi la kwanza lilikuwa la babaangu,
kaburi la pili lilikuwa
limeandikwa jina langu na kaburi la tatu lilikuwa
limeandikwa jina la
daangu na la mwisho ndilo lililoniumiza zaidi
baada ya kuona jina la
mamaangu na kaburi lilionyesha wametoka
kumzika mamaangu dakika chache
zilizopita.
Nililia kama mtoto mdogo wakaja watu na
kujaribu kunibembeleza bila
mafanikio siku hiyo ilikuwa ni siku mbaya sana
hatasikuondoka pale kaburini
mbaka asubuhi, wachungaji wangu walinishauli
na kunambia ni mambo ya kupita
tu na kunipa pole nyingi wakitolea mfano kupiti
Ayubu aliyepata majaribu
mazito zaidi
Tulikaa na wazee wakitaka kujuwa siku
zote nilikuwa wapi ambapo
niliwaeleza kila kitu bila kuficha na kilichoniumiza
nipale nilipoambiwa
mama amefariki dunia kwa kukosa pesa ya
kumpeleka hospitari wakati mimi
nina mahospitari nchini jambo ambalo niliamua
hospitali zangu zote
nikabidhi makanisa ili yatoe huduma.
Tuliudhulia siku zote za msiba watu
walimiminika pale kijijini kuja
kuniona baada ya kunisikia sana katika vyombo
vya habari na siku ya mwisho
ya msiba ilibidi niwashukuru wanakijiji kwa
msaada wao na nyumba
kulikabidhi kanisa alilokuwa akisali mamaangu
kisha safari ya kurudi jijini
Dar es Salaam ikapangwa.
Asubuhi na mapema safari ya kurudi Dar
es Salaam ilianza siku hiyo
nilimfikiria sana Mwenyezi Mungu kwa mambo
aliyonotendea mbaka nilipofikia.
Maisha yaliendelea huku nikipata mialiko
mingi sana katika mikutano
ya Injili nnje ya nchi na ndani ya nchi. Tuliishi
kwa kulitangaza jina la
Mungu na baadaye tukawa wahubili maarufu
duniani na kubadilisha maisha ya
watu wngi sana.
Katika maisha ya wokovu tuliishi maisha
mazuri naya furaha lakini
siku zote tulizingatia sana dozi tulizokuwa
tukitumia ili kupambana na
madhara ya virusi vya UKIMWI ugonjwa tuliokuwa
tunaishi nao.
Watu wengi walipenda maisha yetu,
mapenzi yangu kwa mke wangu
yaliongezeka na maisha tuliishi yalikuwa ni ya
furaha sana.
Mwenyezi Mungu hashindwi kitu na ni
mwema jina lake liiidiwe
Ameeni.
We are sincere Government well registered and certified private moneylender permitted to render financial assistant to individual and cooperate bodies, ranging from the Amount of $1,500 to $50,000,000 Million Dollars ,Euro and Pounds with long loan repayment period of 1 year to 50 years. Loan Available now are Business, Personal, House,Travel and Student Loans. Apply for a loan today. Its Easy and fast to get at 3% interest rates and monthly installment payments. Check-out this great offer. If you are interested do get back us with these information,Your Name: Address:City:Country:Phone:Amount Needed:Loan Duration: Contact via email.bayportsaservice@gmail.com to proceed.
JibuFutagadi mlwilo from Tanzania phone +2557556659 / +255715971027
Futa