RIWAYA JELA YA KICHAWI SEHEM YA TATU FATILIA UONE JANETH ALICHO MFNYIA JOSEPH WALIKOELEKEA TWEZETUUUU

RIWAYA JELA YA KICHAWI
MTUNZI GADI MLWILO
Whatsap 0755665931
Sehem ya tatu

ILIPOISHIA......
Tukiwa bado tunashangaa nnje
mlango wa kile kibanda ulifunguliwa ,
aliingia Yule kisura aliye nipiga na mkia
siku ya kwanza nafika pale “Joseph njoo” nikaanza kutetemeka
akanisogelea na kunishika bega
nilijikuta nipo juu ya mbwa akikimbia porini kwa woga nikawa nimemkumbatia
nisianguke. 


SONGA NAYO.....

“ashilaaaaashi” Yule mrembo
aliongea kitu nisicho kijua Yule mbwa
akasimama tukashuka “tukae pale”
alionyesha kwa kidole, tukaketi kwenye
gogo “naomba usiniogope” nikatikisa
kichwa huku hofo ikinitawala
“nimesikia wewe ni mtu wa Mafinga” aliniuliza swali “ndio” mimi naitwa Janeth ni mtoto
wa pekee katika familia yetu naaaaa ni
mzaliwa wa Iringa Ndolezi”
nilishituka kusikia vile “na wakati
nikiwa mdogo wazazi wangu
walifukuzwa pale kijijini wakidhaniwa ni wachawi” nilikumbuka kitu kilichotokea miaka ya nyuma pale kijijini “inamaana wewe ni mtoto wa Kinyunyu?” “ndio”.

Nilikumbuka nilipokuwa mdogo
nilikuwa na rafiki aliitwa Janeth, Janeth
alisimama na kunikumbatia “Jose wewe
ni rafiki yangu wa utotoni na siku
zote nilikuwa nakufikiria sana” aliongea
Janeth kwa sauti ya chini huku
machozi ya kimtoka “usijari naomba
usilie” nilimbembeleza Janeth akiwa
bado amenikumbatia mwili wangu ulianza kusisimka kwa joto nililo lipata kutoka kwa Janeth na hasa maziwa yake yalivyo kua yamesimama yakinichomachoma kifuani kwangu.

Janeth alikuwa ni mrembo wa Dunia
pasipo kujijuwa, umbo lake jinsi
lilivyo umbika utazani kajitengeneza
mwenyewe Janeth alikuwa ni mzuri
kiasi kwamba ukisema umwelezee sifa zake utakesha kwa kusimulia bila kummaliza.

“Janeth” “abee” aliitika kwa sati ya
chini “baba mbona sijamwona yuko
wapi?” swali hilo lilimfanya janeth abadilike na kutia huruma zaidi huku machozi yakizidi kumtoka, "Jay nimekuuliza mbona unakuwa ivyo tena kwa nini tatizo???" Janeth iliinuwa uso wake na kuniangalia kisha akajibu kwa uchungu “usijari Joseph ila mama alimtoa kafara babaangu ili yeye
amiliki himaya ya kichawi pale
kijijini” alinijibu kwa huzuni zaidi
“inamaana yule ndio mamaako mzazi?”
“ndio na ninamchukia sana mama kwa
kumuua baba” “Janeth nahitaji msaada
wako na sikia sisi ni wakufa tu katika
kijijini chenu?” “usijari mimi
ntakusaidia na nimefurahi sana
kukuona na ningependa siku moja tuishi
pamoja, naaaah muda umeenda
tutaongea kesho twende tuondoke” kwa kweli sikutaka tena kurudi kule kijijini lakini haikuwa kazi kubwa kwa Janeth
alinishika bega nikajikuta nipo
juu ya yule mbwa na baada ya muda mfupi nikikuwa ndani ya kibanda.

Wakati Janeth anatoka mlangoni
kulikua na mbwa mweusi amekaa
“mama!!!” Janeth aliita kwa mshangao, yule mbwa akabadilika na kuwa mtu niliogopa kumwona yule mama “umetoka wapi?” “ndani” Janeth alimjibu mamaake huku akiondoka “wewe kuja hapa” yule mama aliniita akininyoshea kidole mimi nilimsogelea huku mwili ukitetemeka “mimi unanikumbuka?” aliniuliza swali nikakataa kwa kutikisa kichwa “aah haa safi umekua kijana mzuri sana na endapo utafwata masharti yangu basi
huto kufa” aliongea maneno yasio
eleweka na kuondoka mle ndani.

Nnje watu walikuwa wachache
ilinibidi nianze kuwaeleza yalio tokea
huko niliko kuwa na Janeth “dah
afadhari mwenzetu hutokufa” kimoti
aliongea maneno ya huruma sana “usiseme hivyo kimoti jambo la msingi tuangalie tutajitoa vipi humu kibandani mbona bado tupo pamoja?” “ni kweli” Chazi alinisapoti kwa niliyoyaongea naye.

Ilikua asubuhi tulishitushwa na
kelele za watoto nilipoangalia nje
nilistuka sana kuona watoto wakikimbia
angani huku wakigombania kichwa cha
binadamu, kwa mshangao niliwatazama
wenzangu nikagundua kimoti alikuwa
akilia uso wake ulilowa machozi “Kimoti
vumilia brother, amini yatakwisha”
“hapana mdogo wangu sifikirii kifo
changu ila naikumbuka familia yangu
istoshe mke wangu nilimwacha na
ujauzito sielewi wapo vipi na wanaishi
vipi….??” Kimoti aliongea kwa uchungu
sana mpaka alinitoa machozi “jamani
kila mmoja anamakubwa yake hapa sasa sidhani kama kulia kutasaidia jambo la msingi tuangalie tutajiokoa vipi” aliongea babu Ally kwa ujasili wa
kulazimisha kama hakuwa na hofu
moyoni mwake.

ITAENDELEA KESHO SAA TATU ASUBUHI
Utamu ndio kwanza unaanza ndani ya jela ya kichawi tukutane kesho saa tatu panapo majaaliwa

Hakuna maoni