RIWAYA: JELA YA KICHAWI Sehem ya pili Utamu unaendelea

RIWAYA: JELA YA KICHAWI
MTUNZI:GADI MLWILO 
Sehem ya pili

ILIPOISHIA....
Walinikamata na kunifunga katika
miti iliyopangwa kama kichanja na
safari ya kule kule bondeni nilikokuwa
nataka kwenda ndiko tulikoelekea,
“anaweza akatumika kesho eh?” “mmmh
sidhani maana bado wapo kama saba
hivi”
“natamani sana hata angetumika leo
huyu” sikuzielewa stori zao ila zilizidi
kunitisha na kunichanganya akili yangu.
“mamaaaaaaaaaah” nililia nilipoona
kichwa cha mtu kimeshikwa na mtoto
akichezea kwa mbele ngozi ya
binadaamu ilikuwa imeaanikwa, wale
jamaa wakawa wanacheka sana “aaaaaaaaah” nililia tena baada ya kubamizwa chini kama mzigo wa kuni mbaka vumbi likatoka.

SASA ENDELEA KUSONGA NAYO....

“CHIKATEEEE” mmoja wa wale
jamaa aliongea hilo neno kwa sauti ya
juu, baada ya muda mfupi watu waliwasili na kunizunguka “ha-ha-ha-ha-ha-ha” kilikua ni kicheko cha mama mmoja wa makamo akinisogelea wakati nimelala pale chini “kijana unaitwa nani? Na ni mwenyeji wa wapi?” alinitupia swali yule mama “naitwa Joseph Mponzi wa Iringa Ndolezi” “mponzi…!!!!!!!”
aliitikia kwa mshangao kama alinijua
vile “Ndolezi, Mponzi!!!” alijisemesha
huku akishika kichwa “vipi
unamfahamu? Mzee mmoja alimtupia
swali lakini akakana kwa kutikisa kichwa
“mpelekeni kwa wenzake”.

Alisogea binti mmoja akiwa ameziba
sehemu zake za siri tu huku kifua
chake kikiwa wazi alikua anaumbo zuri
hatasikumwelewa kwanini aliyachagua
maisha yale hali alikuwa mzuri kiasi
kile hata angeamuwa kugombea miss
Dunia yawezekana angeweza kushinda,
yule binti alikuwa na bilauli mkononi
na mkia kama wa ngombe, aliuchovya
ule mkia na kunipiga nao usono kisha
wale jamaa wakanibeba na kunipeleka
waliko agizwa.

“Joseph!!!!!!” “babu Ally!!!!”
nilishangaa sana kumkuta babau Ally
katika kile kibanda cha miti kilichokuwa
wazi na upande mwingine ulizibwa
kwa maboksi, Babu Ally alinikumbatia
kwa nguvu.

“vipi kijana?” “mzee nashindwa
kuelewa kwanini wanatufanyia hivi
hawa watu na umefika vipi huku babu?”
“mjukuu wangu kama nilivyo chukuliwa
vile pale shambani” tuliongea mambo
mengi sana na babu Ally nikawa nalia tu
“kijana vumilia, kulia haina maana
yeyote ile sisi ni vitoweo tu kwa hawa
mbwa…..” “no Kimoti usiseme ivyo
jambo la msingi nikuangalia tunajinasua
vipi mikoni mwa hawa watu” yalikua ni
mabishano ya Kimoti na Chazi ambao
walikua ni wafungwa nilio wakuta mle
ndani na nilipokua kule gerezani
nilisikia stori zao kama nao walikuwa
pale na walichukuliwa katika
mazingira tatanishi.

Niliwaza mambo mengi sana,
usingizi ukanipitia nikaja kushitushwa
na kelele za watu nnje “vipi tena??”
niliuliza wenyeji wangu “shiiiiiiiiiii
ndo mida yao ya kula hii subiri uone
maajabu” Kimoti alinijibu nikawa
nasubiri nione nini kitafanyika.

Watu walikusanyika pale nnje ya kile
kibanda watoto, vijana, watu wa
makamo na wazee mkononi wakiwa na
sahani. Ililetwa miili ya wanawake
wawili na kulazwa chini ikiwa uchi wa mnyama “Bony…..” “naaam” “Sonyo…” “naaam” “haraka fanyeni ibada watu waweze kula tumechelewa leo” alikuwa ni mama mmoja akiamrisha ibaada ifanyike.

Walitokea njemba wawili waliojazia
wakiwa nao kama walivyo zaliwa na
chupa mikononi. Walitoa vitu katika zile
chupa na kupaka katika nyeti zao
na kupaka katika sehemu za siri za ile
miili ya wale wanawake, sikuamini
tendo linalotaka kufanyika wakati ule,
yani hata mshipa waaibu hawakua nao
wale jamaa wakaanza kufanya mapenzi
na zile maiti “mamaaaa hivi hawa jamaa
wakoje?” “subiri kijana bado utaona
makubwa zaidi” babu Ally alinijibu kwa
sauti ya upole.

Tukiwa bado tunashangaa nnje
mlango wa kile kibanda ulifunguliwa ,
aliingia Yule kisura aliye nipiga na mkia
siku ya kwanza nafika pale
“Joseph njoo” nikaanza kutetemeka
akanisogelea na kunishika bega
nilijikuta nipo juu ya mbwa akikimbia porini kwa woga nikawa nimemkumbatia
nisianguke.
ITAENDELEA KESHO SAA TATU PANAPO    MJAALIWA. Share kwa washikaji

Hakuna maoni