P Square wamzika baba yao leo Mr.Okoye aliyefariki 24 november 2014 jambo ambalo limewashitua wengi

Katika hali iliyowashtua watu wengi kuwa baba mzazi wa mapacha Peter na
Paul wa kundi la P-Square la Nigeria,
Mr. Moses Okoye aliyefariki dunia
November 24 mwaka jana hakuzikwa
mpaka sasa.

Mzee huyo anatarajiwa kuzikwa leo
Ijumaa January 30 huko nyumbani
kwao Ifite Dunu, Anambra State.

Haijajulikana bado sababu za
kuchelewa kumpumzisha mzazi wao,
lakini baada ya Mr. Okoye kufariki
mapacha hao waliendelea na maisha
yao mengine ya kawaida na kimuziki.

P-Square wamempoteza baba yao
ikiwa ni miaka miwili toka
waondokewe na mama yao Mrs
Josephine Okoye aliyefariki July 11,
2012.katikati ni mzee okoye na wanawe wakiwa wanaenda kumzika mama yao
mzee okoye enzi za uhai wake

Hakuna maoni