RIWAYA JELA YA KICHAWI
MTUNZI GADI MLWILO
WHATSAP 0755665931
ILIPOISHIA......
Nilipata dili ya kupeleka mzigo
China, mipango yote ikawa sawa usiku
nilipelekwa kwa daktari aliye nifanyia
operation na kuniweka madawa
tumboni. Safari ya kwenda china ilianza
na katika viwanja vingi vya ndege
nilipita safi lakini nilipofika China watu
ambao ilibidi waje kunichukuwa
walikuwa hawaja fika mwili ulikuwa
umeanza kupoteza nguvu na baadaye
nilianguka chini na kupoteza fahamu.
SONGA NAYO ....9
Fahamu zililejea nikiwa kitandani na
mkononi nilikuwa nina pingu
“ooooh nimekwisha” nilijiongelesha
huku nikijaribu kujifungua asikari akaja
na kunionya. Hali ilizidi kuwa mbaya
ikabidi wapige simu ubalozi wa
Tanzania ikabidi kufanyiwa utaratibu
wa kurudishwa nchini chini ya ulinzi
mkali, nilifikishwa hospitali ya
muhimbili na kupewa matibabu nilipo
pona
nika somewa mashitaka na kupelekwa
katika gereza la ukonga jijini Dar es
salaamu.
Basai safari ya maisha ya gerezani
ndipo ilipoanza na kunifanye
nikutane na maswahiba ya ajabu yaliyo
badilisha kila kitu katika mfumo
maisha yangu.
***************
Ilikuwa imebaki siku moja ili
kufanikisha adhima yao ya kunitoa
kafara pale kijijini. Siku ambayo
nilitawaliwa na mawazo mengi
kichwani nililia bila kupumzika hata machozi hayakunitoaka tena.
Usiku uliingia tukawa tunasubiri
kukuche ile siku iliyopangwa
niondolewe dudiani, nikiwa katika
mawazo mazito mlango ulifunguliwa
aliingia Janeth “ Joseph njoo”
nikasimama na kumfwata, tulienda
porini umbari mrefu sana “lala hapo subiri baba eh” alinisubirisha akawa
anazunguka huku anazunguza maneno
kwa lugha nisiyo ijua.
Alimaliza kazi yake nakunisogelea
“Jose unahitajika kuwa na moyo wa
kiume kwa kazi inayokwenda kufanyika
sawa?” niliitikia kwa kutikisa kichwa
ingawa sikujuwa ni kazi gani “na
unachotakiwa nikukubaliana na kila kitu
kitakachotokea mbele yako,
umenielewa?” “ndio” “na huu ndio
utakuwa msaada
wangu wa wewe kutokuuwawa”
nilikubaliana na kila kitu ingawa
sikujuwa Janeth anania gani na mimi “simama” nikasimama na kusubiri kama alivyo niambia.
Janeth aligeuka nyuma na kuanza
kuongea tena maneno ambayo sikuweza
kuelewa hata neno moja, aliponigeukia
alikuwa ni mtu aliye badilika sana
mbaka nikataka kukimbia lakini
kwasababu alinambia niwe na moyo wa
kiume ilibidi nijikaze, alinisogelea “panua
mdo” aliniamuru basi nami nikafanya
alinishika mashavuni na kutoa moshi
mweusi mdomoni mwake na kuuingiza
midomoni kwangu kwa muda wa dakika
moja.
Alipo maliza liletendo mwili
uliishiwa nguvu basi nikaanguka chini
kwa mbali nilimsikia akinambia
“naomba usiniangushe Jose wangu
utaniuwa endapo hutofanya watakayokuagiza” nilijikuta nimetokezea pangoni ambako nilipokelewa na mtoto mdogo mwenye umri kama wamiaka sita hivi “nifwate” yule mtoto alinambia kwa kujiamini ikabidi nimfwate.
Katika lile pango kulikuwa na
mambo ya ajabu sana niliona mafuvu ya
watu kulikuwa na panya wakubwa
wakitembea tembea na milio ya ajabu
lakini nikawa najikaza namfwata yule mtoto huku nikiogopa sana tulifika sehemu kulikuwa na giza nene sana, yule mtoto alikuwa hana hofu hatakidogo alifika sehemu akainama na kuinuka “shika hii” alinikabidhi gogo na kuliwasha moto
ilikuupata mwanga.
Tulitembea kwa muda wa dakika
kama kumi katika lile giza, mbele
niliona kama ulikuwa mwisho hivi
“mlango funguka ni mimi Kashebo na
mgeni wangu” lango likafunguka nikaona madhari nzuuri inayovutia ilionekana kama waliishi watu mabilionea sana.
Tuliingia katika jengo lililojengwa
kwa dhahabu tupu kulikuwa na
mtu ameketi kwekiti kilichokuwa na
namna ya pekee na sijawahi kukiona
katika maisha yangu yote niliyozunguka
katika nchi mbalimbali duniani
“fanya nifanyavyo” mtoto Kashebo
kama alivyojitambulisha mlangoni
alinimbiaBkwa sauti ya utulivu, akapiga magoti nami pia nikafanya vile atakavyo kisha akaanza kusujudu nilifwata kila
alichokifanya bwana mdogo Kashebo
huku nikitetemeka.
Tulipo maliza tukainuka nilishangaa
kumwona yule jamaa pale kwenye
kiti amegeuka mzee na ameota pembe
mbili alisimama akicheka kwa kujidai
“karibu sana katika falme za dunia
kijana na leo nitakupa uwezo wa kinga
yako ya mwili kama nilivyoombwa na
endapo utakubaliana na sisi utaifaidi
sana dunia” alipomaliza kuongea
kunamaneno alinambia niyafwate vile
anavyo ongea maneno ambayo sikuyatambua mbaka na maliza.
Nilifanya kila watakalo huku
nikiyakumbuka yote aliyo nambia Janeth
endapo nikishindwa basi atauwawa,
yule mzee alinikabidhi bilauli lilokuwa
na kimiminika chekundu kama damu
“kunywa yote” nikawa naogopa kupokea
“naomba usiniangushe Joseph utaniuwa
endapo hutofanya wachokuagiza”
maneno ya Janeth yalijirudia kichwani mwangu na nilipokumbuka kuwa nimebakiza masaa machache kuuwawa nililipokeaBlile bakuli na kugugumia haraka niligundua nimenyweshwa damu tena damu ya binadamu, vicheko vilifwata vikionyesha kufurahia lile tendo
nilolifanya.
Sikujuwa kama ndio niliingizwa
katika uchawi “safi sana kijana sasa
nipe mkono wako wa kushoto” nikampa
nikijisemea liwalo na liwe, niliona
dada mmoja akija na sinia ambalo
lilikuwa na visu viwembe na vyuma
vyuma yule mzee alichukuwa kiwembe na kunichana mkononi, nilisikia maumivu makari nikawa na vuta mkono bila mafanikio alichukuwa kitu kama sindano na kuniweka pale nilipopasuliwa na kupafunika na kiganja chake alinena kwa
lugha nisiyo ijua alipotoa nilishangaa
kuona pamejifunga na kama
hapakupasuliwa.
Nilianza kupewa darasa jinsi ya
kutaka jambo litendeke na likafanyika
kwa kuongea pale katika ile sindano
mkononi niliruka hewani
nakufundishwa mambo makubwa kupitia ile sindano
mkonini mwangu, “unaweza kwenda
kijana na
unapo hitaji msaada usisite kutuita”.
Yule mzee alinishika paji la uso,
“nenda kijana” niilijikuta na
inuka pale chini nilipokuwa nimeanguka
wakati nipo Janeth, nilimwona Janeth
amepiga magoti huku amefumba macho
utafikiri alikuwa akisali, nilimshitua
katiak maombi yake kwa kujikoholesha
“khooooo khoooooo” aliinua kichwa na
kunitazama huku akitabasamu “ahsante
kwa kutoniangusha, sasa utakuwa kijana shujaa na hakuna atakaye kuuwa tena” “kweli Janeth?” “ndio” “jambo la
msingi fwata masharti tu na
usimwambie siri hii mtu mwingine”
tukaanza kucheza angani lakini nilihisi kama ndoto tu “sasa inabidi tuondoke muda umekwenda sana” “sawa” “sio sawa jibu ngraaaaaaaaaaa” ikabidi nijibu “ngraaaaaaaaaa” tukaondoka mbio mbaka kijijini yeye alienda ndani na mimi nikaenda kibandani.
Sikutaka kuwambia wenzangu
yaliotokea kwakuwa niliambiwa ni siri,
mawazo yalinichukuwa nikawa nawaza
endapo nimedanganywa alafu nikafa
“potelea pote” nilijisemea lakini sauti
ikanitoka wenzangu wakanisikia
“vipi mjukuu wangu” “hapana babu Ally
kuchanganyikiwa tu” “usijari kijana
sisi sote ni wakufa hakuna atakaye pona
naitamani sana nafasi yako ili
nijikomboe katika hiki kifungo” aliongea
kwa busara sana jamaa mmoja alieye
kuwa mle ndani “siogopi kufa hofu
yangu ni mamaangu na dadaangu kule
nyumbani maana niliwacha na hali
mbaya sana, hata sielewi wanaishi
vipi?” “mwachie Mungu hujui anamakusudi gani na familia yako”.
Tuliongea mambo mengi sana mbaka
kunakucha hata hatukulala kabisa
usiku ule lakini ilipo fika mida kama ya
saa nne asubuhi usingizi mzito
ulinipitia kwasababu sikulala kabisa
usiku wakuamkia siku hiyo nikawa
nimelala sijielewi kabisa.
“heeeeeeeeeee” nilishitushwa na
kelele zilizokuwa zinapigwa nnje
na watu walikuwa wamejaa pale
kichanjani wakiwa wameshika sahani
na kikombe
mikononi, watu walioandaliwa kwa
kufanya unyama ile siku walikuwa
wamejazia
na walikuwa wanafuraha sana.
Nyimbo nyingi ziliimbwa za ajabu
ajabu kila mmoja alionyesha
ushirikiano wa hali ya juu. “kamleteni
huyo ngedele” mama Janeth aliongea
na watu wakashangilia sana utafikiri
walikuwa hawanipendi hata chembe.
ITAENDELEA KESHO SAA TATU ASUBUHI
Samahanini kwa kutokuwa na riwaya hii siku ya jana kutokana na sababu zilizo kuwa nje ya uwezo wetu ila hakijaharibika kitu.
Ahsate pia kwa wale wanao unga mkono kwa kununu riwaya hii pasipo kungoja kesho na wewe kama ni mhitaji nicheki hapa 0755665931 ahsanteni
Hakuna maoni