Hii ni albam mpya ya Lil Wayne na mpenzi wake kamuweka wazi icheki hapa

Rapa Lil Wayne amesema yupo tayari
kutoa album yake mpya ya “Free Weezy
Album” mwezi wa nne mwaka huu 2015.
Lil Wayne anasema album itatoka kama
solo projet yake mwenyewe ikiwa ni ya
pili baada ya Sorry 4 Tha Wait iliyotoka
January baada yakushindwa kutoa Tha
Carter 5.

Wayne ambaye ni Bosi wa kundi la
Young Money, amemuweka wazi mpenzi
wake mpya, Christina Milian, ambaye ni
mmoja wa wanachama wa kundi hilo
analoliongoza. Baada ya kuweka wazi
habari hiyo, Wayne kupitia mtandao wa
Twitter, aliandika, “ Samahani kwa
kusubiri muda mrefu kujua nini
kinaendelea, kwa sasa hakuna tena
maswali nikiwa na Christina, huyu ni
mpenzi wangu .”



Hakuna maoni