Kaa tayari kwa ujio mpya wa Nemo 2015

Mkali wa RnB Nemo ambaye alitamba pia kwa ngoma ya Afro Pop 'Number one' aliyomshirikisha Ommy Dimpoz amewataka fans wake kukaa mkao wakula kwa ujio wake mpya 2015.

Akizungumza na gami dee kupitia 99.3MHZ Ice fm kwenye kipindi cha Zero  Planet Nemo amesema "kwasasa nimerudi kwenye game nikiwa na managment mpya na tayati kuna project nimefanya combination sound na tunatarajia kushoot video nchini kenya hivi karibuni"
 
Alipoulizwa na dj Josee kuhusu ngoma ya hero ambayo alifanya na Msodoki Nemo alisema "hiyo ngoma haikua official ila ipo niliyo fanya pekeangu nayo pia ni moja kati ya ngoma tunazo kwenda kushut video Kenya"

"kwasasa nipo na managment mpya sipo tena chini ya mtu nipo huru tofauti na kipindi kile nimeajiriwa hivyo sasa ni kazi tu mwanzo mwisho" alisema

Hakuna maoni