Akiongea na waandishi wa Habari, meneja wa Bia ya Kilimanjaro,Pamela Kikuli amesema kuwa zoezi la wananchi kupendekeza majina ya wasanii watakaowania tuzo hizo litaanza march 30 hadi april 19.
Tuzo za mwaka huu zina jumla ya vipengele 34 huku kilele cha tuzo hizo kimepangwa kuwa june 13 mwaka huu.
Wananchi watapendekeza majina yao kwa kutumia njia za sms,tovuti na whatsapp.
Kwa upande wake meneja udhamini wa kampuni ya bia, TBL, George Kavishe alisema kwa miaka minne sasa kasoro zilizokuwa zinajitokeza ni zile zile za wasanii kujiondoa kwenye mchakato wa
tuzo hizo umepungua kwa kiasi kikubwa kwakuwa na maboresho mengi yamefanikiwa pamoja na kutolewa elimu kwa wasanii.
Labels: KILIMANJARO MUSIC AWARDS 2015 KILIMUSICTOUR
RELATED ARTICLES
PLEASE USICHAFUE MAZINGIRA LUGHA ZA MATUSI HAZIHITAJIKI.
Hakuna maoni