C9 Recordz yaja na mpango mzuri kwa wasanii mikoani

Ujio mpya wa C9 record kwa mwaka 2015 ni mpango mzuri kwa wasanii wa mikoani na wenye kipato cha chini hususani wasanii chipukizi.Akizungumza kwenye 180 Power ya Gami the doctor ndani ya 99.3MHZ Ice Fm Radio Makambako mmiliki na mtayarishaji wa Muziki wa bongo flavour C9 kanjenje amewataka wasanii kuingia mkito.com ili kudownload beat ambazo anazitengeneza kwaajili ya wasanii kufanyia kazi sehemu yeyote ile.

"hizi beat nimewalenga sana wasanii wa mikoani ambao wanakosa kufika dar hivyo wanaweza kurecord studio yeyote ile na hata kama beat watatumia watu watano poa ila mtu akihitaji beat iwe yake pekeake tuwasiliane nae" amesema C9

hata hivyo c9 amewataka fans wake kukaa mkao wa kula kwa 2015 ambao amesema anangoma nyingi alizofanya na mastar richa ya kuendelea kufanya kazi za chipukizi pia.
kuhusu producer anayemkubali bongo amemtaja Allan Mapigo

Hakuna maoni