KISWAHILI SARUFI O'LEVEL

KISWAHILI SARUFI OLEVEL
NAFSI UMOJA UWINGI
Ya Kwanza Ni- Tu-
Ya Pili U- M-
Ya Tatu A- Wa-
SARUFI
Sarufi nimfumo na kanuni za
lugha zinazomwezesha mtumiaji wa
lugha kuitumia lugha husika kwa
usahihi. Mfumo huo humwezesha
mzungumzaji kutunga sentensi zisizo na
kikomo ambazo hukubalika na wazawa
wa lugha wanaoifahamu lugha hiyo
barabara. Hivyo ni dhahiri kwamba
kila lugha ya mwanadamu huwa na
mpangilio na sheria zinazoilinda ili
kuifanya kuwa toshelevu na sanifu, na
uzingatiwaji wa kanuni na taratibu hizo
kwa mtumiaji humfanya na
kumtambulisha kama mmilisi wa lugha
hiyo.
Sheria za lugha zimegawanyika
katika makundi manne yanayojulikana
kamamatawi ya Sarufi ambayo ni pamoja
na; matamshi, maumbo, muundo na
maana.
1. SARUFI MATAMSHI
Sarufi matamshi ni tawi la sarufi
ambalo limejikita katika kuchunguza
sauti na matamshiyanayotumika katika
lugha Fulani na kulinda matumizi sahihi
ya matamshi hayo baina ya watumiaji
wa lugha hiyo. Lugha ya Kiswahili kama
zilivyokuwa lugha zote duniani ina
matamshi ya aina mbili; Irabu na
konsonanti.
A. Irabu
Irabu ni aina ya vitamkwa
ambavyo hutolewa pasi na kuwepo
kizuizichochote katika mkondo hewa
utokao mapafuni ukipitia katika chemba
ya kinywana chemba ya pua kwenda
nje. Lugha ya Kiswahili inazo Irabu tano
ambazo ni; /a/, /e/, /i/, /o/, na /u/.
B.     Konsonanti
Konsonanti ni aina ya sauti
ambazo hutamkwa kwa kuzuia mkondo
hewa kutoka mapafuni, ukipitia chemba
ya kinywa na chemba ya pua kwenda
nje. Katika lugha ya Kiswahili zipo jumla
ya konsonanti zifuatazo; /b/, /ch/, /d/, /
dh/, /f/, /g/, /gh/, /h/, /j/, /k/, /l/, /m/, /n/, /
ny/, /ng’/, /p/, /r/, /s/, /sh/, /t/, /th/, /v/, /
w/, /y/ na /z/.
2. SARUFI MAUMBO.
Hili ni tawi la sarufi ambalo
hujishughulisha na uchunguzi wa
maumbo mbalimbali ya maneno katika
lugha ya Kiswahili. Maumbo hayo ni;
silabi, mofimu na neno lenyewe.
A. Silabi
Silabi ni kipashio cha kifonolojia
kinachohusu matamshi ambacho kwacho
sauti za
Lugha hutamkwa mara moja kwa pamoja
kama fungu moja la sauti. Kuna aina
mbili za silabi, yaani silabi
fungenasilabi huru.
Silabi huru ni zile ambazo huishia na
irabu.
Kwa mfano; la, ma, kwa, mba,
n.k.
Ilhali silabi fungeni zile zinazoishia na
konsonanti ambapo katika lugha ya
Kiswahili ni nadra kuzipata maana
lugha hii inatumia silabi huru lakini
hupatikana katika maneno ya Kiswahili
yanayokopwa kutoka katika lugha
nyingine.
            Kwa mfano;   Alhamisi – a-l-ha-
mi-si
Taksi - ta- k -si
Miundo ya Silabi za Kiswahili
a. Muundo wa irabu peke yake (I) - Yapo
maneno katika lugha ya Kiswahili
yanayoundwa na irabu peke yake kama
silabi. Mfano; u+a = Ua, o+a = Oa, a+u =
Au, n.k.
b. Muundo wakonsonanti pekee (K) –
Kiswahili hakina maneno mengi
yanayoundwa na silabi pekee isipokuwa
maneno machache ambayo huwa ni ya
nazali /M/ na /N/ na huwa zinatumika
ama mwanzoni au katikati ya neno.
Mfano; m+ke = Mke, m+bwa = Mbwa, n
+chi = N chi n.k
c. Muundo wa konsonanti na irabu (KI) –
Katika muundo huu konsonanti
hutangulia irabu. Mfano; b+a = Ba, k+a
= Ka n.k.
d. Muundo wa konsonanti mbili na irabu
(KKI) – Katika muundo huukonsonanti
mbili hutangulia irabu. Mara nyingi
konsonanti ya pili huwa ni kiyeyusho.
Mfano; k+w+a = Kwa, m+w+a = Mwa, b
+w+a = bwa, n+d+e = Nde, n.k.
e. Muundo wa konsonanti tatu na irabu
(KKKI) – Muundo wa namna hii
hujitokeza katika maneno machache.
Mfano; Bambwa, Tingw a, Ti ndwa, Mbwa,
n.k.
f. Muundo wa silabi funge – Huu
hujitokeza katika maneno machache
ambayo huwa ya mkopo. Mfano; Il -ha-li
= Ilhali, Lab-da = Labda
B.     Mofimu
Mofimu ni kipashio kidogo kabisa cha
lugha ambacho kina uwezo wa kusitiri
maana ya neno ambalo kwalo
limeundwa. AU ni kipashio kidogo
kabisa cha lugha chenye maana kisarufi.
AINA ZA MOFIMU
Mofimu huru ni aina ya mofimu
ambayo huweza kusimama pekee na
kujitosheleza kimaana yaani huwa na
sifa ya neno. Mfano; mama, Baba, Dada,
Kaka, Mjomba, Shangazi n.k. Kwa
kuangalia utagundua kuwa mofimu huru
haziwezi kugawanyika zaidi na kubeba
maana kisarufi, kwa maana kwamba
mofimu ‘baba’ ikigawanywa ba-ba, ‘ba’
hii haina maana yoyote kisarufi zaidi ya
kuwa silabi.
Mofimu tegemezi ni aina ya
mofimu ambayo huweza
kuvunjwavunjwa na kubeba maana
kisarufi, mofimu tegemezi hutegemeana
ili kuleta maana kamili ya neno.
Mfano; neno ‘anakula’ limeundwa
na mofimu zifuatazo:- [a-na-kul-a]
ambazo kila moja hubeba dhana Fulani
ya kisarufi.
VIAMBISHI
            Ni mofimu zinazopachikwa
nyuma au mbele ya mzizi wa neno ili
kubadilisha dhana ya neno. Kwa kuwa
mofimu hizo hupachikwa sehemu mbili
tofauti, tunapata aina mbili za viambishi
kwa mujibu wa nafasi zake katika
nenoyaani; viambishi awaliambavyo
hupachikwa mwanzoni au nyuma ya
mzizi wa neno,viambishi kati ambavyo
hupachikwa katikati ya neno (Kiswahili
hakina viambishi hivi) na viambishi
tamati ambavyo hivi hupachikwa mbele
au mwishoni mwa mzizi wa neno.
Mfano:-
VIAMBISHI AWALI MZIZI WA NENO VIAMBISHI TAMATI NENO JIPYA
A na chez ew a Anachezewa
Wa li chez ean a Walichezeana
Tu ta chez e a Tutachezea
1. Viambishi awali Hivi hupachikwa kabla
ya mzizi wa neno na huwa ni vya aina
tisa:-
i.                    Viambisha awali vya nafsi- hivi
hudokeza upatanishi wa  nafsi katika
kitenzi, zipo nafsi tatu, nafsi ya kwanza,
ya pili, nay a tatu.
M
Mfano:-Ni nalima
Tu nacheza
ii. Viambishi awali vya ngeli- hivi
hupatikana mwanzoni mwa nomino au
vivumishi ili kudokeza hali ya umoja na
uwingi.
Mfano:-M tu (umoja) – Wa tu (uwingi)
M safi (umoja) – Wa safi (uwingi)
iii. Viambishi awali vya ukanushi - hivi
hudokeza hali ya uhasi wa tendo.
Huwakilishwa na mofimu (ha-) na (si-)
Mfano:- Amekula (uyakinifu) –
Ha jala (ukanushi), Nakula (uyakinifu) –
Si li (ukanushi)
iv. Viambishi awali vya Njeo- hivi
hudokeza nyakati mbalimbali ambazo ni
wakati uliopita, uliopo na ujao.
NYAKATI MOFIMU
Uliopo -Na-
Uliopita -li-
Ujao -Ta-
Mfano:- Mli tuona
Uta kuja
v. Viambishi awali vya hali- hivi
hudokeza hali mbili za nyakati ambazo
ni mazoea ambayo huwakilishwa na
mofimu {hu} na timilifu
inayowakilishwa na mofimu {me}.
Mfano:-Hu cheza
Amelima
vi. Viambishi awali vya masharti-hivi
hudokeza hali ya masharti au
uwezekano katika tendo. Mofimu hizo ni
kama –ki-, nge-, ngali- n.k.
Mfano:- uki ja
Unge kuja
Angali mkuta
vii.              Kiambishi cha urejeshi wa mtenda
(kiima)- mhiki hudokeza urejeshi wa
nomino inayotenda katika kitenzi.
Mfano: - Aliye kuja {-ye-} hudokeza
urejeshi wa mtenda.
viii. Kiambishi kiwakilishi cha mtendwa
au mtendewa (shamirisho) – hivi
huwakilisha mtendwa au mtendewa wa
jambo.
Mfano; Nilimpiga, Uli u kata, Nime i penda,
Wame niteta.
ix. Kiambishi awali cha kujirejea
(kujitendea) – hiki huwakilishwa na
mofimu (-ji-)
Mfano; kuji penda
2. Viambishi tamati – Hivi hudokeza kauli
mbalimbali za vitenzi.
Mfano: - Anacheza – kutenda
Unachezw a- Kutendwa
Utachezew a- Kutendewa
Nimemli a- Kutendea
Wamewasomesh a- Kutendesha
n.k
Mzizi Kiambishi
cha Kauli
Kiambishi
tamati
maana
Neno
jipya
Kauli Viambishi
vya kauli
Chez a Cheza Kutenda -a
e a Chezea kutendea -e-
Pig ian a Pigiana Kutendeana -ian-/-ean-
iw a Pigiwa Kutendewa -iw-/ew-
Som esh a Somesha Kutendesha -ish-/esh-
eshw a Someshwa Kutendeshwa -ishw-/
eshw-
Lim ik a Limika Kutendeka -ik-/-ek-
an a Limana Kutendana -an-
w a Limwa Kutendwa -w-
DHANA YA MZIZI NA SHINA LA KITENZI
Mzizi wakitenzini sehemu ya neno
inayobakia mara baada ya kuondoa
viambishi vyote vya awali na tamati
katika neno hilo. Mfano: - a-na-chez-a {-
chez-}, m-ku-lim-a {-lim-}
Mzizi fungeni ule ambao hauwezi
kujikamilisha kimaana yaani hauwezi
kusimama kama neno. Mfano; -lim-, -
chez-, -imb- n.k.
Mzizi huru ni ule ambao huweza
kusimama kama neno na
ukichanganuliwa zaidi hupoteza maana
yake ya msingi. Mfano; Kinu, Kazi,
Arifu, Sali n.k.
Shina la kitenzi ni sehemu ya neno
ambayo huongezwa viambishi fuatishi
(tamati) au nisehemu ya neno ambayo
hubakia baada ya kuondolewa viambishi
tangulizi. Mfano:- chez+a = cheza, lim+a
= lima. Sehemu hii ya neno hutumika
kuundia neno jipya.
Shina sahili – hili ni shina ambalo
huundwa na mofimu moja tu ambayo ni
mzizi wa neno hilo, huwa ni mofimu
huru, Mfano; Kesho, jana, kitabu, jarida
n.k.
Shina changamano – shina hili huundwa
na mzizi na kiambishi tamati maana.
Mfano; cheka, lala, lia, kula n.k
Shina ambatani – shina hili huundwa na
mofimu mbili ambazo ni huru. Mfano;
mwana + kwenda = mwanakwenda ,
mbwa + mwitu = mbwamwitu
UAMBISHAJI NA MNYUMBULIKO
WA MANENO
Uambishaji
Uambishaji ni ule utaratibu wa
kuongeza viambishi katika mzizi wa
neno , ili kulipa neno maana ya ziada.
AU ni hali ya kubadilishabadilisha
mofimu katika mzizi wa neno ili
kuonesha upatanisho wa kisarufi katika
tungo hiyo.
Kiambishi:
Kiambishi ni sehemu (mofu)
ambayo huambikwa kwenye mzizi wa
neno ili kulipa neno hilo maana ya
ziada. Tunapopachika viambishi hivyo
mwanzoni mwa mzizi wa neno hali hiyo
huitwa ‘uambishaji ’. Uambishaji upo wa
aina mbili; Unyambuaji au unyambulishi:
Huu ni aina ya uambishaji
unaosababisha neno kubadilika kutoka
kategoria moja hadi nyingine .
NaMnyambuliko: Ni aina ya uambishaji
ambao huhusisha kurefusha nenona
kuliweka katika hali tofauti za katagoria
ileile.
Uambishaji wa kategoria mbalimbali za
maneno.
Uambishaji wa vitenzi – Uambishaji wa
vitenzi hujitokeza kwa kutegemea dhima
tofauti tofauti za mofimu kama vile:-
i. Viambishi vya nafsi
ii. Viambishi vya njeo
iii. Viambishi vya ukanushi
iv. Viambishi vya urejeshi
v.            Viambishi vya hali
vi. Na viambishi vya kujitendea
Mfano; mzizi –lim- unaweza kupachikwa
viambishi hivyo na kuweza kubadilika
kidhana kama ifuatavyo:-
A-na-lim-a
Hu-lim-a
U-me-lim-a
Ni-na-vyo-lim-a n.k.
Uambishaji wa majina– Uambishaji wa
majina huwa unazingatia upatanisho wa
kisarufi kimofolojia ambao hujikita
katika kuangalia alomofu tofauti
zinazowakilisha ngeli moja katika umoja
na uwingi wa majina hayo.  Kwa
mfano:-
UMOJA WINGI ALOMOFU
m-tu Wa-tu M/WA
m-ti mi-ti M/MI
Ki-ti vi-ti KI/VI
u-gonjwa Ma-gonjwa U/MA
Ø-fisadi Ma-fisadi Ø/MA
Ø-kaka Ø-kaka Ø/ Ø
Uambishaji wa vielezi – Vielezi katika
lugha ya Kiswahili havitokani na
kategoria nyingine ya maneno, bali ni
maneno ya kawaida yanayopatikana
katika lugha na si rahisi kupachika
mofimu yoyote katika maneno hayo
isipokuwa vielezi vichache ambavyo
hupatikana kwa kupachikwa kiambishi
awali cha namna {ki-} katika kivumishi
au nomino mfano: ki-jinga, ki-janja, ki-
toto, ki-raia, ki-puuzi n.k.
UNYAMBULISHAJI
Ni hali ya kupachika viambishi tamati
katika mzizi wa neno. Mofimu hizo
huitwa mofimu fuatishi.
Unyambulishaji wa kategoria mbalimbali za
maneno ya Kiswahili.
i. Viwakilishi . Mfano; Mimi = mi ye,
Sisi = si ye, Ambalo, Ambacho, Ambao,
Ambaye n.k .
ii. Majina. Mfano: Nyumba+ni =
Nyumbani, Shamba+ni = Shambani, n.k.
iii. Vivumishi. Mfano: Safi = Safi sha,
Refu = Refu sha n.k.
iv. Vitenzi. Mfano: Lima-limika-
limishwa-limwa-limiana-limiwa n.k.
Ukitazama kwa makini utangundua
kwamba unyambulishaji mara nyingi
hubadilisha neno kutoka katika
kategoria moja na kuipeleka katika
kategoria nyingine.
DHIMA ZA UNYAMBULISHAJI
i. Kuongeza msamiati wa lugha ya
Kiswahili.
ii. Kuzalisha kauli mbalimbali za
vitenzi vya Kiswahili
iii. Hupanua maana ya neno.
TABIA ZA VITENZI VYA KISWAHILI
V itenzi vya Kiswahili huwa na
tabia tofauti tofauti zinazotokana na
dhima za mofimu ambazo hupachikwa
katika vitenzi hivyo, hivyo kulingana na
dhima za mofimu, vitenzi vya Kiswahili
huwa na tabia zifuatazo:-
I. Kutambulisha nafsi. Mfano:-
A nayesoma
II.            Kutambulisha tendo. Mfano:- Cheza,
Lima, Imba n.k.
III. Kutambulisha wakati. Mfano:-
Ulikuja
IV. Kutambulisha hali ya uyakinishi na
ukanushi. Mfano:- A nacheka – Ha cheki
V. Kutambulisha kauli mbalimbali za
tendo. Mfano:- cheza-chezwa-chezewa-
chezeka n.k.
VI. Kutambulisha hali ya tendo. Mfano:-
Hu imba, Amekula.
VII. Kuonesha urejeshi wa mtenda,
mtendwa na mtendewa ambao
hujidhihirisha katika ngeli ya nomino
iliyotajwa kwa kuzingatia upatanisho wa
kisarufi. Urejeshi huo ni wa O-rejeshi.
Katika urejeshi huo vitenzi hubeba
viambishi ngeli vya –O- isipokuwa kama
nomino ni ya ngeli ya kwanza umoja
ambapo hutumia –e- badala ya –O-.
Mfano:-
NGELI KIAMBISHI CHA
O- REJESHI
MFANO
A-WA -YE- na –O- Ali yepiga / Wali o kuja
U-I -O- na –YO- Uli o katwa / Iliyo katwa
LI-YA -LO- na –YO- Lili lochanika /
Yali yo chanika
KI-VI -CHO- na –VYO- Kili chovunjika /
Vilivyovunjika
I-ZI -YO- na –ZO- Iliyo fungwa /
Zili zo fungwa
U-ZI -O- na -ZO Uli o katika / Zili zo katika
U-YA -O- na –ZO- Uli o nipata / Yali yo nipata
KU -KO- Kuli ko tokea
PA-MU-KU PO-MO-KO Pale alipo ingia / Mule
ali mo tokea / Kule
ali kofunga
ZOEZI
1. Fafanua dhana ya sarufi kisha eleza
tanzu zinazoijenga.
2. Eleza umuhimu wa kujifunza sarufi ya
Kiswahili.
3. Onesha tofauti iliyopo kati ya irabu na
konsonanti.
4. Eleza maana ya silabi na uoneshe kwa
mifano miundo mitano ya Silabi za
Kiswahili.
5. Nini maana ya mofimu? Fafanua aina
zake.
6. Bainisha dhima za kila mofimu katika
maneno yafuatayo:-
a. Anakula
b. Waliokutafuta
c.       Tulipokukosa
d. Nikikukumbuka
e. Aliyempigia
f. Hakufika
g. Huimba
h. Mnavyopendana
i. Amemtukana
j. Ungelifika
7. Nini maana ya uambishaji na
mnyumbulkiko wa maneno? Onesha jinsi
dhana hizo zinavyochangia kukuza
lugha.
8. Eleza kauli mbalimbali za vitenzi vya
lugha ya Kiswahili.
9. Pachika viambishi ngeli vya O- rejeshi
katika vitenzi vifuatavyo ukibainisha
umoja na uwingi:-
a. Chura amekufa
b. Kitabu kimechanika
c.       Meza imevunjika
d. Daftari limechanika
e. Simu imeita
f. Ameingia mahali humu
g. Amepitia pale
h. Imevunjiwa kule
10.
C. Neno
Ni silabi au mkusanyiko wa silabi
zinazotamkwa au kuandikwa ambazo
huwa na maana (maana yaweza kuwa ni
ya kileksika au kisarufi).
AINA ZA MANENO
1. NOMINO
Ni aina ya neno ambalo hutaja mtu,
kitu, mahali, hali na kitendo. Mfano;
Mwajuma, Kalamu, Mwanza, Udakitari,
Kulima n.k.
Aina za nomino :
· Nomino za pekee: Nomino za pekee
hutaja na kutambulisha nomino mahsusi
na za kipekee. Yaani kuwa kitu ni hicho
na wala si chengine chochote. Hizi ni
nomino zinazohusisha majina kama vile
ya watu, nchi, miji, mito, milima,maziwa
na bahari. Herufi za kwanza za nomono
za pekee huwa kubwa hata kamanomino
hizi zinapatikana katikati ya sentensi.
Mfano; baba, Asha, Tanzania, Dodoma,
Kilimanjaro, Victoria n.k
· Nomino za jamii : Hizi kwa jina jengine
huitwa nomino za jumla. Nomino
hizihazibainishi wazi wazi vitu ambavyo
habari zake zinatolewa. Kwa mfano
ikiwa nimtu, mahsusi hatambuliwi.
Haituambii kama ni Kelvin, Tuafu ama
Zawadi.Ikiwani ziwa halitambuliwi
kama ni Michigan , Victoria au Nyasa,
yaani hutaja vitubila kutaja umahsusi
wake kama ilivyo katika nomino za
pekee. Hizizinapoandikwa si lazima
zianze kwa herufi kubwa isipokuwa
zimetumiwamwanzoni mwa sentensi au
zimetumika kama anuani ya kutajia kitu
kama vileMkuu wa Sheria. Katika mfano
huu ‘sheria’ kwa kawaida ni nomino ya
kawaida,lakini hapa inaanza kwa herufi
kubwa kwani inataja anuwani ya
kipekee. Mfano wa nomino za kawaida
ni; Mwanafunzi, Mwalimu, Mnyama,
Mtazamaji, Askari n.k
· Nomino za kawaida: Kundi hili la
nomino hutumia kigezo cha uwezekano
wakuhesabika kuziainisha. Hapa
tunatofautisha kati ya nomino
zinazowakilisha vitu vinavyohesabika
kwa upande mmoja, na vile
visivyohesabika kwa upande mwengine.
Nomino ya vitu vinavyohesabika
vitanda, nyumba, vikombe vitabu
kadahlika. Zile zisizohesabika hurejelea
vitu ambavyo hutokea kwa wingi na
haviwezi kugawika, kwa mfano maji,
mate, makamasi, maziwa, moshi,
mafuta. Aghlabu nomino hizo huwa
sawa katika umoja na wingi.
· Nomino za kitenzi jina : Hizi ni nomino
zinazohusu vitenzi . Huundwa kwa
kuongezwa kiambishi {ku-} cha
unominishaji kwenye mzizi wa kitenzi
cha kitendo halisi ili kukifanya kiwe
nomino. Mfano; Kulima, Kucheza,
Kuimba n.k
· Nomino dhahania: Hizi ni nomino
ambazo hurejelea vitu vinavyoweza
kuhusika na mwanaadamu kupitia
milango ya hisia kama macho, mapua,
masikio vidole na ulimi- yaani vitu
ambavyo haviwezi kushikika,
kuonekana, na kuonjeka. Mfano; Vita,
Njaa, Ugonjwa, Shetani, Mungu n.k
2. VIVUMISHI
· Ni maneno ambayohutoa ufafanuzi au
maelezo ya ziada kuhusu jina ili
kuitambulisha vyema.
Aina za vivumishi.
· Vivumishi vya sifa : hutoa sifa za
nomino /kiwakilishi cha nomino. Sifa
hizi huweza kuwa nzuri, mbaya au
yoyote ile. Mfano; mzuri, mbaya,
mrembo n.k
· Vivumishi vya idadi : vinaweza
kujitokeza katika aina tatu
ndogondogo.Vivumishivya aina hii hutoa
taarifa kuhusu idadi ya nomino ambazo
kiwango chakekimetajwa. Mfano;
wawili, watano, wengi, wachache n.k
· Vivumishi vya kumiliki : Ni vivumishi
vinavyoonesha kuwa kitu fulani kina
milikiwa na mtu au kitu chengine.
Mfano ; yangu, yake, yako, kwetu n.k
· Vivumishi Vioneshi: Vivumishi vya aina
hii huonyesha mahali au upande kitu
kilipo. Vivumishi vya aina hiihujengwa
na mzizi {h} kwa vitu vilivyopo karibu
na mzizi {le} kwa vitu vilivyo mbali.
Mfano; hapa, pale n.k
· Vivumishi vya kuuliza: Hivi ni
vivumishi ambavyo hufafanua nomino
kwa kuuliza habari zake. Hujibu
swali“gani?ipi? ngapi?”
· Vivumishi vya pekee: Vivumishi hivi
huitwa vya pekee kwa sababu kila
kimojawapo huwa na maana
maalumu.Pia kila kimojawapo huchukua
upatanisho wake wa kisarufi kulingana
na ngeli yanomino ambayo
kinaivumisha. Mizizi vivumishi hivi
ni ote, o-ote, enye, -enyewe, -ingine, -
ingineo. –ote. Huonyesha ujumla wa kitu
au vitu-o-ote Kivumishi cha aina hii kina
maana ya “kila”, “bila kubagua” –
enyeKivumishi cha aina hii hutumika
kuleta dhanna ya umilikishaji nomino
Fulani. – enyewe Kivumishi cha aina hii
hutumika kuisisitiza nomino fulani. –
ingineKivumishi cha aina hii huonyesha/
huonesha ‘tofauti na’ au ‘zaidi ya’ kitu
Fulani. – ingineo Kivumishi cha aina hii
hutumika kuonesha/kuonyesha ziadi.
· Vivumishi vya A- unganifu: Vivumishi
vya aina hii huundwa kwa mzizi wa
kihusishi a- unganifu. Kihusishi
hikihuandamana na nomino kuunda
kirai husishi ambacho huvumisha
nomino iliyotajwaawali. Vivumishi vya
aina hii hutumika kuleta dhanna
zifuatazo:- -Umilikaji-Nafasi katika orodha.
Mfano; wa kwangu, wa Juma, ya tano ya
Sita n.k
4. VIELEZI
Maana ya vielezi: Vielezi ni maneno
yanayofafanua vitenzi, vivumishi
auvielezi vyengine. Huweza kuarifu
kitendo kilichotendeka kilitendeka wapi ,
namnagani na hata mara ngapi?
Aina za vielezi
· Vielezi vya namna au jinsi . Vielezi vya
namna hii huonyesha jinsi au namna
kitendo kilivyotendeka. Vielezi
vyanamna vipo vya aina kadhaa.
- Vielezi vya namna halisi.
Hivi ni vielezi vinavyotumia maneno
ambayo kimsingi yana sura ya vielezi
moja kwa
moja katika uainishaji wa aina za
maneno. Mfano; kuimba sana
-Vielezi vya namna mfanano
Hivi ni vieleziambavyo hutumika
kufananisha vitendo na vivumishi au
nomino
mbalimbali. Hujengwa kwa kuongeza
kiambishi (ki-) au kiambishi (vi-).
Viambishi hivi
hujulikana kwa jina la viambishi vya
mfanano.Ulifanya vizuri kumsaidia
mwanangu.
-Vielezi vya namna vikariri
Hivi nivieleziambavyo hufafanua vitenzi
kwa kurudiarudia neno moja mara
mbili.Mfano; polepole, harakaharaka.
- Vielezi vya namna hali
Hivi nivieleziambavyo hufafanua juu ya
kitendo kilichotendeka kimetendeka
katika
hali gani. Mfano; kivivu, kibabe,
kizembe, kipole n.k
- Vielezi vya namna ala/kitumizi
Hivi ni vielezi vinavyotaja vitu ambavyo
hutumika kutendea kitendo. Mfano; kwa
kisu, kwa kalamu n.k
- Vielezi vya namna viigizi.
Hivi vinaelezea zaidi jinsi tendo
lilivyofanyika kwa kuigiza au kufuatisha
sauti
inayojitokeza wakati tendo
linapofanyika au kutokea. Mfano;
alimpiga paaaah!
· Vielezi vya idadi. Vielezi vya namna hii
huonyesha kuwa kitendo kilitendeka
mara fulani au kwa kiasifulani. Mfano;
amempiga mara mbili
· Vielezi vya mahali.. Vielezi vya namna
hii huonyesha mahali ambapo kitendo
kinatokea.Huweza kudokezwakwa
viambishi au kwa maneno kamili.
Mfano; amekaa jikoni
· Vielezi vya wakati : Vielezi vya namna
hii huonyesha wakati wa kutendeka kwa
kitendo.Huweza kutokeakama maneno
kamili au hodokezwa kwa kiambishi
{po.} Mfano; alimkaribisha alipo kuja.
5. VITENZI
Kitenzi ni neno linaloeleza jambo
lililotendwa au lililotendeka. Kitenzi
huarifu lililofanyika au lililofanywa na
kiumbe hai chochote kinachoweza
kutenda jambo. Kitenzi cha Kiswahili
huundwa na mzizi pamoja na viambishi
vyenye uamilifu wa aina tofauti.
AINA ZA VITENZI
· Vitenzi vikuu (T) : Vitenzi vikuu ni vile
ambavyo hubeba ujumbemuhimu wa
kiarifu cha sentensi. Mfano; Mtoto
amekuja.
· Vitenzi visaidizi: Hivi hutoa taarifa ya
kusaidia vitenzi vikuu. Hutoa taarifa
kama vile uwezekano , wakati, hali
n.k.Vitenzi visaidizi daima hutumika na
vitenzi vikuu, ndivyo vinavyobeba
viambishi vya wakati. Mfano; Alikua
anacheza, Huwa namfurahia.
§ Vitenzi visaidizi huweza kupachikwa
urejeshi wa nomino na kusaidia
kuifafanua nomino hiyo. Mfano; motto
ali ye kua anacheza. Virejeshi hivyo ni
kama; -ye-, -yo-, -o-, -lo-, -cho-, -wo- n.k
· Vitenzi vishirikishi: Hivi ni Vitenzi
ambavyo hufanya kazi ya kuunga
sehemu mbili za sentensi. Havichukui
viambishi vya nafsi, njeo ama
hali.Vitenzi vishirikishi ni vya aina
mbili, ambavyo nikitenzi kishirikishi
“ni” cha uyakinishi na kitenzi
shirikishi“si” cha ukanushi.
Kazi za kitenzi kishirikishi
-kushirikisha vipashio vingine katika
sentensi
-Kuonesha tabia fulani iliyopo au
isiyokuwepo ya mtu fulani au kitu
fulani.
-Kuonyesha cheo au kazi anayofanya
mtu.
-kuonyesha sifa za mtu.
- kuonyesha umoja wa vitu au watu
-kuonyesha mahali
-kuonyesha umilikishi wa kitu chochote.
6. KIWAKILISHI
Kiwakilishi ni aina ya neno linaloweza
kutumika badala ya jina .
AINA ZA VIWAKILISHI
Viwakilishi vya kuuliza/viwakilishi viulizi
ambavyo huashiriwa na mofu /
kiambishi {-pi} ambavyo katika tungo
hutanguliwa na kiambishi ngeli cha jina
husika. Mfano- Mtoto yupi
Wiwakilishi vya urejeshi ambavyo
vinajengwa na shina amba pamoja na
vipande vidogo vidogo –ye-, - o-, -cho-,
vyo, lo, po, mo, ko n.k ambavyo
vinachaguliwa kilingana na ngeli ya
majina yanayorejeshwa navyo.
Viwakilishi vya idadi: Viwakilishi hivi
hutuarifu kuhusu idadi ya nomino hiyo
huweza kuwa kamili (halisi) au ya jumla.
Mfano; Wengi wamekuja
Viwakilishi vya pekee:- Hivi ni aina ya
vivumishi vya pekee kuwakilisha
nomino. Hufuata sheria za upatanisho
za nomino zinazowakilishwa.
Viwakilishi vya A-unganifu :- Viwakilishi
hivi huundwa kwa kihisishi cha A-
unganifu kusimamia nominoiliyomilkiwa,
inayochukuwa nafasi fulani katika
orodha au nomino ya aina
fulani.Kihisishi a-unganifu huandamana
na nomino kuunda kirai husishi
ambacho husimamamahali pa nomino.
7. VIUNGANISHI
Ni maneno, kikundi cha maneno
au kiambishi chenye kuunganisha
maneno, kirai, kishazi au
sentensi.Dhima ya kiunganishi ni
kuunga vipashio viwili au zaidi vyenye
hadhi sawa kisarufi .
Aina za viunganishi:
· Viunganishi huru: hivi ni viunganishi
vinavyosimama pekee katika tungo,
katikati ya vipashio vinavyo ungwa.
Hujumuisha: -
-Viunganishi nyongeza/vya kuongeza.
Mfano; Tena,Na,Zaidi ya n.k.
- Viunganishi vya sababu/visababishi.
Mfano; Kwa kuwa,kwa sababukwa vile,
kutokana na, n.k.
- Viunganishi linganishi/vya kinyume.
Mfano; Ingawa, Japokuwa, Lakini n.k.
- Viunganishi vya wakati.
Mfano; kasha, baadaye, Halafu, Baada
ya n.k.
- Viunganishi vya masharti.
Mfano; Kama, Ikiwa, Iwapo n.k
- Viunganishi vihusishi
Mfano; Cha, La, Wa, Za n.k.
· Viunganishi tegemezi: Ni viambishi
ambavyo hutiwa katika kitenzi cha
kishazi tegemezi ili kukiunga na kitenzi
kikuu cha kishazi huru ambavyo kwa
pamoja huunda sentensi changamano au
shurtia. Mfano; -ye-, -po-, -ki-, -cho- na -
nge-.
8. VIHUSISHI
Ni maneno ambayo huonyesha
uhusiano uliopo baina ya neno moja na
jengine.Vihusishi aghlabu huonyesha
uhusiano kati ya nomino au kirai
nomino na maneno mengine.
Mambo mbalimbali yanayoweza
kuonyeshwa na vihusishi
- huonyesha uhusiano wa kiwakati
- huonyesha uhusiano wa mahali
- huonyesha uhusiano wa kulinganisha
- huonyesha uhusiano wa umilikaji
- huonyesha uhusiano wa sababu/kiini
Aina za vihusishi
-vihusishi vya wakatiMfano; kabla ya,
baada ya n.k
-vihusishi vya mahali Mfano; chini ya, juu
ya, ndani ya, mbele ya n.k.
- vihusishi vya ulinganishi/ vya
kulinganisha Mfano; kuliko, zaidi ya n.k.
-vihusishi vya sababu/ kusudi/nia Mfano;
kwa sababu ya, kwa ajili ya n.k.
-vihusishi vya ala (kifaa)- Mfano; kwa
- vihusishi vimilikishi Mfano; cha, za n.k.
-vihusishi vya namna/jinsi/hali Mfano;
moto wa kuotea mbali, macho ya
mviringo
Matumizi ya ziada ya kihusishi
“kwa”
-kihusishi hiki huonyesha mahali au
upande
-kihusishi hiki huonyesha sababu au
kisababishi cha jambo
-kihusishi hiki huonyesha wakati
-kihusishi hiki huonyesha sehemu Fulani
ya kitu kikubwa
-kihusishi hiki hutumika kuonyesha ‘nia
ya pamoja na’
-Kihusishi hiki huonyesha jinsi kitendo
kilivyotendeka
9. VIHISISHI /
VIINGIZI
Ni maneno ambayo hudokeza
hisia za moyoni mwa mzungumzaji
baada ya kuwa katika hali ya furaha,
huzuni, majonzi, maumivu, kushangaa,
majuto n.k. Mara tunapotumia viingizi
katika tungo huathiri tungo hiyo
kuifanya kuwa na mshangao, hivyo
tunaongeza alama ya mshangao mbele
ya tungo hiyo. Kwa kuzingatia hisia
tunaweza kuwa na aina ya viingizi
zifuatazo:-
· Viingizi vya huzuni – pole! Jamani!
Maskini! N.k
· Viingizi vya mshangao – waow!
Lahaula! Eboo! Haiii! Ati!
· Viingizi vya kuitika – abee! Lamaa!
Naam!
· Viingizi vya kutakia heri – Inshallah!
· Viingizi vya kiapo – Wallah! Haki ya
nani! Kweli kabisa!
ZOEZI
1. Tofautisha majina dhahania naya
kipekee.
2. Fafanua matumizi matano ya vitenzi
vishirikishi kwa mifano bayana.
3. Ainisha maneno katika sentensi
zifuatazo:-
a. Mtoto mzuri ameondoka.
b. Yusuph na Ndonje hawaelewani.
c.       Kwenye kikapu kuna mboga.
d. Loo! Huna aibu kumuita.
e. Atakayekuja awe amejiandaa kujibu
maswali.
f. Nimesoma kitabu lakini sijagundua
kinahusu nini.
g. Mkaribishe, aingie.
h. Nataka nikija nikute tayari.
i. Ustaarabu umenishinda.
j. Mwalimu alisema, tuonane kesho.
4. Tunga sentensi ukionmesha matumizi
matano ya kihusishi ‘kwa’.
5. Kwa kutumia mifano eleza tofauti ya
viunganishi na vihusishi.
6. Eleza kwa mifano bayana aina tatu za
vitenzi.
7. Onesha matumizi matano ya vielezi
katika sentensi.
8. Kivumishi ni nini? Onesha matumizi
matano ya vihusishi vya nomino.
9. Tunga sentensi sita kwa kila aina ya
kiunganishi.
10. Tumia viingizi vifuatavyo kutunga
sentensi sahihi:
a. Taibu
b. La hasha
c.       Salale
d. Mashallah
e. Ebo


Hakuna maoni