Makala Jinamizi lila wasanii (na gadi mlwilo)

Nimekua mdau wa Muziki kwa muda mrefu sana na nimekua nikiufuatilia hatua kwa hatua lakini kitu kimojo ambacho kimekua kikinichanganya ni pale ambapo wasanii wanakuja na kupotea uwa sielewi ni nini tatizo.

Inamaana nikweli wanakua hawana uwezo au kunakitu gani kimejificha nyuma ya pazia? na kama ni kitu je ni kitu gani hicho? kunabaadhi ya watu wanasema eti hutoka kwa kutumia pesa, swali ni je mbona kunawatu wanapesa zao lakini hawapenyi kwenye game? binafsi sielewi jinamizi gani linalowatafuna wasani wanaokuja na kupotea.

Kuna  jamaa anaitwa Pig black kwa kweli nimewahi kua shabiki wa huyu jamaa najua wengi tumemfaham kupitia 'nini mnataka' ngoma iliyofanywa na P Fank Majani Bongo record na kufanikiwa kupenya na kueleweka kwa watu na ni ngoma ambayo hadi sasa ukiisikiliza kuanzia beat na jinsi jamaa alivyotembea lazima utakubali kuwa alistahili kutoboa mwisho wa siku Pig alienda shule jambo lililofanya awe kimya kwa muda mrefu na ndipo alipokuja kufanya ngoma nyingine 'nisikilize' akiwa amemshirikisha Mr Blue lakini nisikilize ilianza kushika kwa kusua sua kutokana na style aliyorudi nayo ingawa baadaye ilieleweka na kufanya vizuri mpaka sasa ikawa ndio bye bye japo watu tulimuelewa na ilikua kazi nzuri pia.

Ukizungumzia Latifa, mapenzi kitu gani Inaamana naamini tutamkumbuka MB Dog sana katika RnB wengi waliamini hakuna tena kama mb dog ila jamaa akapotea wakaibuka wengine na gemu lina songa, yu wapi Spack mzee wa 'ombi langu' coz naye alihit vizuri na kupotea mpaka sasa

hapo ni zamani na tukiachilia mbali kile kizazi cha kina Chelea Man ingawa jamaa alitoa ngoma nyingi ila ikawa ni yale yale ya mshumaa, 20% ni moja kati ya wasanii walioitikisa nchi hususani kipindi kile anachukua tuzo za kili tano lakini leo imebaki stori kama za kina mr nice kuwa walikuepo kwenye game.

Utaongea nini juu ya mtoto wa kitanga Top C na ngoma yake ya Ulofa? yu wapi huyu jamaa? ni kwamba jinamizi lilimpitia au ndio wale wanaosemekana wabanaji walisimama kwenye vyeo vyao? sawa sio kesi ila ndio gemu ya bongo ilivyo.

Sielewi ni nini kimemkuta Mo music coz jamaa alifanya vizuri sana kwa ngoma moja tu 'basi nenda' jambo ambalo lilipelekea kufanya shoo nyingi kwa mwaka 2014 akiwa ni chipukizi ambaye alijizolea mashabiki lukuki hususani kwa watoto wa kike.

Mo amekuja kufanya ngoma nyingine ya pili lakini haikupokelewa vizuri kama ya mwanzo ishu iliyopelekea fans wake waanze kuhisi aliotea kijana hajakata tamma kaachia ngoma yatatu ila bado haijapokelewa kama basi nenda sielewi lile jinamizi lililofanya kazi kwa wasanii wengine kama kina Sajna wa Iveta, Z Antoni mzee wa kisiwa cha malavidavi, Rado wa usiulize, Marlow wa nimechoka kupiga honi ngoma iliyo imbwa mpaka na watoto wadogo, Daz Baba japo anajikongoja ila haonekani na wengine wengi ambao wamepotea kwenye game ya bongo.

Kila nikimsikiliza Baraka da Prince wa siachani nawe, Pamdaffa wa nimempata na chipukizi wengine wa kali basi hofu uwa inanishika na kuomba yasitokee kama yalio tokea kwa wengine na ikiwezekana ni vyema tukaangalia tatizo lipo wapi ili kushindana na hili jinamizi lila wasanii tena wenye uwezo mkubwa wa kuimba na kama ni kweli wabovu kwenye uandishi basi ni heri wakawepo watunzi na wakauza nyimbo zao kwa hawa wenyeuwezo wa kuimba.

Uwa naamini kuna watu wanaweza sana kuaandika ila kuimba ni sifuri naona nibora tukapanua wigo wa ajira hata kwa watunzi ili kupata wakali wengi watakao peperusha bendela ya Taifa nasi siku moja Tukajivunia kuwa na wasanii wengi wakali Tanzania na ntafurahi zaidi siku tuzo kubwa za kimataifa zikiletwa nyumbani na wasanii watano nakuendelea sio kila siku Diamond, Vee Money na AY.

Mbona Nigeria wameweza na wanazidi kufanya vizuri Afrika huku wakizidi kuchanja mbuga kutafuta soko la Dunia?.

Naamini kwa pamoja tunaweza tukiungana kupingana na jinamizi hili linalo tupotezea vipaji vyetu basi game ya bongo tutaipush mbali na kulitangaza Taifa letu.

Japo kuna wasanii wanafanya vizuri na kutengeneza pesa ingawa hatuelewi kama ni pesa maneno au pesa kweli naamini tunaweza kupata mapato mazuri kwa wasanii endapo tukiweza kuwekeza kwenye Muziki.

na gadi mlwilo ni follow instagram kwa gamideetz facebook gami dee tz na twitter gami gadi ila ukihitaji makala za sauti andika makala tuma  kwa namba 0755665931 ni kwa watumiaji wa whatsap

Hakuna maoni