Raisi mpya Nigeria ameahidi kuwatokomeza boko haram kwa muda mfupi


Rais mpya wa Nigeria, Muhammadu Buhari amesema kuwa anatarajia kupambana na kulishinda kundi la wananmgambo wa Boko Haram baada ya dhamira mpya kutoka jeshini
na msaada wa nchi jirani.

“Kwa ushirikiano na majirani zetu Cameroon, Chad, Niger na jumuia ya kimataifa na dhamira ambayo tutapata kutoka katika jeshi, Nafikiri itachukua muda mfupi zaidi kukabiliana nao.”Amesema Buhari.

Akihojiwa na BBCJenerali Buhari amesema tayari ameainisha msingi wa tatizo linalokabili nchi ya Nigeria na kuwataka raia wa nchi hiyo kuwa
wavumilivu.

“Tumebaini matatizo makubwa matatu. Ambayo ni kukosekana kwa usalama nchini, tatizo ambalo kila mmoja analifahamu na lingine ni ukosefu wa ajira, hii ina maana uharibifu wa
uchumi ikiwa ni kutokana na vitendo vya rushwa na rushwa yenyewe.

Matatizo haya matatu makuu, Wanigeria wote wanafahamu na tunaomba ushirikiano wa wananchi wa Nigeria, wasitarajie miujiza kutokea katika kuyapatia ufumbuzi matatizo haya katika kipindi cha miezi michache baada
ya kutwaa madaraka kwa sababu uharibifu umechukua miaka mingi takribani miaka kumi na sita ya utawala wa chama tawala.

Hakuna maoni