Mkali wa Hip Hop Bongo Nikki Mbishi ametujuza kujitoa rasmi kwenye mtandai maarufu ambao wasanii hutumia kwa kuuza nyimbo zao Mkito.com, na kudai kwamba hata kazi zake hazitapatikana tena katika mtandao wa Mkito.
Rapa huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram amewataka fans wake kutumia mtandao wa Mdungndo.com ili kuzipata kazi zake kirahisi zaidi
“Taarifa rasmi sipo tena kwenye site ya Mkito, wala kazi zangu hazitopatikana tena huko.
Unaweza kupata kazi zangu Mdundo na sehemu nyingine" Ameeandika Nikki
Nikki Mbishi juzi kati ameachia ngoma inaitwa Kwanini Mimi aliomshirikisha Becka Tittle
Kwa sababu gan mbona hajasema sababu @gamideetz
JibuFutaKwa sababu gan mbona hajasema sababu @gamideetz
JibuFuta