Q Boy ndio alieniunganisha na Diamond: Lizer Classic

Lizer Classic


Mtayarishaji wa muziki nchini kutoka WCB 'Lizer Classic' amefunguka jinsi alivyopata shavu katika studio za Wasafi Record zinazomilikiwa na mwanamuziki Diamond Platnumz.

Akizungumza na Gami Dee kutoka Ice Fm Lizer amesema kazi alizofanya na Lol Lo ndio zilifanya afahamike kwa Diamond

"Diamond baada ya kufanya nae kazi aliwatumia watu wake wa karibu wanaofahamiana na mimi, alimtumia Q Boy  kwasababu Q Boy nilikua nafahamiana nae na nilifanya nae kazi nyingi. Alimtumia Q Boy akamwambia yule producer yule ambae tulifanya nyimbo na Lol Lo na ambae anaekufanyiaga na wewe nyimbo mi nahitaji kufungua studio naona kama atanifaa unaweza kuwasiliana nae kama anaweza kutufanyia kazi kwahiyo Q boy aliwasiliana na mimi nikawambia kama nnamkataba ukiisha tunaweza kufanya kazi wakasema okey tunakusubiri wewe."

Lizer ameitaja vita za wenyewe kwa wenyewe burundi ndio sababu pia ya kumuwahisha kufika Wasafi Record"Kuna vita ilitokea burundi ikabidi nirudi nyumbani kwa kua nilikua nyumbani nikaona nisikilizie mchongo na wao ndio kumbe walikua kwenye mipango ya kunicheki ikabidi wanitumie nauli nikaja ndio kazi nikanza rasmi."

Na Gami Dee (Ice Fm)
Instagram: @gamideetz
Phone: 0715971027

              SIKILIZA HAPA 


Hakuna maoni