Mmoja kati ya waasisi wa muziki wa bongo flava nchini Boni Luv amefunguka jinsi walivyokua wanafanya kazi kipindi cha nyuma wakati muziki wa kizazi kipya unaanza nchini.
Akizungumza na mtangazaji wa Ice Fm, Gami Dee Boni Luv amelinganisha ufanyaji kazi wa sasa na zamani nakuona tofauti kubwa ni kipato
"Zamani Tulikuwa Tunarekodia Wasanii Nyimbo Bure Kabisa mambo ya Wasanii kutoa Pesa ili warekodiwe Yalianza Mwaka 1995 na Bei ya kurekodi Ilikuwa 5000 na Elfu Tano Yenyewe Bado Ilikuwa Shida Wasanii Kuipata."
Pia amezungumzia suala la radio presenters na dj kuwatoza pesa wasanii "zamani tulikua tunafanya kazi na presenter ndio walikua wanatafuta kazi kutoka kwetu sisi lakini kwa sasa lazima uandae bajeti."
Boni Luv amemtaja Omary Tambwe Lill Ommy kama mtangazaji ambae anakuja vizuri sana na anaejituma sana.
Na Gami Dee Ice Fm
Instagram @gamideetz
Phone: 0715971027
Hakuna maoni