BARUA KUTOKA JELLA FULL Na Gami Dee Gadi Mlwilo

BARUA KUTOKA JELA
Mtunzi: Gami Dee

Hello Gami Dee hope u mzima, Naandika barua hii nikiwa jela mwaka wa pili tarehe 13 october nitakamilisha mwaka wa tatu hapa nilipo. Naomba nisilitaje jina langu ila mimi ni miongoni mwa mashabiki wako ambao nilikua nakukubali sana ukiwa kwenye mic.

Nivumiliee kwa maelezo haya marefu ambayo nimeandika maana imenichukua siku tatu kukamilisha kuandika barua hii kutokana na ratiba zetu hapa gerezani.

Ombi langu kwako naomba uwafikishie wadau wako habari hii naamini kunakitu watajifunza na wataacha kuoa kwa kukurupuka maana nilimuua mke wangu kipenzi tena wa ndoa kwa ujinga wake ambao sijutii hata chembe kwa nililolifanya nawaza hatanikifa tuakutana nae huko kuzimu atanipa kesi nyingine tena.

Mimi ni mzaliwa wa Kijiji cha Lyadebwe Mkoani Njombe japo sijakaa sana huko kutokana na kazi ya babangu ya uwalimu tulikua wa kuhama hama sana japo Darasa la saba nilihitimu katika shule ya msingi Makambako sikufanikiwa kumaliza elimu ya sekondari kutokana na kukosa sapoti ya kusomeshwa maana baba alivyofariki maisha hayakua poa sana kwetu japo mafao yake yalitusaidia kumuuguzia mamaetu bila mafanikio.

Sio lengo langu mnijue saaaana ila lengo ni kuhusu ndoa yangu ambayo imenipelekea mimi mpaka wakati huu unasoma habari hii nipo jela natumikia kifungo cha maisha nilichohukumiwa baada ya kumuua mke wangu.

Sikuwahi kuwaza hata siku moja kama nitakuja kuitwa muuwaji, katili, jitu lenye roho mbaya kama wengi walivyonichukia nakuona sikustahili kuwepo duniani tena wengine wakahukumu ikibidi ninyongwe nife kabisa.

Ndugu zangu haimaanishi napenda kuishi huku niliko, kiukweli jela sio kuzuri hata kidogo nataman hata kunyongwa nife ili nisimkumbuke tena yule kahaba mnisamehe kwa kutumia jina hilo baya kwa marehem maana mwanamke yule alikua ni mfano wa shetani tena shetani mtoa roho katika maisha yangu.

Hebu nikae kwenye point nikupe kisa kizima cha ndoa yangu mpaka kufikia maamuzi magumu na mabaya ambayo najutia mpaka wakati huu kwanini nilioa...? Japo sijutii kuuwa.

Baada ya kuondokewa na wazazi wangu nilikua mnyonge sana nikawaza nioe ili nipate mama mwingine nitakae saidiana nae kwenye pilika pilika za kusaka tonge hivyo niliwaza nikaolee kijijini maana mademu wa mjini niliamini ni pasua vichwa na niliona kabisa hawatanifikisha kwenye lengo isitoshe bushi yule shetani alinambia anamimba yangu nikaona its a right time kuoa.

28-08-2010 ilikua jumamosi ndio ilikua siku ya ndoa yetu nakumbuka 26-08-2010 ilikua alhamisi ndio ilifanyika sendoff huko Kijijini kwao Mdandu karibu na Njombe au Igwachanya siku tu ya sendoff ya yule mwanamke ndio nilianza ona mapichapicha ambayo sikuelewa kwa kipindi kile.

Wakati nafunga ndoa na yule mwanamke mwenye roho ya kishetani alinambia anamimba yangu hivyo nikaona pia ni muda sahii wa mimi kuoa na kuanzisha familia yangu maana kwa baba tulizaliwa wawili tu mimi na mdogoangu ambaye alikua Jijini Dar es salaam akifanya kazi za ndani.

Ndoa ilifanikiwa na kufaana sana, kwahiyo zoezi lilipita na tukawa na maisha ya furaha siku za mwanzo kama kawaida ujuavyo ndoa changa kwa waliooa wanaelewa kama hujaoa unamchumba basi nisema mapenzi mapya yanavyokua na mapenzi motomoto yaani mahaba niue.

Kunasiku nilipigiwa simu na mtu aliejitambulisha ni mjombaake mke wangu na akasema anataka aje atutembelee Makambako bila hiyana nikamkaribisha na kwakua nilipanga chumba na sebule nikaona niombe chumba cha mwenyenyumba alichokua anakifanya kama stoo ili mjombaake afikie katika chumba hicho.

Basi bwana nilikua na kiakiba changu kidogo ikanibidi nimshirikishe wife akanambia kwanini tujitese mzuie asije, we unaona ndio kwanza tunaanza maisha, nikaona sio poa ngoja nipambanie mpaka nifanikishe lile zoezi.

Sikutaka kumkatalia wife kwa muda ule ikabidi ni sema sawa japo sikuimanisha ile sawa yangu na nikawa nawasiliana na uncle anauliza hali ya mke wangu namjibu fresh.

Siku ya kuja ikafika ikanibidi nijikamue kiume ikanilazimu kuvunja kibubu changu, nikanunua kakuku mjomba akifika apige kipunga na kuku aone kweli nimefika kwa mkwe kumbe usilolijua ni sawa na usiku wa giza, maneno ya wahenga.

Nilipofika nyumbani nikamwambia wife ninawageni wawili wanakuja ni washikaji wangu sana na wanapenda sana ubwabwa na kuku naomba utupikie wakifika wajisikie freshi, wife akanielewa na akaandaa diko flani shikamoo sana.

Majira ya saa 12 jioni mgeni alifika ikanibidi nimwambie wife naenda kuwachukua wageni wangu diko yaani chakula si kipo tayari....? Akanijibu tayari baba kipindi hicho wife anakaribia kujifungua .

Nilienda stendi kumpokea mjomba alikua na kifurushi kilikua na mchele pamoja na begi dogo nikakodi bajaji hadi home, wife hakuamin kwa surprise ile alishangilia kama Ronald kaifunga team ya Messi. Nilitamani ningekua namimi nina ndugu tunapendana vile maana sio kwa furaha ile ya mke wangu na mjombaake waliokua nayo.

Chaajabu tukiwa chumbani wife alikua anaonesha kama hajapendezwa na ugeni ule ila wakiwa wawili unaweza hisi ni mtu na rafikiake waliokuwa pamoja wakati mjomba alikua dingi flani wa makamo kabisa.

Kama ujuavyo ukitaka kumjua vizuri mwenza wako tabia zake na mambo yake uliza majirani huwa wanakua na mkanda full wa maisha yenu, huwezi amini kumbe mjomba ndio alikua msaidizi wangu katika kumpa furaha mke wangu.

Akili yangu haikutaka kabisa kumuani Mariam ambaye alikua mpangaji mwenzangu alivyonambia mjomba anamla wife, jinsi nilivyokua namuamini mbwa yule sikuwaza kama kweli anaweza nifanyia ukatili ule na uchafu mkubwa kwanza hata mri wake haukufanana kabisa na sisi hata sijui wanawake hujirahisi popote.

Mjomba alikua kama babaetu kabisa, kwahiyo hata sikua tayari kumuamini Mariam kama kweli wife anagawa uroda kwa mjombaake.

Mbaya zaidi nikikumbuka jinsi ambavyo nilijitesa kutafuta hela kisa ndugu yake wife, kumbe shetani mjomba yule mchana anamla fala mwenzie, na usiku boya mimi sipewi mzigo naambiwa nimechoka mtoto leo tumboni kanichosha sana. Nanyimwa show navuta blanketi nalala kirohi safi kumbe nakadiliwa boya.

Ilikatika siku 5 mjomba akaaga kurudi kwao Mdandu Njombe, kumbe hata sio wa mdandu ni jitu kutoka Mbeya tena kyela huko wanakolima mpunga nadhani ndio sababu Makambako aliingia jioni tena na peto la mchele mbwa yule mzee asie na haya.

Mshenzi wa tabia mjomba aliondoka nikabaki na wife, kama ujuavyo wapenzi wakiwa chumbani wawili wakiishiwa tu stori huanza kuwasema watu.

Nikajikuta naropoka "Mariam mpuuzi sana kanifuata eti ohhhh unajua mgeni wako kama ni mume mwenzio...?" wife akashituka na kuuliza umesemaje...? Nami bila hiyana nikarudia tena kama nilivyosema. Nilipangwa saundi flani kama mtoto mdogo na nikamuamini wife na kuona Mariam ni Mpashukuna mbea wa Dunia funga kazi kumbe nilikua gizani.

Kunasiku niliomba simu ya wife nijirushie picha zetu maana wife alikua anapenda sana kupiga selfie, nikaona sms imeingia "oya vipi mwanangu anaendeleaje...?" Namba imesevu Mjomba kwa ujinga wangu nikahisi huyo mwanangu labda ni mimi.

Ilifika siku ya kujifungua nikafurahi kuona nimepata mtoto wa kike nikampa jina la marehemu mamangu na ukimcheki mtoto kwa asilimia  kubwa alifanana sana na mamake na kila alie muona alinambia mzee inaonekana ulizidiwa siku ya kumsaka huyu mrembo kichanga, zilikua ni kauli zinanikera ila nilimezea kiume na kujichekesha tu huku nikijifariji akikua atafanana kama babake.

Simu za yule mshenzi mjomba mkulima ziliongezeka kwenye simu ya mke wangu hadi nikaona kero.

Siku moja wife amerudi nyumbani akiwa bafuni simu ilita jina limeseviwa Rose Twin nikajua labda ni rafiki yake sikupokea. Simu ikaita tena nikasema nipokee nimwambie yupo kuoga nilichosikia kwenye simu kikanipa wazimu.

Ile nimepokea niweke sikioni nasikia sauti ya kiume "huyo boya yupo nini, mbona hukupokea simu mpenzi wangu" mmh nilishikwa na butwaa nikakata simu wife nae alikua anatoka bafuni ikabidi simu nirudishe pale kwenye kiti.

Muda huo nilitamani nimmeze mzimamzima nikawaza kasichana kadogo kale kataishije hali hata miezi mitano hakajafunga. nikawa mpole huku natafakari nini nifanye.

Usiku tupo kitandani tumelala nilishituka nikaona wife kashika simu nikigeuka anailalia kuficha mwanga then anajifanya kalala, nikizuga nakoroma anaichukua simu anaendelea kuitumia, ikanibidi niulize "kwani unachati na nani...? Mbona unaficha simu yako ukiona nageuka....?" Akanambia "sikutaka mwanga ukupige machoni mume wangu nilikua insta nafuatilia umbea tu.

Basi vile tunaongea tukawa tumemshitua mtoto akaanza kulia ikabidi ampe ziwa dogo anyonye kwa bahati nzuri au mbaya wakabebwa na usingizi wote wakalala, muda huo mi nawaza huyu malaya anachati na nani au ndio anachati na Rose Twin.

Jamani kama unamoyo mdogo usithubutu kupekua simu ya mpenzi wako kama unajijua huwezi kuachana nae kwa wakati huo usipekue simu yake omba hata password abadilishe usiijue kabisa.

Nilikuta sms mpya tano ila inaonekana walikua wanachati kisha sms anafuta ila zile tano nilizoziona ndio zilinichanganya zaidi sms 2 zilikua za mjomba na alikua anamtaka mtoto wake yaani kichanga changu anadai ni chake na anasema tutaficha hadi lini kwanini tusimchane tu huyo boya ajue mi namtaka mwanangu, nilistuka nakuzisoma zile txt mara mbilimbili huku mapigo ya moyo yalikua speed na ghafla nilichemka na kushikwa na hasira sana.

Nikajikaza nisome sms 3 zilikua za Rose Twin naye anadai mtoto ni wake kama mjomba tu, nilihisi kizungu zungu kwa muda ule niliwaza nichukue mto nimfunike mtoto pale pale  akose pumzi, lakini nikawaza tu mtoto hana hatia na vita hii haimuhusu kabisa.

Usiku ule kwangu ulikua usiku wa kikatili sana, nilijitahidi kuvumilia lakini ilinishinda baadae ilinibidi nimuamshe ili anipe maelezo juu ya zile sms.

Ile kuona tu akaanza kulia anaomba samahani, wakati huo me nahitaji kujua mtoto ni wanani kati yetu sisi watu watatu, nilitamani aseme mtoto ni wangu nadhani ingesaidia kupunguza speed ya mapigo ya moyo na ingeshusha hasira niliokuwa nayo.

Kila nikihoji kuhusu mtoto wa nani sipati jibu, vile nikiwaza nikivyooa kwa shida, nilivyolea mimba kwa shida, nikajikuta hasira inakua kama inanikaba koo niliinuka na kofi moja zito la usoni akajibamiza kwenye mbao ya kitanda ya kicjwani "nambie huyu mtoto ni wanani kati yetu, hataki kusema analia tu anaomba msamaha na kudai ananipenda.

Kichapo kilitembea pale ndani, na vile sikuwahi kupiga mwanamke wala kupigana basi sikua na elewa wapi nipige nilikuja kusikia tu majirani wakihangaika kuvunja mlango waje wamsaidie yule mshenzi.

Nilitoka kwenda sebleni kuangalia mlango na kuongeza meza pale mlangoni, wakati ninavyorudi chumbani niliona kisu mezani hapo sifikirii kingine zaidi kujua mtoto ni wanani...? Niliokota kisu na kuingia chumbani.

Nimwingia chumbani nikamwambia we malaya nakuuwa leo nambie haraka mtoto ni wanani....? Ile alivyoona kisu ndio akaanza kunambia mtoto ni wa yule mjomba wa Mdandu yaani anaendelea kunidanganya wakati yule boya ni wakyela mbeya huko na kile kipindi anakuja home kumbe alikua anakuja kwa mke wake na mimi na nunua na kuku najipinda hali mbaya kumbe lile dingi linamega tu kisela nilipatwa na hasira ya kiwango cha mwisho kabisa.

Nilishikwa na hasira, huku nikibubujikwa na machozi mwili nao ulikua ukitetemeka wakati huo yule malaya ndio anajimwaga kunieleza upuuzi eti baba wa mtoto kasaidia sana familia yake kiasi kwamba hata nyumbani kwao wanamjua na wanalijua hilo na ndiomaana yeye aliona kurudisha fadhila kwa yule mbwa ni kumpa uroda wa penzi bahati mbaya ndioakashika mimba.

Yaani kumbe mpaka wakwe wanajua, huu ni ushenzi wa aina gani...? kwanini wameamua kunifanyia hivyo mimi..? yaani najiuliza hivyo huku nipo kama kichaa kabisa.

Bila kupepesa macho nilimzamisha visu vya kutosha  yule malaya kwenye kifua chake na mpaka majirani wanafanikiwa kuvunja mlango nilikua mwekundu nimeloa damu mwili mzima na yule mshenzi anatapatapa tu kitandani mtoto wakati huo analia kama alijua kinachoendelea na vile nasikia kilio cha mtoto nikawa natamani nako nikatie beto.

Majirani kuona vile walinipiga sana na kunihesabu mimi ni mnyama na mkatili wa hali ya juu nadhani hawakujua yalionikuta maana sijawahi gombana tangu kuzaliwa kwangu.

Hata sielewi nani aliita polisi nilikuta tu naambiwa nipo chini ya ulinzi hapo mwili hauhisi maumivu yoyote mwilini kutokana na kichapo nilichotembezewa na majirani.

Nilibebwa kwenye gari mpaka kituo cha polisi, kesi ikafunguliwa kipindi hicho natamani hata nitoroke ili nikathibitishe kama yule fala amekufa kweli maana alinipa hasira ambazo ni za kiwango cha mwisho.

Nilikaa selo nikiwa ni mtu wa kulia tu huku nikijiona me ni boya sana yaani nilimkumbuka hata yule mbea Mariam maana asie sikia la mkuu ndio lilikua limenipata kwa wakati huo.

Ilifika siku ya mahakama nilitamani nipate hukumu ya kunyongwa nife nisiwaone tena wanadam lakin ubaya kesi ilihairishwa na kusogezwa tarehe mbele nikarudishwa selo.

Nashukuru Mungu hukumu ilifika na nikahukumiwa kifungo cha maisha maana nilikua natukana sana hakimu na kuleta fujo jambo ambalo lilipelekea nionekane kichaa, nimechanganyikiwa kisa mapenzi.

Kuna mengi yalitokea nimeshindwa kuandika yote kutokana na muda mchache nilionao huku gerezani lani kwa machache haya naamini kunakitu umejifunza kupitia mimi.

Kuna wakati natamani Serikali itengeneze sheria kuhusu watu wanaocheza na hisia za watu unakuta mtu unamalengo nae kumbe yeye yupo tofauti na maamuzi yako.

Mbaya zaidi wanawake wengi sikuizi wanawaza kuolewa ili wapate picha za shela za kupost Instagram na hawawazi kabisa kuhusu ndoa.

NB naomba msinitafute kwa haya mmeyajua kuhusu mimi, nimeandika haya ili kuacha yangu ya moyoni kwa wale waliokua wananichukulia mimi mkatili kumbukeni nimeumbwa kwa udongo na moyo wa nyama hivyo naumia pia.

Na nitumie nafasi hii kuwaaga maana barua hii ni barua yangu ya mwisho kabisa, kama kunakukutana naamini tutaonana sehemu nyine mimi siwezi kuendelea kuishi kwenye huu ulimwengu

Zaidi bwana Gami Dee naomba ujitahidi ujumbe huu uwafikie watu wengi zaidi. Ahsanteni na Mungu awabariki.

FUNZO
Jitahidi sana kumshirikisha Mungu juu ya chaguo la mwinzi wako na Imeandikwa wanawake tuishi nao kwa akili, Mume ampende mkewe na mke amuheshimu mumewe pia wahenga walisema hasira hasara. Fikiri kabla ya kutenda na mbio za sakafuni........

Naitwa Gadi Mlwilo a.k.a Gami Dee ni Radio Personality pia ni muandishi wa riwaya hivyo BARUA KUTOKA JELA  hadithi hii sio kweli jamani ni kazi ya fasihi yaani yakutunga tu so niwashukuru pia kwa kuifuatilia na mwisho wa stori hii kunanyingine nyingi zinakuja ahsanteni sana.

Kuipata kwa sauti ipo youtube  GUSA HAPA 


Hakuna maoni