WASIFU (BIOGRAPHY) YA WITNESZ KIBONGE MWEPEC (Witnesz M Sigbjorn)

WASIFU WA WITNESZ KIBONGE MWEPEC (Witness M. Sigbjorn)

Jina Kamili: Witness M. Sigbjorn
Jina la Sanaa: Witnesz Kibonge Mwepec
Tarehe ya Kuzaliwa: Novemba 15
Falsafa ya Maisha: “Tumia baada ya kuwekeza”
Mahali alikozaliwa: Dar es Salaam, Tanzania


UTANGULIZI

Witness M. Sigbjorn, maarufu kama Witnesz Kibonge Mwepec, ni msanii mashuhuri wa hip hop kutoka Tanzania na mmoja kati ya wasanii wa kike waliovunja vikwazo katika muziki wa hip hop Afrika Mashariki. Alilelewa na baba wa kambo raia wa Canada, Stanley Meldrum, aliyemfundisha falsafa ya kujiamini na kufuata ndoto bila kuogopa.

Akitambuliwa kwa uchangamfu wa kipekee jukwaani na mbinu ya kufoka yenye nguvu, Kibonge Mwepec alivutiwa na mtindo wa Busta Rhymes. Safari yake ya muziki ilianza mwaka 1997 baada ya kufanya utafiti kuhusu athari za hip hop kwenye jamii ya Kinondoni. Kukosekana kwa wanawake kwenye tasnia ya hip hop kulimfanya ajitose bila woga, akiwa sauti mpya yenye msisimko.

Jina lake la kisanii "Kibonge Mwepec" lilizaliwa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza na kujimudu jukwaani licha ya mwonekano wake mkubwa wa mwili – ishara ya kuondoa vizingiti vya kimwili katika sanaa. Alitambulika kama “Jicho Pekee la Hip Hop” kwa sababu ya mtazamo wa kipekee, ujumbe mzito na ushawishi wake jukwaani.


MATUKIO MAKUU YA KAZI NA USHIRIKIANO

  • 2004: Mshindi wa mashindano ya Coca-Cola Pop Stars nchini Tanzania, akaanzisha kundi la Wakilisha na wasanii wenzake Sarah (Shaa) na marehemu Langa.
  • 2005: Alishirikiana na Zap Mama (Belgium/DRC) kwenye wimbo For the Blues uliolenga kupinga ukeketaji.
  • 2006: Alitumbuiza nchini Norway na wasanii wakubwa kama Mari Boine na Angélique Kidjo katika tamasha la CARE International.
  • 2006: Alifanya kazi na kundi la Norway Dark Side of the Force (DSF) na kurekodi albamu Khaya Khaya.
  • 2008: Albamu ya Khaya Khaya ilitolewa Norway na kuuzwa kwa mafanikio makubwa, kisha kuingia sokoni Ufaransa.
  • 2008: Aliachia wimbo ZERO akiwa na Fid Q – wimbo ulioteka hisia za watu kutokana na ujumbe wake wa kujitambua, nguvu ya wanawake na mafanikio katika tasnia ya wanaume.
  • 2009: Nyimbo mbili Attention Please na Umwe ziliwekwa kwenye mkusanyiko wa Norway Imagine Africa.
  • 2018: Wimbo Attention Please ulitumika kwenye filamu ya Kiswidi East of Sweden.

MAONESHO YA KIMATAIFA

  • Afrika Kusini: 2004 (The Club House, Club Berogue, TSV Filming School); 2008 (Big Brother Africa – Season 3, Channel O Awards)
  • Norway: 2006 (Tamasha la CARE, Oslo); 2009 (Ziara ya Khaya Khaya)
  • Tanzania: 2006 (Music May Day); 2009 (Bongo Star Search); 2010 (Fiesta Fit Program); 2017 (Komaa Concert)
  • Uganda: 2005 (Lugogo Stadium – Wakilisha walitumbuiza kwenye uzinduzi wa albamu ya Blu3)
  • Marekani: 2012 (Detroit na Los Angeles – chini ya International Visitors Leadership Program - IVLP)
  • India: 2024 (Suraj Kund International Crafts Mela)
  • Mabalozi: 2008 (Kwa Waziri Mkuu wa Norway Jens Stoltenberg); 2013 (Kwa Balozi wa Marekani nchini Tanzania)

TUZO NA HESHIMA

  • 2008: Channel O Music Video Awards – Mshindi: Best African East | Nominated: Best Duo/Group, Best Hip Hop Video (ZERO)
  • 2008: World Hip Hop Awards (Nigeria) – Nominated (ZERO)
  • 2008: Kilimanjaro Music Awards – Best Rapper (ZERO)
  • 2009: Channel O Awards – Best Dance Video (Attention Please)
  • 2022: COSOTA Honorary Award – Kwa mchango wake mkubwa kwenye muziki wa Tanzania

MIRADI MAALUM NA UTETEZI

  • 2000: Utafiti wa UNICEF kuhusu muziki wa hip hop Wilaya ya Temeke
  • 2009: UNDP – Hotuba & burudani kwenye uzinduzi wa mradi wa uchaguzi Tanzania
  • 2012: IVLP (Marekani) – Aliiwakilisha Tanzania katika mradi wa kujifunza kuhusu hip hop na uongozi kijamii
  • 2015: Save the Children – Alikuwa Executive Producer wa wimbo & video SHARIFA kuhusu ndoa za utotoni
  • 2018: Norwegian Church Aid – Executive Producer wa kipindi cha TV kuhusu usafi (Kibuyu Chirizi)
  • 2025: Mradi wa ILO kwa ushirikiano na AU – kuhusu ajira yenye staha kwenye sekta ya ubunifu Afrika

MUZIKI WA ASILI NA MCHANGANYIKO

  • 2005: Alianzisha kundi la Mshumaa Gizani linalochanganya muziki wa hip hop, ngoma za asili, sarakasi na maonesho ya moto. Albamu yake Khaya Khaya ni mfano wa mchanganyiko wa kiutamaduni – ikiwa na lugha ya Kiswahili, Kifaransa, Kinorwe, Kimatengo na Kiingereza.

AINA ZA MAONESHO

  • Bendi kamili (zaidi ya watu 7)
  • Seti ya DJ
  • Hip hop ikichanganywa na ala za kitamaduni
  • Maonesho ya beatbox live

LUGHA ANAZOTUMIA KATIKA SANA

Kiswahili, Kiingereza, Kinorwe, Kifaransa, Kimatengo



USHIRIKIANO MAARUFU

  • Wasanii: Dark Side of the Force (DSF), Anania, Bob Rudala, CBH
  • Mtayarishaji Mkuu: Sigbjorn Nedland

VIPAJI NA MAJUKUMU MENGINE

  • Mcheza dansi, Muigizaji, Mtoa Hamasa
  • Mtayarishaji wa vipindi vya TV & Redio
  • Mwandishi wa filamu na tamthilia
  • Muelimishaji kuhusu UKIMWI
  • Legacist – Mrithi wa sanaa ya kizazi

UONGOZI NA UANACHAMA

  • Makamu Mwenyekiti: Tanzania Urban Music Association (TUMA)
  • Mjumbe wa Bodi: Tanzania Music Rights Society (TAMRISO)
  • Mjumbe: Shirikisho la Muziki Tanzania (TMF)
  • Rais: Chama cha Wanamuziki Tanzania (TAMUCA)
  • Balozi: Mradi wa wanawake 54 kutoka nchi 54 za Afrika – mwakilishi pekee kutoka Tanzania (kwa ubunifu wa Queens of TOGATA, waliokuwa waimbaji wa Lucky Dube)

NDOTO YA USHIRIKIANO

Kushirikiana na Busta Rhymes – ndoto ambayo kwa kiasi ilitimia alipoonana naye mwaka 2009 na kusaini Biblia yake kama ishara ya ahadi na shukrani.



MITANDAO YA KIJAMII & MAWASILIANO

  • YouTube: Witnesz Kibonge Mwepec
  • Instagram: @witnesz.kibongemwepec
  • TikTok: @witnesz_kibonge_kibongemwepec
  • Online Stores: WITNESZ KIBONGE MWEPEC
  • Booking Email: kibongemwepec@gmail.com
  • Simu: +255 753 32 000 9



Maoni 1 :

  1. Ningependa kumpendekeza mmoja wa wazimu wanaoheshimika zaidi wa wakati wetu. Ni mtu ambaye amewasaidia watu wengi jijini wakati wa hali ngumu.

    Baadhi ya watu hata humwita "mungu mdogo" kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kiroho na jinsi anavyowasaidia wale wanaomjia kwa ajili ya mwongozo.

    Unaweza kumtumia ujumbe kwenye WhatsApp: +2349046229159
    Barua pepe wightmagicmaster@gmail.com

    Tafadhali zungumza naye kwa heshima na ueleze hali yako wazi, naye atajitahidi kukusaidia.

    Anatoa mwongozo wa kiroho na usaidizi kwa hali tofauti, ikiwa ni pamoja na:

    • Masuala ya mapenzi na uhusiano, ikiwa ni pamoja na kusaidia kuungana tena na mpenzi wa zamani.

    • Kurejesha ndoa na mahusiano yenye matatizo.

    • Maombi na mila za kiroho kwa ajili ya ulinzi na mafanikio.

    • Tiba za mitishamba za kuponya VVU, saratani, malengelenge.

    • Maombi ya uzazi na usaidizi wa kiroho kwa wanandoa wanaotaka kupata mimba katika wiki chache.

    • Uwezo wa Telekinesis. Uwezo wa kubadilisha umbo.

    • Tambiko na maombi ya utajiri wa papo hapo.

    • Msaada wa kiroho katika hali ngumu kama vile kesi za mahakamani, kurejesha mali iliyopotea, na changamoto zingine za maisha.

    Watu wengi wamepokea msaada na mwongozo kupitia kazi yake ya kiroho.

    JibuFuta