Riwaya *SITAKI KUOGA
WhatsApp: +255(755-399-075)
sehemu ya mwisho kabisa inayohitimisha simulizi yetu ya ```SITAKI KUOGA```
~Ilipoishia~
MARIETA alimjibu naomba niolewe na mwanao ...........
*Endelea*
Mwinyi alistaajabu jambo alillo omba msichana yule kisha alishusha pumzi na kuzima ghafla kama MTU aliyepungukiwa maji mwilini. Hatimaye wakati anatafuta lakumjibu punde so punde alikuja Dada wa kaka NORI. Alifika pale kakuta wanatazamana na hatimaye aliwauliza kuhusu ukimya ule.
Pia Dada wa NORI alistaajabu kisha akasema ndugu yangu hataki kuoga halafu unamtaka na itakuwaje jambo hili maswali mengi yalisisitizwa mahala pale wakuu wa baraza walibaki wakistaajabu. Lakini binti MARIETA hakukata tamaa aliendelea kusisitiza huku akifichua siri kwamba na mimba amebeba. Jambo lile liliendelea kuwasfaajabisha mno. Punde si punde aliingia mtoto NORI mahala pale akiwa kishavalia mavazi ya sherehe yaani harusi ambayo inayotalajiwa kufungwa. Alipofika mahala pale alibaki ameduwaa mwili ulimpata ganzi na hatimaye alidondoka chini.
Baada ya muda mfupi kupita na huduma ya kwanza kuisha NORI aliamka kisha akaketi na kuuliza swali kwa baba yake *hivi baba mwanamke ambaye unatarajia ni huyu au mwingine* Baba yake alijikuta yupo kimya kwa muda mfupi kisha akasema *muda unaelekea ukingoni shughuli ndio inachangamka na mrembo hayuko sasa si bora umwoe huyu* Jambo lile liliwashangaza wengi na hatimaye wakuu wa baraza wakapitisha jambo lile. Binti MARIETA aliruhusiwa pale pale aende kujiandaa kwa ajili ya harusi.
Hatimaye muda ulipowadia alijisogeza karibu na mume wake wakati wakumfungua na kelele za vigeregere kuendelea NORI alijikuta anapiga kelele za kuogofya ```baba hiki miye si HUSU huyu mwanamme kabisa``` mbona kunitia laana baba angu. Watu waliokuwa kwenye chereko lile walizima mziki wakitizamana. Ila MARIETA ambaye ni HUSU kavaaa kinyago kwaa ajili ya kuwa alikuwa anamtafuta mwanamme ambaye yuko kamili. Alishusha kinyago chake chini kisha kamtizama NORI na kumwambia *nimekupata wa Maisha wa kudumu nami Katika shida na raha*. Wote walistaajabu jambo lile na pale pale alipokuwa Katika mshangao maji yaliletwa mbele yake kama ndoo tatu hivi kubwa zilizo jaa na baada ya pale mwendesha chereko ile alimsihi MARIETA amwagie maji mumewe ishara ya upendo maana Katika siku ile, maana tangu alipofariki mama ake na kumpa wosia hakugusa maji.
NORI alijikuta anaanza Julia machozi na huzuni ulimtawala machoni alimpiga kelele nzito kama simba amekosa nyama porini. Na baada ya pale aliinama chini kisha akamwambia baba ake ```SIFATI KUOGA``` Niwache lakini. Baba hakusikia maamuzi ya mwanae na hatimaye maji yalimwaga mwili mzima wa NORI baada ya shuguli ile kuisha ..mwili wa NORI ulianza kumomonyoka kama udongo juuu hadi chini mwisho kabisa ukawa udongo Katika sherehe ile ilikuwa ni moja ya ajabu kabisa wote walikimbia huku na kule sherehe ilikuwa vituko ndege waliruka angani na vyura walitambaa ardhini. MARIETA alimwangalia baba wa NORI kisha akamwambia baba *jambo LA mwanao lilikuwa kweli* bab alimjibu tusilaumiane yashatokea. Mam yake NORI baada ya muda ule kupita alitokea mahala pale kisha kawambia *mtoto akikuomba jambo na kukusihi sanaa usidhubutu kumakatalia kwani tabia ngozi ya mwili kamwe huwezi kuibadili*
Alitoa laana juu ya MARIETA kwamba hutokaa kugusa maji wala mwanao pia kwani hii ndio tabia na hutoibadili Maisha .MARIETA aliogopa snaaaa na kusema baba umeniponza kweli Tabia ngozi ya mwili kamwe huwezi kuibadili. Aliichukua ndoo na kukusanya udongo ule...................m...
MWISHO.
Maoni na ushauri yanahitajika toa maoni yako kupitia
WhatsApp +255-755-399-075
Instagram
@officialnest1
Facebook @nest delicious
Asanteni tukutane tena Katika story nyingine.
Hakuna maoni