CHID BENZ: TALE ANAJIPENDEKEZA KWANGU

Rapper Chid Benz a.k.a King Kong ambaye kwasasa anafanya vizuri kupitia wimbo wake mpya uitwao Chuma ambao amemshirikisha Rayvan wimbo uliopikwa na maproducer wa wili Mr T Touch na Leizer ndani ya Wasafi Record amesema "Tale anajipendekeza kwake"

Kupitia The Play List ya Times Fm Chid amesema hayo ikiwa ni ishara ya kutorudi nyuma na kusonga mbele kupitia muziki wake
Ikumbukwe kua Tale ndie ambaye amemsadia Chid kurudi katika muziki wake na afya pia. "Kunawakati mi nasemaga Boss Tale anajipendekeza kwangu hivyo kama mtu anapesa zake hana shida yoyote lakini anajipendekeza kwangu kwanini mimi nisijishushe?" Alisema chid benz

Pia amemtaja Juma Nature, Prof Jay, Mr Blue na marehemu Ngwea pamoja Ranga kua ni wasanii ambao anawakubali sana. Na amekomaa na kauli yake ya wasanii ambai wametengeneza kuwa yeye hakuna msanii wakufananishwa naye kwenye muziki wa kuchana kwakua yeye anamiliki Tuzo tano na hakuna msanii wa hip hop ambaye amewahi kuchukua tuzi Tano

Post a Comment

Hakuna maoni