BARUA KWA AMBWENE YESAYA (AY)

Awali ya yote ningependa kutanguliza heshima yangu kwako Ambwene Yesaya (AY), bila shaka naamini utakua mzima wa afya njema na nikupe pole kwa shughuli za kila siku za ujenzi wa taifa letu changa la Tanzania.

Napenda kuchukua fursa hii pia kukupongeza na kukushukuru katika harakati zako binafsi za kuusukuma muziki wa kizazi kipya nchini kwa connection ambazo umeweza kuwaonyesha baadhi ya wasanii wa Tanzania.

Dhumuni la kuandika barua hii ni kukueleza machache kuhusu muziki wa bongo flava na  inawezekana ulishaambiwa lakini si vibaya na mimi nikakukimbusha kwa nafasi yangu ili kutilia mkazo katika hili.

Nimeamua kuandika barua hii kwa sababu kuu tatu, kwanza wewe ni mmoja kati ya wakongwe kwenye hili game la muziki wa bongo flavour, pili umekua mtu wa tofauti sana katika harakati za muziki kwa Tanzania na nje ya Tanzania na tatu ambapo ndipo palipo nifanya kushika kalam na karatasi ni vile ulivyo na connection kubwa ya muziki nnje ya bongo.

Kaka nikiangalia wakongwe kwenye hili game la muziki wa Tanzania wengi wanakimbilia kwenye Siasa jambo ambalo sielewi ni kwanini wameamua kufanya siasa na kuuikimbia muziki wakati bado tunahitaji uwepo wao ili kuinua muziki wetu na kuutetea pia kutokana na magumu mengi walio pitia na bado tunahitaji busara zao, kuna makala niliandika kuhusu hili suala la wasanii kukimbilia dodoma na kuutelekeza muziki maana sioni kinachowasukuma kwenda huko wakati huku tu ni majanga na katika makala yangu nikatolea mifano kwa kina Jet Lee na Jack chain wao wamefungua academy baadaya ya kustaafu ili kuendeleza sanaa kwa vizazi na vizazi.

Ombi langu kwako kaka naamini unaweza kwa asilimia 100 endapo ukaamua kuweka nguvu zako katika muziki wetu pendwa wa bongo flava  kuusukuma kwa kupitia njia uzijuazo wewe ili tupate kufanya vizuri na nnje pia.

Sitaki kuamini kama ni kweli lugha inatukwamisha wakati kuna wasanii washapenya na wanafanya vizuri ukiwepo wewe mwenyewe AY, Diamond Platnum, Vanessa Mdee na baadhi wanao onekana kuonesha nia, hata hivyo mbona kuna watu wanafanya poa bongo tena kwa lugha tusizo zielewa na tuna wakubali wakiwemo kina Sarkodie wa Ghana watu wa South Africa Nigeria na sehem nyingi.

nikiwaangalia baadhi ya wasanii Tanzania wanauwezo mkubwa sana wa kuimba lakini tatizo ni wasimamizi njaa wasio jua muziki ndio huwapoteza mbona nikimsikiliza Wizkid wa Nigeria na Rich Mavoko bongo naona mavoko mkali sana.

Sio siri kunawakati mwingine natamani nikushawishi ustaafu muziki kabisa lakini usimamie muziki wa bongo kwa kuwashika wasanii mikono na kuwaonyesha njia sahihi za kupita kabla tamaa za kifisadi za siasa hazijaingia kichwani mwako, naamini unaweza ukawa kumbukumbu kubwa kwa vizazi na vizazi ndani ya muziki wa bongo flavour.

wako katika ujenzi wa Taifa Gadi Mlwilo (gami dee)

Post a Comment

Hakuna maoni